mtambobajeti
Member
- Jun 22, 2008
- 5
- 0
Wanajamii
Ni juzi tu bungeni wametangaza kuongeza kiwango cha mishahara ingawaje hakikidhi haja ya mdanganyika anayeteseka.
Cha kushangaza ni kuwa serikali inaanza kukopa nguvu za wanyanyasikaji wake.
Pale Muhimbili hospitali wafanyakazi wamewekewa tangazo kubwa kabisa kuwa mshahara ni mpaka tareha 6 August.Yaani malipo ya July.Hakuna anayejua ni mshahara mpya na malimbikizo au ni nini.
Je kweli tutafika?Watu wanaoishi kwa mishahara kweli kuna usalama hapo?
Angalia wagonjwa pale wamelala chini karibia wodi zote hasa wodi ya wazazi.Afya wapi na wapi.Mkeo anawezakwenda pale mzima akarudi na magonjwa maana kuna wengine wanalazwa pale kwa ajili ya watoto wao wagonjwa [njiti]
Mimi sitashangaa kuona mgomo wa wafanyakazi tena hapo muhimbili ikiwa utaratibu ndo huo.Media kaangalie muwaeleze na watanzania wengine.
Nimeliona tangazo kwenye mbao za matangazo nimesikitika sana.
Toeni maoni yenu wazalendo.