Msemo 'Utakiona cha Mtemakuni' asili yake ni ipi? Mtemakuni alikuwa nani au kilikuwa nini?

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
5,659
6,452
Habarini wakuu,

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada. Kuna huu msemo uliozoeleka wa "utakiona cha mtemakuni" huu ni msemo wa kuonya au kutisha kuwa usipofanya kama ulivyoelekezwa na mhusika basi utapata tabu sana.

Nijuavyo mimi kila kitu kina origin yake. Huyu "mtemakuni" alikuwa ni nani? au ilikuwa ni kitu gani? Au hapo awali kulikuwa na mtu mbabe kiasi kwamba alikuwa anatisha hadi anatema kuni live?

Samahanini kama mtaona ni swali la kijinga ila huwa linanipa wakati mgumu sana kila nikimuwaza huyu "mtemakuni"
 
Mtemakuni- mtafuta kuni porini,mtenya kuni porini,mkata kuni kwaajili ya kuchoma mkaa kama unawafahamu basi utakakuwa umeelewa,kwa wasiowafahamu hawa watu zamani walikuwa ni watu wa miraba minne/wenyewe wananguvu/mapande ya watu kwasababu kazi ya kuangusha kuni au miti mikavu si ya kitoto/si kazi ndogo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambiwa msemo huu wahenga waliupata katika kisa kimoja cha zama za kale. Wanasema kulikuwa na msitu jirani na kijiji, ndani ya msitu kulikuwa na miti mingi sana. Ilitokea kuwa katika msitu ule, kulikuwa na miti inapishana sana kwa uzuri, na kati yao ulikuwepo ule ambao ni mzuri sana!

Mtema kuni (Mtemakuni maana yake ni Mkatakuni) alienda katika msitu ule katika shughuli zake za kila siku za kukata kuni!
Alipofika jirani na ule mti mzuri, huku akiwa na shoka mkononi, ule mti zuri sana ulikuwa jirani na mti mbaya sana!

Katika hali ya kufedhehesha (kwa nyodo na maringo) ule mti mzuri sana ukawa unamcheka na kumdhihaki ule mti mbaya, kwamba hauna mvuto na ndio maana kuanzia mbali kabisa, Mtemakuni akaonyesha kuvutiwa na (yeye) Mti mzuri! Huku Mtemakuni akizidi kuusogelea mti mzuri, mti mbaya sana ukajifariji kwa kumwambia mti mzuri basi subiri “utakiona cha mtema kuni”

Kilichofuata ni kweli, Mtema kuni aliukata na kuucharanga Mti mzuri sana kiasi cha kuugeuza kuni za kumfaa kubeba na kuondoka nazo, huku akiuacha ule mti mbaya salama salmini pale msituni!

Yakawa ni majuto kwa Mti mzuri na furaha kwa Mti mbaya! Hivo ndio nilivyopokea kisa cha “mtema kuni”

UJUMBE WAKE KWA JAMII

1. Mliobarikiwa uzuri punguzeni maringo na nyodo!
2. Usijutie ubaya wa maumbile yako, Mungu ana maana kubwa sana kukuumba hivyo!
3. Shukuru Mungu kwa kila ulichonacho!
tapatalk_1569556612979.jpeg
 
Nilisikia visa viwili tafauti vya mtema kuni.

Kisa cha kwanza kilikuwa kwenye shairi, pengine kwenye kipindi cha RTD, na mghani wetu Athuman Halfani. Miaka hiyoo, ya 19kweusi. Kibwagizo cha shairi lile kilikuwa:

badala ya kutema kuni, alitema mguu wake.
 
Back
Top Bottom