Mshahara kiasi gani unatosha kwa baba wa familia ya watoto watatu?

Mwasapile

JF-Expert Member
Apr 20, 2020
206
441
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuwa je, kiwango cha mshahara ninachokipata kulingana na majukumu niliyonayo kama kinanitosha, ni baba wa mke mmoja na watoto watatu ambao kati yao wawili wameshaanza shule.

Sasa kila nikipokea mshahara let say tar 01 ikifika tar 03 huwa sina kitu mfukoni, nimefika mahala mpaka nahisi huenda nina changamoto katika matumizi yangu ya pesa lakini nikiangalia sioni popote pesa ilipoenda kwenye matumizi ambayo sio ya lazima.

Kutokana kwamba watu ni wasiri sana haswa kwenye suala la kipato anachopata, imenibidi niulize huku kwamba atleast "Take Home Salary" inatakiwa isipungue kiasi gani kwa mwezi. Ili endapo labda kiasi ninacholipwa ni chini ya hapo niparangane kutafuta ajira mahali pengine.
 
Nafikiri hakuna kanuni moja ila muhimu ni kuwa; mshahara ukiongezeka na matumizi huongezeka hivyo, wengi watakuambia mishahara ya kawaida huwa haitoshi labda wale wachache waliopo kwenye taasisi nyeti au walamba Asali

Mfano: Mtu akikaa kwenye nyumba ya 50,000; mshahara ukipanda atahamia kwa nyumba ya 100,000; kama alikuwa anatembea kwa miguu atanunua pikipiki ambayo inahitahi mafuta na anaweza kuhamishia watoto kwenye shule za English medium na kuboresha msosi kiasi unakuta habakiwi na kitu.......

Mwingine alikuwa na pikipiki atahamia kwenye gari, na nyumba ya laki mbili, na kujitahidi kuvuta familia yake kwa kuwasaidia hapa na pale; si unajua huku Afrika akitoka mmoja Familia yote inamuangalia...nk nk nk
Jitahidi umfungulie wife ka biashara, hata saluni, mama ntilie, Kibanda nk (ila iwe biashara anayoipenda ili asimamie) itakusaidia sana. Mradi wa kufuga kuku ni mzuri pia kama mazingira yanaruhusu... utanishukuru baadae....
 
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuwa je kiwango cha mshahara ninachokipata kulingana na majukumu niliyonayo kama kinanitosha, ni baba wa mke mmoja na watoto watatu ambao kati yao wawili wameshaanza shule. Sasa kila nikipokea mshahara let say tar 01 ikifika tar 03 huwa sina kitu mfukoni, nimefika mahala mpaka nahisi huenda nina changamoto katika matumizi yangu ya pesa lakini nikiangalia sioni popote pesa ilipoenda kwenye matumizi ambayo sio ya lazima.,

Kutokana kwamba watu ni wasiri sana haswa kwenye suala la kipato anachopata, imenibidi niulize huku kwamba atleast "Take Home Salary" inatakiwa isipungue kiasi gani kwa mwezi. Ili endapo labda kiasi niancholipwa ni chini ya hapo niparangane kutafuta ajira mahali pengine.

Mkuu upo wapi Kama upo DSM tumia formula ya kununua vitu vya ndani kea jumla vinavyotosha mwezi mmoja Kama hivi

Mchele kg 25=60k
Unga kg kg 15=25k
Sukari kg 5 =15k
Gas/mkaa 58k-60k
Umeme 20k
Mafuta Lita 5 18-20k
Maharage kg 10-15 =30-40
Maji 10k
Chakula Cha mwezi mmoja Pamoja na Umeme na maji jumla 200k lakimbili

Kila siku unaach nyumbani elfu 10k hii ni hela ya kubadilisha Mboga na vitafunwa na Nauli za watoto kwenda shule Kama wanasoma.

Then mke wako Kama ni Mama wa nyumbani kwa mwezi mpatie hata 40k kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo Kama kusuka n.k na vocha.

So kwa mwezi hesabu inasoma 240k jumla pia tenga 60k hii ni ya emergency kama kuumwa n.k
Total =540k
Hapo nadhani ukiwa na take home Kuanzia laki sita , unaweza kutoa 540k ikatoboa mwezi mzima

Then hiyo 60k
Inayobaki tumia kwa ajili ya Nauli n.k then ile 60k hapo juu Kama mtu hajaumwa acheni ikae bank msiitumie itasaidia Kodi ya pango n.k

Nb hata Kama una Pesa kiasi gani Jenga muunganiko Mzuri na muuzaji wa duka la matumizi unapopokea mshahara Tumia mfumo wa kukopa na kulipa unakopa mahitaji yako yote then ile Ambayo ungemlipa iweke bank then usubiri mshahara uingie usikubali kukaa bila hela bank na usikubali kukaa ndani bila chakula Ahsante

Usalama wa kwanza ni Kuwa na chakula ndani then pesa bank
 
Mkuu upo wapi Kama upo DSM tumia formula ya kununua vitu vya ndani kea jumla vinavyotosha mwezi mmoja Kama hivi

Mchele kg 25=60k
Unga kg kg 15=25k
Sukari kg 5 =15k
Gas/mkaa 58k-60k
Umeme 20k
Mafuta Lita 5 18-20k
Maharage kg 10-15 =30-40
Maji 10k
Chakula Cha mwezi mmoja Pamoja na Umeme na maji jumla 200k lakimbili

Kila siku unaach nyumbani elfu 10k hii ni hela ya kubadilisha Mboga na vitafunwa na Nauli za watoto kwenda shule Kama wanasoma.

Then mke wako Kama ni Mama wa nyumbani kwa mwezi mpatie hata 40k kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo Kama kusuka n.k na vocha.

So kwa mwezi hesabu inasoma 240k jumla pia tenga 60k hii ni ya emergency kama kuumwa n.k
Total =300k
Hapo nadhani ukiwa na take home Kuanzia laki sita , unaweza kutoa 300k ikatoboa mwezi mzima

Then hiyo 300k
Inayobaki toa 250k kwa ajili ya Nauli au mafuta na chakula chako Cha mchana then 50k weka bank itasaidia Kodi
Sijaona kodi hapo..
 
Mkuu upo wapi Kama upo DSM tumia formula ya kununua vitu vya ndani kea jumla vinavyotosha mwezi mmoja Kama hivi
Mkuu, mpangilio wako mzuri ila hesabu imekuponyoka kidogo.

Pale juu kwenye vitu, tayari ni 240k, ukiweka na hiyo 10k ya kila siku, jumla ni 540k, weka sasa na hiyo 40k ya wife, 250k ya kwako binafsi!

Huwezi kuweka 50k kwaajili ya kodi kwa mwezi, nyumba gani hiyo?

Tayari una 830k, sasa weka na 300k ya kodi.

Take home ya kuanzia 1,000,000 ni reasonable kama unataka kuishi maisha hayo na kwa hesabu hiyo!

Kinyume chake, kila take home inafaa tu, ndio maana kuna level tofauti za kimaisha!
 
Mkuu upo wapi Kama upo DSM tumia formula ya kununua vitu vya ndani kea jumla vinavyotosha mwezi mmoja Kama hivi

Mchele kg 25=60k
Unga kg kg 15=25k
Sukari kg 5 =15k
Gas/mkaa 58k-60k
Umeme 20k
Mafuta Lita 5 18-20k
Maharage kg 10-15 =30-40
Maji 10k
Chakula Cha mwezi mmoja Pamoja na Umeme na maji jumla 200k lakimbili

Kila siku unaach nyumbani elfu 10k hii ni hela ya kubadilisha Mboga na vitafunwa na Nauli za watoto kwenda shule Kama wanasoma.

Then mke wako Kama ni Mama wa nyumbani kwa mwezi mpatie hata 40k kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo Kama kusuka n.k na vocha.

So kwa mwezi hesabu inasoma 240k jumla pia tenga 60k hii ni ya emergency kama kuumwa n.k
Total =300k
Hapo nadhani ukiwa na take home Kuanzia laki sita , unaweza kutoa 300k ikatoboa mwezi mzima

Then hiyo 300k
Inayobaki toa 250k kwa ajili ya Nauli au mafuta na chakula chako Cha mchana then 50k weka bank itasaidia Kodi
Hesabu imejaa uwongo,haina uhalisia.

Umesema baada ya kununua kila kitu akaweka ndani atakuwa ametumia 200k,alafu awe anaacha hela ya mboga na nauli za watoto kila siku elfu 10. Hiyo 10k peke yake Mara mwezi ni laki 3. Jumlisha na hiyo laki mbili,inakuwa laki 5. Katika hesabu yako ya laki 6 inabaki laki moja.

Hapo sijajumlisha hesabu zingine ulizoandika hapo,maji,umeme,nauli,Kodi 50k na bla bla zingine.

Rudi edit,Kisha mshauri tena.
 
Kuna mtu aliwahi ku comment kuwa Mshahara hautoshi.

Unachotakiwa kufanya ni kupitia upya matumizi yako na kupanga upya kwa kushirikiana na Mkeo.

Pia ukiweza mfungulie Biashara Mkeo au wewe mwenyewe kufanya baada ya muda wa Muajiri kuisha Jioni ili kuongeza kipato.

Pia wakati huu wa mavuno unaweza kuagiza mazao ya chakula kutoka mikoani ili kupunguza gharama.

Mfano bei ya sasa ya Mchele wa Kutoka Kyela/Kamsamba ni shilingi 33,000 - 39,000 kwa debe la kilo 20.

Unaweza kupunguza gharama kwa kununua debe kadhaa ambazo zitaweza kukusogeza miezi kadhaa.
 
Back
Top Bottom