Mseto wa zanzibar waiweka CUF njia panda kama chama cha upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mseto wa zanzibar waiweka CUF njia panda kama chama cha upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuthumiwa haule, Dec 30, 2010.

 1. k

  kuthumiwa haule Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika mitego mibaya ambayo Chama cha CUF wamewahi kutegewa na kunaswa ni kujikuta wameingia kwenye mseto ambao kimsingi umewavua sifa ya kuwa watetezi wa wananchi kwa kuleta changamoto mbadala, kwa kujiunga na sisiem na serikali hiyo kuwa chini ya uongozi wa sisiem na makamu wa pili wa rais na kwa mantiki hiyo kushindwa kufikia malengo kokote kutakako tokea Cuf hawawezi kuilaumu sisiem, bali wote kwa pamoja walaumiwe, na jingine la kujiuliza ni hili , ile CUF ya mwaka 2000 iko wapi , CUf iliyojijengea umaarufu mkubwa kuwa mbadala wa sisiem , cuf iliyothubutu kutetea haki hata kupelekea watanzania kupoteza maisha , Lipumba kupigwa makofi na aliyekuwa mnene wa polisi Dar wakati huo, lakini bado aliweka msimamo wa kuto rudi nyuma ,je hayo maamuzi waliyoyachukua ya kuunda mseto ndiyo malipo kwa watanzania tuliyokuwa tukiyatarajia,Leo CUf imekuwa chama cha kufubaza juhudi za watanzania kujikomboa na mfumo huu kandamizi kwa zaidi ya miaka hamsini. inasikitisha , inatia huruma. it's a long way towards total self support .Naomba kambi kambi ya upinzani bungeni tulindeni, ila CUF msiwaamini.
   
Loading...