Mshahara serikalini wapendekezwa:Kima cha chini 100,000/-
Na Reuben Kagaruki
BARAZA la Majadiliano na Kamati ya Utumishi wa Umma, limewasilisha mapendekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bibi Hawa Ghasia, likipendekeza kima cha chini cha mshahara kwa mtumishi wa umma uwe sh. 100,000.
Kama Bibi Ghasia ataridhia mapendekezo ya Baraza hilo, ambalo limeundwa kisheria kujadili maslahi na ustawi wa wafanyakazi katika utumishi wa umma, kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa Serikali kitakuwa kinatofautiana kwa sh. 10,000 na cha mtumishi wa ndani anayefanya kazi kwa Balozi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bibi Anastasia Mmuni, alisema mapendekezo hayo yana unafuu ikilinganishwa na kima cha chini cha sh. 84,740 kilipitishwa katika bajeti ya mwaka huu.
Bibi Mmuni alisema kwa mujibu wa sheria, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwa waziri mwenye dhamana ya utumishi, ili kupata baraka na kwa kuzingatia taratibu hizo, mapendekezo hayo tayari yamewasilishwa kwa Bibi Ghasia.
Alisema Baraza lilipokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo iliyoundwa Septemba 14 mwaka huu na kukubaliana nayo juu ya nyongeza ya kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa mwaka 2007/08.
Alipoulizwa kama mapendekezo hayo yanaendana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa alipoingia madarakani kuwa anataka kuona mfanyakazi wa umma anapotoka ofisini kwenda kula anarudi akiwa amebadilisha nguo kutokana na kupata maslahi bora, Bibi Mmuni alikiri kuwa kiasi hicho hakitoshi.
"Baraza linajua kiasi hiki hakitoshi, lakini ni bora kuliko kubaki kile kile kilichopitishwa kwenye bajeti," alisema Bibi Mmuni. Alipoulizwa kama haoni kuwa Baraza lake litakuwa linajiaibisha mbele ya jamii kwa kupendekeza kiasi ambacho linafahamu hakitoshi, Bibi Mmuni alikataa hilo.
"Tumejiaibisha kwa lipi? Nadhani hatujajiaibisha," alisema na kuongeza kuwa kamati ndogo iliyotoa mapendekezo hayo ilikuwa na wataalamu mbalimbali iliyoangalia mambo mengi kuhusiana na maslahi ya mfanyakazi wa umma.
Alipoulizwa kama kiasi hicho kilichopendekezwa hakitaibua mvutano baina ya vyama vya wafanyakazi na Serikali, alisema: "Kwenye Baraza tulikuwa na uwakilishi sawa, nusu ya wawakilishi walitoka vyama vya wafanyakazi ambao wameridhia kiwango hicho." Alisema wamependekeza wafanyakazi wa kima cha chini wasikatwe mishahara.
Katika madai yao wafanyakazi wamekuwa wakisisitiza kima cha chini cha mtumishi wa umma kiwe sh. 315,000. Hivi Karibuni Serikali ilitangaza viwango vipya vya kima cha chini kwa watumishi wa sekta ya binafsi ambavyo viligawanywa katika makundi wa juu ukiwa ni sh. 350,000.
Katika makundi hayo wafanyakazi ambao wanapata kima cha chini kinachokaribiana kabisa na sh. 100,000 zilizopendekezwa kwa ajili ya watumishi wa umma ni wafanyakazi wa ndani na wahudumu wa baa.
SOurce: Majira