Msemo wa 'Hapa Kazi Tu' unatumiwa vibaya Jukwaa la Elimu

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Wanabodi

Kumekuwa na tabia ambayo mimi binafsi sipendezwi nayo kabisa, tabia hii imeibuka punde tu baada ya matokeo ya Rais kutangazwa. Kwa yeyote ambaye ni mfuatiliaji wa Mada zinazowekwa humu na majibu ya wachangiaji atakubaliana na Mimi kuwa msemo "hapa kazi tu" unatumika vibaya sana tena katika mambo ya msingi.

Wanafunzi wengi wanaamini kuwa JF ni sehemu ya kupata ushauri ila baadhi ya watu wamekuwa wakikatisha tamaa kwa majibu yao ya hapa kazi. Yaani mtu ameweka mada nzuri na anategemea majibu mazuri yenye busara lakini cha ajabu anatokea mtu ambaye huenda hata mada hajaisoma vizuri anaamua kuandika "hapa kazi tu" wakati mada husika haipingi kazi.

Kuna mwenzetu mmoja aliwahi kuweka bandiko la kuomba ushauri baada ya kukosa mkopo maana baba na mama wote marehemu ila majibu aliyopewa hayakuwa mazuri kabisa maana "hapa kazi tu" ziliongozana, hivyo hamna umuhimu wa JF kwake maana watu wa JF wanataka mada za kazi tu.Tujirekebishe ili kurudisha hadhi ya JF ya 2006-2012 ambapo kweli walikuwa wanapatikana great thinkers wa kweli.

Tunaomba jambo hili lipingwe na kila mmoja wetu maana halifai tena tupinge kama tunavyopinga matumizi ya "X" .
 
Mkuu polee tatzo wengi wanalolitumia ni vilazaa tuu!! Kwani siku zote walikuwa hawafanyi kaz?? Livumilie hili neno linamwisho wake
 
Hapa kazi tu na sasa kazi tu, uchaguzi umeisha tufanye kazi na sio bla bla na ujanja ujanja mwingi usio na tija. Na mtaisoma namba
 
Back
Top Bottom