Msemo wa "wanaume wakimya ni wabaya" hauniingii akilini

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,697
9,774
Je, ushawahi kutana na ile kauli ya "wanaume wakimya waone hivihivi" kutoka kwa wanawake? Walio wengi huamini kuwa wanaume wakimya wanafanya mambo mengi hususan ya kingono wakiwa faragha! Ila inawawia vigumu watu wengi kuwanasa watu wa aina hii

Pia kuna kauli ya "wanaume wakimya ni mafundi katika uwanja wa kufanya mapenzi, kuwa akitoka na mwanamke, mwanamke huyu iwe isiwe lazima atalizishwa vya kutosha kiasi cha kukidhi haja yake ya kimapenzi, ingawaje inaaminiwa kuwa wanaume wa aina hii hawako romantic katika mahusiano, yaani kwa issue ya kupet pet n.k, mambo yao mengi sana yamefichika, huwa si waongeaji pia!

Mimi ni moja ya wanaume wakimya zaidi kuwahi kutokea ulimwenguni! Lakini sioni kama ukimya wangu una relate na performance yangu kitandani! Sio mzembe kivile, ila ni kwa kiasi ambacho siwezi kuwafikia wataalamu wa kidunia! Ukimya wangu si kwamba ni natural, ila ni kwa vile huwa nakosa cha kuongea pindi niwapo na partner, najiuliza nizungumze naye kuhusu nini! Tumseme mtu, hapana! Nimuulizie kuhusu yeye, hapana! Yote kumhusu nayafahamu! Hivyo tunabaki kutazamana tu!

Nawavutia wasichana wengi hapa mtaani! Wanatamani japo nizungumze nao walau kwa salamu, ikitokea nimekaa na mmoja wapo, basi, wengine hujisogeza taratibu kupindua mazungumzo! Nachukuliwa mtu serious saana na maisha! Ujanja wangu ni kwenye sms na social media tu! Hakuna mwanamke hapa mtaani nimejaribu japo kwa kumuita akakataa! Hata ninaowabahatisha kuwa nao kimapenzi, inakuwa ni ngumu kwa wao kuniacha ingawa sifikii level za kimataifa!!

Hivi ni nani aliwadanganya wanawake kuwa wanaume wakimya ni wa kuwang'ang'ania katika mahusiano? Kwamba wana upendo wa dhati licha ya kuwa na partner wengi?

Ngoja tuone wao wanawazungumzia vipi wanaume wakimya!!
 
Wanaume wakimya huwa hatuna tabia ya kuandika uzi mrefu namna hii,sema wewe ni mwanaume mwenye kiburi
 
Kwahiyo mkuu ukikutana manzi mazungumzo huwa hivi..
Wewe: mambo Rachel
Rachel:. Poa vp...
Wewe: fresh karibu.

Rachel: Asante.
KWISHAAAA.

Baada ya hapo ni kunjunjana then..
Wewe: kwaheri Rachel
Rachel: Nashkuru.
 
Wanaume wakimya huwa hatuna tabia ya kuandika uzi mrefu namna hii,sema wewe ni mwanaume mwenye kiburi

Nimecheka sana! Kwa sababu niliwahi pita kwa wakina dada wanne walikuwa wakisukana, nikawaambia "habari zenu" wakaitikia! Nilivyokunja kona nikasimama nikawasikia wakisema," huyo kaka ana kiburi, halafu anajiskia, anavunga hana time na mapenzi, ngoja yamfike shingoni! Tutamuona atakavyoturejea huku akijishusha, tutamtazama bila huruma".

Nikashindwa kuhusisha kati ya upole na kiburi!
 
Hizi kauli zipo sana.

Mtoto wangu wa kiume mmoja ni mpole. Wakija wageni kwangu wengi husema dogo atakuwa hatari hapo baadae eti kwa kuwa ni mkimya na mpole.

Huwa sioni mahusiano.

Ni kama vile ambavyo wadada wengi wamemezeshwa kuwa wanaume wa kipare ni wahuni sana.
Pia sioni mahusiano baina ya kuwa mwanaume mpare na tabia za kihuni.
 
Back
Top Bottom