Mshahara August 6

mtambobajeti

Member
Jun 22, 2008
5
0
Wanajamii
Ni juzi tu bungeni wametangaza kuongeza kiwango cha mishahara ingawaje hakikidhi haja ya mdanganyika anayeteseka.

Cha kushangaza ni kuwa serikali inaanza kukopa nguvu za wanyanyasikaji wake.
Pale Muhimbili hospitali wafanyakazi wamewekewa tangazo kubwa kabisa kuwa mshahara ni mpaka tareha 6 August.Yaani malipo ya July.Hakuna anayejua ni mshahara mpya na malimbikizo au ni nini.

Je kweli tutafika?Watu wanaoishi kwa mishahara kweli kuna usalama hapo?
Angalia wagonjwa pale wamelala chini karibia wodi zote hasa wodi ya wazazi.Afya wapi na wapi.Mkeo anawezakwenda pale mzima akarudi na magonjwa maana kuna wengine wanalazwa pale kwa ajili ya watoto wao wagonjwa [njiti]

Mimi sitashangaa kuona mgomo wa wafanyakazi tena hapo muhimbili ikiwa utaratibu ndo huo.Media kaangalie muwaeleze na watanzania wengine.

Nimeliona tangazo kwenye mbao za matangazo nimesikitika sana.

Toeni maoni yenu wazalendo.
 
Wanajamii
Ni juzi tu bungeni wametangaza kuongeza kiwango cha mishahara ingawaje hakikidhi haja ya mdanganyika anayeteseka.

Cha kushangaza ni kuwa serikali inaanza kukopa nguvu za wanyanyasikaji wake.
Pale Muhimbili hospitali wafanyakazi wamewekewa tangazo kubwa kabisa kuwa mshahara ni mpaka tareha 6 August.Yaani malipo ya July.Hakuna anayejua ni mshahara mpya na malimbikizo au ni nini.

Je kweli tutafika?Watu wanaoishi kwa mishahara kweli kuna usalama hapo?

Kwa utafiti mdogo niliofanya nasikia Muhimbili Hospitali wana kawaida ya kulipwa mishahara mapema sana na hawana longolongo. Kama mshahara wa mwezi July utatolewa tarehe 6 August baada ya ku-effect nyongeza nafikiri hakuna shida, natumaini wafanyakazi wa hiyo hospitali watavuta subira wakijua ni jambo la dharura tu na si kawaida yao. Ni kweli kutakuwa na usumbufu kidogo kusubiri hiyo pesa lakini sidhani kama itakuwa ni busara kwa mtu yoyote kugoma. Mashirikia yetu hayako that smart kiteknolojia kubadili mshahara wa kila mtu kulingana na ngazi yake kwa muda mfupi hivyo, nafikiri hiyo extension ya muda ni jitihada tu za kufanya hayo marekebisho ili kila mtu aanze kufurahia mshahara mpya hii JULY. Ingekuwaje kama wakikuambia usubiri Makarisaji hadi December?!!

Lets hope kuwa hizo ada za shule na deni la mchele kwa mpemba litalipwa around tarehe 6 August.
 
Tangazo uliloliona limeenea nchi nzima, maana hata huku kwetu kulikosahaulika limefika. Ile misururu mirefu (foreni) ambazo mtu anazikuta benki kila mwisho wa mwezi hazipo kabisa na mambo ni kimyaaa kabisa.

Mnyanyaswaji ataziki kuumia kwa hali mpya na kasi mpya hii. Vitu madukani navyo ndivyo hivyo, bei zinazidi kwenda juu kwa kisingizio cha ongezeko la mishahara.

Tunakoelekea hatuji...
 
Wanajamii
Ni juzi tu bungeni wametangaza kuongeza kiwango cha mishahara ingawaje hakikidhi haja ya mdanganyika anayeteseka.

Cha kushangaza ni kuwa serikali inaanza kukopa nguvu za wanyanyasikaji wake.
Pale Muhimbili hospitali wafanyakazi wamewekewa tangazo kubwa kabisa kuwa mshahara ni mpaka tareha 6 August.Yaani malipo ya July.Hakuna anayejua ni mshahara mpya na malimbikizo au ni nini.

Nimesikia ikisemwa kuwa ni 'kawaida' mishahara ya July kuchelewa, na kwamba malipo hufanywa mwezi August.
It shouldn't be this way, but well... serikalini mambo ni lelemama!

.
 
Taarifa nilizozipata jana ni kwamba uwezekano wa nyongeza kutolewa mwezi huu ni mdogo.nyongeza itawekwa mwezi wa nane.

Kama ni kweli nchi iko kwa dalali hii
 
Poleni.... lakini wakati mwingine pia ni kukakisha payroll software package inafanya new calculation vizuri otherwise.... unaweza kupasua bomu nchi nzima.
 
Lets just wait and C...maana walisema inge take effect mwisho August...sijui lipi ni lipi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom