Mshahara kima cha chini wizi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshahara kima cha chini wizi mtupu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Apr 19, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,783
  Trophy Points: 280
  KONA YA MLALAHOI: Mshahara kima cha chini wizi mtupu

  Na Adam Mwakibinga
  Mwananchi

  CHANGALAMACHO ni mlalahoi anayefanya kazi moja muhimu sana na yenye kuhitaji uvumilivu wa hali ya juu, kwa kifupi ili uweze kufanya kazi anayofanya Changalamacho unatakiwa uwe na moyo kwelikweli kutokana na mazingira ya kazi yenyewe (UALIMU).

  Wako wanaoiita kazi hiyo ni kazi ya wito nami nakubaliana nao kwa asilimia zote kwamba ni sahihi kuiita kazi ya wito kwani bila kuwa na wito hutofanya kazi hiyo.

  Mshahara anaopata Changalamacho anasema ni ule wa kima cha chini yeye mwenyewe amediriki kuutaja waziwazi bila kificho ili walalahoi wenzake tumuhurumie na hana kitega uchumi chochote anachokitegemea kumuongezea kipato zaidi ya huo mshahara anaopata.

  Anasema mshahara anaopata ni shilingi laki moja na elfu thelathini na tano (135,000), lakini mpaka kuupata lazima mbinde ipite, amekuwa akijaribu kujibana lakini wapi bado ngoma nzito kwake.

  Anajuta kuifahamu kazi ya ualimu, pamoja na kwamba ndio mtambo wa kutengeneza kila mtaalamu duniani kote, hilo halina ubishi.

  Changalamacho ana watoto watatu wanaomtegemea mbali na watoto hao pia ana mke ambaye hana uwezo wa kufanya kazi kwa hiyo naye ni tegemezi wake, vilevile anakaa na mama yake mzazi ambaye umri wake afaa kuitwa ajuza.

  Ni mkazi wa mjini tena jijini na si kijijini hivyo amepanga vyumba viwili kimoja analala yeye na mkewe na kingine wanalala watoto wake watatu wote wa kike pamoja na bibi yao.

  Mlalahoi Changalamacho anasema kila akijitahidi kupanga bajeti ya nyumbani kwake hupata ugonjwa wa moyo kwani haipangiki na inamuumiza kichwa kutokana na ukweli kwamba mshahara anaoupata haukidhi haja ya familia yake.

  Upangaji bajeti yake kwa mwezi ni kama ifuatavyo: kodi ya vyumba viwili alivyopanga ni shilingi 30,000 kila chumba ni shilingi 15,000 kwa mwezi nyumba aliyopanga iko nje kidogo ya jiji, mchele kilo 10 ni shilingi 12,000 kilo moja ni shilingi 1,200, sembe kilo 10 ni shilingi 7,000 kilo moja ni shilingi 700, mkaa gunia moja shilingi 18,000, sukari kilo tano shilingi 6,000 kilo moja ni shilingi 1,200.

  Maharage kilo tano shilingi 6,000 kila kilo moja ni shilingi 1,200, mafuta ya kula galoni moja shilingi 3,000, chumvi paketi 2 shilingi 400, viberiti vya shilingi 480, sabuni ya kufulia(unga) nusu kilo shilingi 1,200, mche mmoja wa sabuni ya kusugua(hutumia kwa kuogea na kuoshea vyombo) shilingi 1,200, mafuta ya kupaka kopo moja shilingi 1,000. Kuchangia ankara ya nishati ya umeme wa Luku ni shilingi 10,000 kwa mwezi.

  Dawa ya meno gramu 80 shilingi 650, nauli kwa ajili ya usafiri wa daladala shilingi 14,000 kwa siku ni shilingi 700, shilingi 350 kwenda kazini na shilingi 350 kurudi nyumbani hii ni kwa Changalamacho peke yake na ile ya watoto wake watatu ni shilingi 12,000 kwa mwezi yaani kila siku mtoto mmoja huondoka na shilingi 200 shilingi mia moja kwenda na mia moja nyingine kurudi, kwa maana hiyo watoto hawa huwa hawali mchana mpaka watakaporudi nyumbani halikadhalika Changalamacho mwenyewe.

  Mpaka hapo mlalahoi Changalamacho amebakiwa na shilingi 6,270 kwa ajili ya kununulia dagaa, nyanya, vitunguu na mchicha japo kwa wiki mara moja, bado hajaweka karo za watoto, mavazi na akiba ya pesa kwa ajili ya matibabu na dharura nyingine, hata hivyo anasema kiasi cha vyakula pia amevibana hulazimika wakati mwingine kukopa madukani vinapokwisha kabla ya mwezi kumalizika.


  Changalamacho anamuomba mbunge wake ambaye yeye hupata kiasi kama hicho cha mshahara wa kima cha chini (135,000) kwa ajili ya posho ya siku moja tu akiwa bungeni amsaidie kupanga bajeti angalau isaidie kumaliza mwezi.Afanaleki eti binadamu wote ni sawa! Amani juu yenu. Kwa maoni mawasiliano ni 0756 202532.

   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha SANA
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huyu anamudu vipi kama siyo kwa kudra ya Muumba wake? Lakini viongozi wetu waone aibu wawatendee haki wananchi.Kiwango cha posho ys siku moja ni vipi kinategemewa kumfaa mtu mwenye familia kama mshahara wa mwezi? Ni vigezo vipi hutumika kupanga hizo posho?
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Yaani dada yangu hatuna viongozi bali tuna wezi watupu wenye kujijali wao wenyewe. Kama mbunge analipwa milioni 7 kwa mwezi na bado anasema hazitoshi aongezewe anamwonaje huyu anayelipwa 135,000? Ubinafsi unatumaliza Africa. Ndo maana hata ufanisi wa kazi unakuwa kidogo, watu wamekata tamaa, ni kwamba tu hawana namna nyingine ya kufanya. Kweli huu ni wizi mtupu!
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yaani hiyo ni very simple analysis lakini inatupa basis za kima cha chini sasa serikali yetu inatumia hesabu gani kupata kima cha chini? Unajua hawa viongozi ukiwambia wajustify uhalali wa kipato cha chini na matumizi yake wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu.
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hali inatisha nyumbani! kama mwalimu analipwa hivyo hii ni hatari. 135,000Tshs, ambao ni mshahara wa siku wa mtu huo.
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hebu tujaribu kutofautisha hapa vitu viwili:
  - Kima cha chini nini maana yake? Ninavyoelewa (na mi si mchumi) inabidi i-reflect the earning ability of the country which includes also GDP ya Tanzania. Hivi tunazalisha nini ili tuweze kudemand mshahara mkubwa zaidi? Je average Tanzanian (not spoilt salaried Tanzanians ambao wanataka mamilioni katika mshahara lakini nazungumzia 80% ya watanzania wanaotegemea kilimo) wao wanapata kiasi gani kwa mwezi? From what most of you are claiming, people are starving in Tanzania because the average farmer doesn't see 135,000 shs kwa mwezi. Lakini that is not the case! So then there is a huge discrepency between Dar-es-Salaam people's view of money and people in rural areas.

  - Wishes, aspirations and illusions - sisi tunataka kuishi maisha ambayo realistically we cannot afford. And this goes to the Parlamentarians, leaders of this country. Hivi leo kila mtu anataka gari, aendeshe gari etc. Sasa tunazalisha nini ili tuweze kuwa na uwezo wa kuishi maisha kama wajapani na wamarekani? Eti wengine wanasema mhadhiri na PhD analipwa ONLY 1.2 million kwa mwezi. ONLY? Eti anastahili mshahara zaidi kwa sababu amesoma zaidi? Really? Mchango wake nini katika uchumi ? Je amefundisha na kutoa wataalam wangapi? Au anataka tu alipwe mshahara kama reward kwa sababu amesoma sana? Same goes for the teachers. Kama anaona mshahara mdogo akatafute kazi nyingine, afungue biashara. Hii ya kutegemea mishahara kutoka serikalini ni diesease and creates falso impressions.

  We have to change our mindset and scale back our unrealistic expectations and wishes.

  I know that another argument will be mfumuko wa bei which I am ready to argue about but believe me the tomatoes that are sold for several thousand shilings in Dar are not the same in rural areas where you can buy them for substantially less. Na wanaofaidika ni middlemen who rightfully tap into the uneven distribution of income between urban and rural areas.
   
 8. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Susuviri, hii nchi ni nchi ya maziwa na asali. Lakini asali wanailamba wachache, wengi wanaishia kulamba mate ya watu badala ya asali. Mara nyingine hawataki tujue kuwa mzinga una asali kibao ili waendelee kula peke yao. Mwalimu anachoomba ni angalau hiyo pesa anayopata iongezeke kidogo ili imsaidie kuongeza angalau kiasi cha dagaa na maharagwe cha kumfikisha mwisho wa mwezi si zaidi ya hapo.
   
 9. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa mkuu, na mimi nimekuja na radical response kwa sababu naona kwamba tumebaki kutingisha vichwa vyetu na kusema 'tsk tsk' and echo similar sentiments zinazonuka sentiments za ujamaa and other utopia. Lakini hatuangalii chanzo cha tatizo. Tatizo si viongozi kulipwa mshahara mkubwa maana ukiwaambia wabunge na wao watalalamika eti Kenya wanalipwa zaidi, oh mawaziri UK hivi.
  Turudi kwa mwalimu. Swali ni kwamba: je bei ya dagaa na maharage katika miji (not only Dar but urban area) ni sawa na yale ya kijijini? If mwalimu au average Tanzania cannot buy dagaa, what are they eating? Who are the ones who can afford dagaa? Definitely not the ones earning 1.2 million!

  Nasema tatizo tunataka kuishi standrd that we cannot afford (BTW that includes me and my family). We should all scale back and put our energy into production, first and consume only what we can afford.
  Let us move beyond just complaining blindly. Je kima cha mwalimu kitaongezwa na nini? Mimi kama mjasiriamali nitakatwa kodi zaidi eti niongeze mshahara wa walimu, why? Naomba nimshauri huyo mwalimu aache kazi yake ya ualimu afanye biashara au abadili career kama kazi yake hailipi.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu!

  With due respect to your opinion which you are entitled to,nadhani tunachojaribu kujiuliza ni kuwa - uwiano uko wapi katika kugawana keki ya taifa.Kuna disparity kubwa sana kati ya viongozi tena wale waliochaguliwa na wananchi, na wananchi wenyewe, hasa wa kawaida sana mijini na vijijini. Achilia mbali vipato vya wengine wanaojipatia vipato kwa njia nyingine ikiwemo ujasiriamali. Umesema kuwa :

  "Tatizo si viongozi kulipwa mshahara mkubwa maana ukiwaambia wabunge na wao watalalamika eti Kenya wanalipwa zaidi, oh mawaziri UK hivi"

  sioni kama huu ulinganifu wa mapato ya hawa waheshimiwa wa TZ na wa nchi nyingine una msingi sana maana hatuna sababu ku peg mishahara yao na watu wa nchi nyingine maana mazingira yetu ni tofauti kwa vigezo vyote , ikiwemo vile ambavyo ulivizungumzia katika tundiko lako la mwanzo.Isitoshe kama vyanzo vyetu vya mapato ni finyu, uhalali wa kuweka viwango vikubwa sana kwa baadhi na vidogo sana kwa baadhi ni upi? Kama ni basic needs nadhani hii ni haki ya kila binadamu na ndiyo maana watu wengi wana advocate for a living wage na siyo kipato kwa ajili ya self actualisation.Mfano- nini mantiki ya kujipangia posho lukuki - sitting allowances, ilahali mtu unahudhuria vikao hivyo kama sehemu ya majukumu unayolipwa mshahara?

  Ushauri wako kwa waalimu sijui itakuwaje kama waalimu wote wangeamua kuacha ualimu na kuingia ujasiriamali.Kwanza haiwezekani na pili nadhani mgawanyo wa majukumu, na shughuli ni muhimu katika kuendeleza jamii.Pia mwingine atasema kama madaktari wanaona mshahara ni mdogo waende kwenye biashara, je hudumu za tiba itakuwaje au ndo tutarudi nyuma kutafuta huduma za waganga wa jadi?Kimsingi kila kazi/shughuli ni muhimu na kwa msingi huo wahusika wafikiriwe na kulipwa kwa kadri ya stahili ya kuweza kujimudu kimaisha.

  Haya ni mawazo yangu tu kwa kufikiria hali ya kawaida ya maisha yetu bila kuangalia nadharia za kiuchumi na hata suala zima la ajira.
   
 11. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pamoja na hayo ndugu Susuvere, hii nyumba yetu ina baba na mama. Cha ajabu wao wanapenda matanuzi lakini watoto wao wanawaambia wakaze buti. Nafikiri wangeanza wao kuonyesha mfano nafikiri watoto wangejibihave kuendana na maisha ya baba na mama yao. Shida iliyopo ni kuwa hao wazazi wanaishi maisha ya peponi huku wakiwaambia watoto wavumilie shida. Wananunua magari ya kifahari na kujiuzia baada ya miaka miwili kwa bei ya kutupwa. Wamejiuzia nyumba za selikari kwa bei ya kutupwa na kuzipangisha kwa kwa bei kubwa zaidi, wanajilipa ma allowance makubwa kuliko mishahara yao na haikatwi kodi,wanajiuzia migodi kwa bei chee (kiwira), wanaingia mikataba njaa na wawekezaji wa kuchimba madini kisa wamepewa kitu kidogo, wanafuja pesa za wahisani mpaka wanashtukiwa na kudaiwa, wanapora ardhi ya watu maskini kwa kuwalipa fidia kidogo na kuiuza kwa bei kubwa, wanaingia mikataba feki ya kuzalisha umeme na kutuuzia umeme kwa bei ya kutupwa, hawawaelekezi watanzania wapi pana ardhi nzuri ya kilimo ili wahamie huko na kulima badala yake wanawapatia wageni hiyo. Hizo ndizo tabia za baba na mama mwenye nyumba inayoitwa Tanzania. Maana kama ni kuongeza uzalishaji wazazi ndio walitakiwa kuwahimiza watoto na kuhakikisha kuwa kile walichozalisha kinatumika ipasavyo lakini mambo hayaendi hivyo.

  Kuhusu mwalimu kuacha kazi aanze biashara, kumbuka sio kila mtu anaweza kufanya biashara, thats why kuna mambo ya specialization. Tumeona watu wengi walioomba kustaafu kwa hiari na kuanza biashara, baadhi yao walikula mkenge baada ya biashara zao kwenda vibaya.
   
 12. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Andindile mkuu, nimekupata vizuri tu na ndo maana nimesema ni sisi wote hakuna exemption. Na ndo maana nimesema hao waheshimiwa wakiambiwa wapunguze matumizi wataanza kulalama eti wenzao wa Kenya hivi na vile.... ni tamaa. Therefore I am not exempting them from their responsibility. Niko tayari hata kuwatwisha burden ya kuonyesha mfano bora, lakini bado nashikilia bango suala la sis watanzania kuwa na unrealistic needs na hapa naongelea sisi ambao ni wasomi na tunaishi mjini, and we set the trend for the rest.

  Kuhusu mwalimu kuingia biashara nakubali si kila mtu ana uwezo huo lakini ukumbuke pia kuna ishu ya kubadili taaluma yako. Nawajua walimu wengi ambao wana kazi tofauti hivi sasa kwani waliona kazi hii hailipi, wengine ni Personal assistants wengine wako katika NGOs kama administrators na kadhalika.
   
 13. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Salama wakuu,

  Hapa kinachotakiwa kujadiliwa si nani kapata nini au kiasi gani, kwa muono wangu nafikiri kitu cha msingi ni kwamba serikali yetu ijaribu walau ku-play Supervisory role kuwabana hawa ma-middlemen, yaani utakuta kipato kama cha Mlalahoi kikipanda basi trend ya mannuzi ya vitu vingine kuanzia mafuta (Diesel/Petrol), nauli, nyanya, mchele etc vinapanda. Hawa wajasiliamali wanapandisha vitu hivyo, kwa logic yakuwa mshahara umeongezeka. Kwa mantiki hiyo hata lile ongezeko la mshahara linakuwa halipo, na ndipo unapokuja kukutana na bajeti kama za Mlalahoi.

  Ni kweli kabisa kwamba we deserve to earn what we produce, hatuwezi kuwa na mishahara kama ya nchi fulani, wakati hatuzalishi kama wao. Na ndiyo hoja yangu inapokuja kwamba basi serikali ijaribu kuangalia na kuhakikisha kuwa kipato inachokiweka kinakidhi zile BASIC NEEDS, na itafanya hivi kwa ku-control bei ya bidhaa isiwe inapanda kiholela just because mshahara umeongezeka. Hivi sasa kila mtu anawinda kumyonya mwenzake, hakuna the so called service provision, hata huyo mwalimu utakuta anachangisha wanafunzi ili wafanye test siku za jumamosi, kitu ambacho ni sehemu yake ya kazi.

  Thanks
   
 14. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mifisadi yetu kuanzia kesho posho zinaanza kumwagika Dodoma ndio watachoma nyama mnadani na kuongea pumba Kitalani. Mungu atawachapa viboko tu! sasa ngoma iko mahospitalini manesi na wahudumu sio ndio utaharakisha kufa kwa kukosa huduma maana njaa sio nzuri
   
 15. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkereketwa mkuu, naona kuwa sasa we are getting somewhere! Na hao middlemen pia nadhani hawana business sense, kwani wangeshusha bei wangepata pesa zaidi. BUt nakubaliana kuwa serikali lazima iwe regulator lakini isiwe mtekelezaji kama enzi za ujamaa! Na regulation ifanyike kwa kutumia taaluma na facts and statistics siyokwa hisia.
   
 16. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari sana lakini ndiyo hali halisi tuliyonayo Tanzania. Na hii imesababisha sana magonjwa kama ukimwi kuenea. Fikiria unamwajiri leo mtoto wa miaka 22 wa kike kwenda kufundisha shule ya msingi kijijini, na kule kuna watu kama Afisa mtendaji ndiyo wanaoaminika kuwa na pesa vijijini kwani kodi ndogo ndogo zinaishia mikononi mwao. Sasa vijiji vingi ukienda utakuta wale wasichana wamekuwa nyumba ndogo za hao viongozi na wengine kuwa wake wa tatu na tatizo siyo kwa kupenda bali ili wapate chochote katikati ya mwezi. Mwisho utasikia data zinaonesha walimu wanakufa sana na ukimwi, lakini chanzo hawataki kusema. SERIKALI inabidi kuangalia sana hili tatizo
   
 17. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Hapa swali siyo uzalishaji. KAMA ni uzalishaji hakuna anayezalisha kama Mwalimu maana wote tunapita mikononi mwake. Kama WoS alivyosema. Kila kazi ina umuhimu wake. Na sidhani kama swala ni sisi kutaka kuishi standards za maisha ya juu. Susuviri, umasikini ni relative term. 135.000.00 tunaiona nyingi kwa sababu ya umasikini uliotuzunguka. Ninavyoelewa mshahara ni ile pesa inayopangwa kulipwa mtu kutokana na hali halisi ya maisha ya kila siku. Umeona mahesabu hapa..ni kwamba zaidi ya kuwa mwizi huwezi kuishi kwa mshahara anaopewa mwalimu. Kifupi numbers dont add up.

  Serikali yetu ifanye nini? Kama ni kufunga mikanda tufunge wote. Ni uonevu kuassume kwamba mwalimu apewe hizo wakati wewe na mimi tunapewa zaidi. Mfano Germany au scandinavia..tofauti ya mshahara wa mwalimu wa primary na chuo kikuu tofauti ni ndogo. Why? Premise ya kwanza serikali inatambua kwamba wote ni binadamu na mahitaji yenu yanafanana. kama kusomesha watoto, nk. ile tofauti inayokuja ni kuonyesha difference ya academic na merit nyinginezo ambayo si kubwa kiasi hicho. Sasa leo Chitalilo na Mwalimu mkuu wa St. Francis Mbeya..nani anazalisha zaidi?

  Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu. Leo ukimuuliza waziri wa kazi akupe vigezo walivyotumia kuja na kima cha chini. Hakika atakosa jibu. Simply put. Hiyo hela haikuwezeshi kuishi bila kuiba.

  Harafu tusigeneralize. Mkulima ana nafasi yake katika maisha yetu. Mfano..yeye hapati hiyo pesa..lakini analima na chakula hanunui. Akitaka karo ya mtoto ndo hivyo inabidi ahangaike auze kahawa. Ulaya hata subsidy wanapewa. Ni kwa sababu mchango wao unathaminiwa. Kwa hiyo sidhani hapa kama tunalinganisha vyema. Na after all, ndo maana watu tunakwenda shule..tunataka tuimprove maisha yetu. Kama isingekuwa hivyo, Masanja ningebaki Kwimba nalima PAMBA.

  Serikali ikiamua kuweko uwiano sawia..(ofcourse tofauti zitakuwepo tuu) kusudi mwalimu, nesi, mganga, nk wapewe hela ya kuishi. Inaweza. Swala la uzalishaji ndo hapo..mwajiri ndo anakusimamia. Kwa nini private sector watu tunafanya kazi mpaka usiku..na ukiondoka unaondoka na laptop? ni kwa sababu mwajiri anakupa goals ukishindwa mnaachana. Serikalini..kama tunavyojua..ni shamba la bibi...kama serikali ikiamua iwawajibishe wafanyakazi wake..inawezekana sana tuu..Hata mwalimu..hivyo hivyo..ana mwajiri wake..lakini kwa mwendo wa laki moja..ni vigumu..(hata morally) kumuwajibisha mtu...maana hana analolipata kwenye hiyo kazi.

  So the buck stops with the government. Huwezi justify mshahara wa dola mia kwa binadamu mwenye mahitaji kama wewe. Not at all.

  Leo mimi ukinipa mshahara..lazima kwanza niangalie kama unalingana na utaalamu wangu. Mfano..najiuliza..nimeinvest kiasi gani katika elimu niliyonayo? (Kama nimesoma Ivy League-Lol)..bado nadaiwa mkopo..kweli Susuviri..ukinipa dola mia..si ni kutafutana ugomvi mkuu wangu?..Swala la kuzalisha ni lingine kabisa..nipe goals za kuachive..nisimamie vyema...nikishindwa fire me..ila sio hadithi eti unanipa kidogo kwa vile sizalishi..Hiyo utakuwa unanionea.
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Masanja et al.,

  Fairness friends on how the cake is being used! Basi..iwe keki kidogo au kubwa basi tu iwe fair!

  Kwa nini mfano. mshahara wa Mkurugenzi uwe 2.0 na ule wa Mwal. Primary uwe 135,000? yaani mara 15 zaidi?? Why?

  Ingekuwa watumishi wote wawe na mishahara say kati ya 500,000 to 1 m! Yaani mtu uwe Mwal. au nesi au Mkurugenzi au mbunge!

  Yes keki ni kidogo..je ni kwa nini wengine wapate sehemu kubwa ya hii keki kidogo??

  Why??

  Is it fair??
   
 19. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Mkuu hilo ndo tunaliongelea. Na serikali kufanya hili its not a big deal. Ukienda serikalini unakuwa unajua unakutana na nini haswa. Hii ingepunguza rushwa, uzembe na kuiba..maana mtu anaona kabisa..kikipatikana kikubwa..na yeye atakumbukwa..ndo maana watu leo hawana motisha wa kuchapa kazi...kwa sababu Chitalilo darasa la saba ale million saba kwa mwezi..Mwalimu aliyesoma na Chitalilo...ambaye anajua kabisa jamaa alifeli ale laki moja unusu..its not fair..

  Mishahara is not a panacea ya matatizo yetu. But it can make a difference katika perception za watumishi.
   
 20. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Tuna lalamika nini wakati tunawachagua wenyewe. kama wabongo tungepata shida ya kweli kweli tungegeuza mwenendo wetu wa kuangalia vituu kiusanii,
  Tunachagua viongozi kiusanii,tunaishi kiusanii maana tu wepesi wa kusema lakini hatuna vitendo.
  Nguvu ya wananchi iko wapi ya kumtaka Rais ajiudhuru kwa kushidwa kutetea katiba ya nch, kwa kulea mafisadi kama akina Kagoda.Leo hii DPP anathubutu kueleza umma anaoutumikia kuwa hawezi kuishitaki Kagoda hana ushahidi. kama angekuwa muungwana angejiudhuru wadhifa huo hange onekana shujaa vinginevyo naye ni kundi la ufisadi.Hii ndo timu tuliyoweka madarakani na hatuna ubavu wakuwang'oa sisi ni wajinga waliwao kwa hiyo kima wanachotupangia kinatosha so far kwani sisi ni binadamu?
   
Loading...