Msemo " Behind every man's success there is a woman" umewaponza watu wengi sana.

Nimetofautiana na wewe mkuu kwa kuugeuza negatively msemo huo mzima, bila kuuwekea upande wa pili wa shilingi.

Hayo maisha uliyojadili wewe hapa ni ya kimjini zaidi na yanachelewesha vijana kuoa.

Familia nyingi Tz hazina mitaji ya kuwezesha watoto wao kuingia kwenye mafanikio ya mapema kabla ya kufikia umri wa kuoa.

Kuoa mapema kuna faida zake nyingi, kwa sababu maisha ya binadamu ni namba, huenda yanapungua.

Mbona mimi hapa nimeoa hohehahe, nikiwa kijana mdogo wakati huo sina unachoweza kuita cha kumiliki!

Lakini tume hustle na huyu mama kwa miaka nendarudi hadi kufikia mafanikio tuliyonayo yenye kutolewa mfano sasa.

Ukioa mwanamke wa aina uliyozungumza wewe bila kupata support yake, kamwe hauwezi kusonga.

Kama atakuwa mtumiaji tu bila kuwa na uchungu wa pato mnalozalisha, hata kidogo alichokukuta nacho kitaondoka na yeye kuondaka kama ulivyokwisha sema.

Wanawake wapo sampuli nyingi, wote si wa kundi moja.
Wapo unaweza kuanza naye maisha bila ya kuwa na chochote mkafanikiwa na wapo wengine kwa ajili ya kula nao tu bata na ukiishiwa siyo wako tena, lakini si wote kama ulivyo wagroup wewe.
 
Back
Top Bottom