Msemo wa KUCHOMOA BETRI unaudhi sana na ni dhihaka kwa marehemu wa ajali ya moto Morogoro

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
574
1,000
Kumezuka msemo mpya wa kuchomoa betri baada ya ajali mbaya ya moto iliyochukua zaidi ya maisha ya Watanzania mia moja.

Wizara ya Mwakyembe ichukue hatua kukataza magazeti hasa ya michezo.

Msemo huo umekua maarufu sana baada ya kusemekena ajali hiyo ilisababishwa na mmoja ya waliokuwa wakichota mafuta kujaribu kitoa betri.

Ilikuwa ni ajali mbaya sana kiasi kwamba mpaka bendera ya taifa ilishushwa nusu mlingoti kwa siku tatu.

Kuna familia zilipoteza wapendwa wao hivyo kila wakiona hayo maneno ya KUCHOMOA BETRI hukumbuka machungu waliyopitia wakati ule.

Tuache kuwakumbusha machungu ndugu zetu waliopoteza rafiki zao, ndugu zao, mama zao,baba zao.
 
Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,984
2,000
Watanzania ni watu wa matukio hawezi kuwakanya kitu hasa wakiamua kufanya.

Siyo msemo mzuri ndiyo ila je unatumiwa na watu gani? Jibu ni Watanzania, ambao maisha yao yanaendeshwa kwa mihemko na furaha za muda mfupi + upuuzi.

Unakumbuka msemo wa 'utapigwa hadi uchakae'
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Aibu na dhihaka ni wizi waliokuwa wanaufanya, tena ukemewe kwa nguvu zote, wizi wizi wizi kwa kisingizio cha maisha magumu hauna maana bora terminator kachomoa betri ovaaaaa

Kumezuka msemo mpya wa kuchomoa betri baada ya ajali mbaya ya moto iliyochukua zaidi ya maisha ya Watanzania mia moja.

Wizara ya Mwakyembe ichukue hatua kukataza magazeti hasa ya michezo.

Msemo huo umekua maarufu sana baada ya kusemekena ajali hiyo ilisababishwa na mmoja ya waliokuwa wakichota mafuta kujaribu kitoa betri.

Ilikuwa ni ajali mbaya sana kiasi kwamba mpaka bendera ya taifa ilishushwa nisu mlingoti kwa siku tatu.

Top Bottom