Mshahara unaotosheleza ni upi?

Hajulikani

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
273
248
Wadau tujadiliane humu, inasemekena wafanyakazi hasa wa uma wanalipwa mishahara ambayo haitoshelezi kumwezesha mfanyakazi kulisha familia, kupeleka watoto shule, kujenga nyumba na kuwa angalau na kitega uchumi.
Je ni Mshahara kiasi gani unaoweza kutosheleza mahitaji hapo juu na kumfanya mfanyakazi kuishi maisha ya staha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok.
Sio kwamba mishahara haitoshi, ila tu, watanzania wengi hasa tukiongelea wafanyakazi hatuna elimu ya Mambo ya fedha ( financial education),:hivyo kushinda kutumia ipaswavyo mishahara yetu. Mfano kwenye upande wa bajeti ya pesa tunazopata watu wengi tunashindwa hapa na matokeo yake tunabaki kulaumu, lakini pia wafanyakazi wengi tunategemea mishahara tu pasinakuwa na njia nyingine za kutuingizia kipato, mfano mtu ni mwalimu wa shule ya msingi anaelipwa laki 3 kwa mwezi, hiyohiyo pesa ale, avae, pengine alipe kodi, michango ya kwenye harusu, mara kwao wanahitaji. n.k. HIVYO SHIDA SIO MISHAHARA SHIDA NI SISI WENYEWE. Akhsante.
 
Robert Kiyosaki aliandika kwenye kitabu chake cha Rich dady Poor dady kwamba Even the high paid slave is still a slave.
 
Back
Top Bottom