Julai 2017: Nyongeza za mishahara na kupandishwa vyeo - Kilio cha Watumishi wa Umma

Brilliant internationary

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
301
193
Kwanza kabisa niwashukuru wafanya kazi wote mnaendelea kuchapa kazi japo kamshahara kadogo sana lakini leo nimeamua kumwambia mheshimiwa kuwa wafanyakazi wote tumekuchoka na kama hali hii itaendelea 2020 utaisoma namba mwenyewe.

Nenda ukamuulize mzee JK pesa alikuwa anazitoa wapi na wewe ufanye kama yeye.

====
Mei 01, 2017
Kwa watu mnaofuatilia kwa makini mtakua mmemsikia mkuu wa kaya alisema kuanzia mwaka unaokuja atapandisha mishahara na kushughulikia promotions za wafanya kazi ikiwa ni pamoja na kuajiri wafanyakazi wapya 52 elfu. Sijasikia mahali popote katika hotuba akitamka neno "MWAKA WA FEDHA" wala "MWAKA WA BAJETI" kama ambavyo tumezoea kuwasikia wanasiasa wengi wawapo majukwaani.Hapa kwa mawazo yangu mukulu alijua kua anaongea na watu anaowafahamu vizuri, anawaelewa vyema watu wake.

Hotuba yake imejaa matumaini kweli kweli,lakini bado hotuba hiyo haijaipiku ile ya mara ya kwanza 2015 wakati anahutubia bunge, ile hotuba ilijaa matumani mpaka iliwaliza baadhi ya watu lakini mpaka hapa tulipo muda unazungumza hivi sasa. Wale tunaojishughulisha na siasa tunazifahamu techniques za wanasiasa wawapo majukwaani.

Naapa kabisa kwa yakini ya nafsi yangu ikifika July mosi 2017, hotuba hii ya leo ikaanza kutekelezwa wala hakuna atakayenishauri juu ya msimamo wangu wa kuandika historia mpya ya kua mwanachama mpya wa chama cha mapinduzi.
 
Habari ambazo hazijadhibitishwa na jamaa angu yupo Hazina inasemekana mishahara inashushwa,mwaka huu maeneo yote mshahara uwe laki nne kwa mwezi
Haina shida na kama kila kitu kinashuka kwa asilimia hiyohiyo, wanadai nia itauzwa mia8 tu. Unga kilo mia 350.
 
nyongeza ya mshahara hakuna acha kazi kuna vijana wengi wako mtaani wanaitamani hiyo kazi yako wako radhi kulipwa hata laki kwa mwezi
 
kuongeza mshahara mkuu msahau na hal mbaya ya uchum unaoendelea huu..mpk mwez wa saba mkuu biashara ,makampun mangap zitakuwa zimefungwa nazikifungwa kodi atapata wap za kuwaongeza nyie mishahara.so mkuu hal ndo iyo iyo hmna cha mshahara wa ajira iv karibun..ila polen sana..
 
Kwanza kabisa niwashukuru wafanya kazi wote mnaendelea kuchapa kazi japo kamshahara kadogo sana lakini leo nimeamua kumwambia mheshimiwa kuwa wafanyakazi wote tumekuchoka na kama hali hii itaendelea 2020 utaisoma namba mwenyewe nenda ukamuulize mzee JK pesa alikuwa anazitoa wapi nawewe ufanye kama yeye.

Khaaaaa......kwahiyo akiongeza mtamsamehe na kutokuisoma namba....??? Hebu fikiria tena.......
 
Back
Top Bottom