Msemakweli amjibu Yusuf Manji kuhusu KAGODA

Warofo

Member
Mar 15, 2011
81
79
Msemakweli ametoa taarifa kumjibu Yusuf Manji kutokana na matangazo yake ya magazeti aliyoyatoa kuhusu wizi wa 40 bilioni/- kutoka akaunti ya EPA ya Benki Kuu kupitia kampuni ya KAGODA.

Taarifa kamili ya Msemakweli hii hapa:

TANZANIA blog
 

Attachments

  • TAARIFA YA MSEMAKWELI.pdf
    604.5 KB · Views: 626
Huenda ni kwa Elimu yangu Finyu ndio hii picha inashindwa kujiunganisha. Naomba msaada kwa Wanajamvi labda mnifumbue macho. Ina maana, pesa zote Bilioni 31 walizoziiba Kagoda walikwenda kumkopesha Manji! Kama hiyo ni kweli, wao walibaki na nini! Bado nachanganyikiwa na dili la aina hii.
 
Msemakweli ametoa taarifa kumjibu Yusuf Manji kutokana na matangazo yake ya magazeti aliyoyatoa kuhusu wizi wa 40 bilioni/- kutoka akaunti ya EPA ya Benki Kuu kupitia kampuni ya KAGODA.

Taarifa kamili ya Msemakweli hii hapa:

TANZANIA blog

Manji kweli ni mwizi na muhujumu uchumi.
 
Huenda ni kwa Elimu yangu Finyu ndio hii picha inashindwa kujiunganisha. Naomba msaada kwa Wanajamvi labda mnifumbue macho. Ina maana, pesa zote Bilioni 31 walizoziiba Kagoda walikwenda kumkopesha Manji! Kama hiyo ni kweli, wao walibaki na nini! Bado nachanganyikiwa na dili la aina hii.

Ni mambo ya mkono wa kulia unachukua unapasia wa kushoto, mtu ni yule yule. CCM oyeeeeee!
 
Fanya kui-copy hiyo pdf ili iwe rahisi nasi 2nao2mia simu kuisoma
 
Simu yangu haina adobe, so nimeshndwa kuona chochote, nitarudi baadae
 
TAARIFA YA KAINERUGABA ERICK MSEMAKWELI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WIZI WA DOLA MILIONI 31 ZILIZOFANYA NA MAKAMPUNI YA KAGODA AGRICULTURE LIMITED NA QUALITY FINANCE CORPORATION LIMITED

Baada ya kusoma na kutafakari taarifa iliyotolewa na Yusuf Mehbub Manji kwa vyombo vya habari Septemba 8, 20011 nimebaini kwamba imejaa uongo na upotoshaji mwingi kiasi cha kunilazimu mimi kujibu kama ifuatavyo.

Matusi na kejeli dhidi yangu na hasa elimu yangu.

Taarifa ya Manji imejaa matusi na kejeli dhidi yangu kwamba mimi si chochote, nabangaiza, natumia vitisho ili kujipatia fedha (yaani blackmailer) na ni mtunzi wa vitabu vya kukashifu watu. Haya yote siyo kweli na ni dhahiri kwamba Manji amepatwa na hasira na jazba baada ya kuumbuka.

Niko tayari kwa matusi, kejeli na vitisho na sitorudi nyuma. Lakini angetumia akili yake vizuri angegundua kwamba mimi nina shahada ya sheria ambayo nilitunukiwa 2008.

Kwamba ninatumiwa.

Hii siyo kweli; historia yangu inajieleza. Ari yangu ni uchungu na nchi yangu ambapo watu wanaweza kuiba mabilioni ya pesa wakajulikana na wasichukuliwe hatua. Nilipokuwa naingia kwenye harakati hizi nilijua wapo watu wenye nia mbaya ambao wangenituhumu natumiwa. Manji ni miongoni mwa watu hawa. Lakini watambue kamwe hawatanirudisha nyuma.

Ushaidi wangu kwa DPP. Katika taarifa ya Manji amejaribu kuuaminisha umma kwamba mimi ni muongo na kwamba eti kampuni ya Quality Finance Corporation Limited ambayo anakiri ni yake imetapeliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited. Huu ni uongo wa wazi.

Manji yuko nyuma ya makampuni yote mawili na kama kawaida yake anataka kuchezea akili za Watanzania. Kwanza kwanini alidhamini Kagoda kufungua akaunti Benki ya CRDB? Kwa nini aliingiza fedha dola milioni 2 katika akaunti ya Kagoda na makubaliano ya fedha hizi yako wapi?

Ilikuwaje aingie mkataba na kampuni ambayo haijasajiliwa? Nyaraka zinaonyesha Kagoda ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni Septemba 29, 2005 wakati mkataba wa kukopeshana ambao Manji anataka tuuamini umesainiwa Septemba 12, 2005. Manji anatakiwa kufahamu kwamba kurejesha mali ya wizi ni wajibu na siyo fadhila kwa maana ukisharejesha hauwezi kushatikiwa.

Tanzania bila ufisadi inawezekana. Watanzania tuthubutu kuwafichua na kuwaanika mafisadi. Ningependa kuwashauri Watanzania wote wenye ushahidi au taarifa za ufisadi wazipeleke kwenye vyombo vya sheria kama nilivyofanya mimi.


Kainerugaba Erick Msemakweli

Dar es Salaam

Septemba 9, 2011
 
Nimeipenda hii ya leo,ndomana mzee wa visuti ameomba mwaliko aende marekani coz nchi inawaka moto.
 
Back
Top Bottom