Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,876
Taarifa zilizotufikia wakati huu ni kuwa yule jamaa 'aliyewalipua' Rostam, Manji na wenzao jana; kakamatwa na Polisi toka ofisi ya DCI (Manumba) na anaendelea kuhojiwa.

Taarifa zinadai kuwa Msemakweli alielekea kwa DPP kama alivyoahidi hiyo jana kuwa angeenda kwake na kuambiwa kuwa appointment yake imesogezwa mpaka Jumatatu lakini akiwa njiani kurudi akakamatwa na maofisa wa polisi ambao mpaka sasa wanaendelea kumhoji.

Hatujapata taarifa za nini amehojiwa na nani kamhoji. Tutaendelea kufahamishana kadiri muda utakavyoruhusu.

Huu ni mwanzo tu, kuna mengine yatajiri muda si mrefu!

KUMBUKA KAULI YAKE:
Rostam na Manji nawamudu, siogopi usalama wangu. Siwaogopi na liwalo na liwe! Sitishiki juu ya usalama wangu.

Msemakweli

UPDATES:

Maelezo mapya:

Msemakweli alikamatiwa ofisini kwa DPP. DCI Manumba alienda kwa DPP asubuhi akiwa na timu yake kisha Msemakweli alipofika na kuambiwa arudi Jumatatu akawakuta nje ya ofisi wakiwa wanamsubiria, akachukuliwa na kwenda naye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani kwa DCI kabla ya kumchukua kwenda naye Mikocheni zilipokuwa ofisi za tume ya EPA.

Update 1:
Ningependa kuwataarifu wana jamii kuwa Msemakweli yuko huru mpaka sasa ninavyoandika. Nimempigia simu muda si mrefu na kunieleza kuwa yuko huru.

Kuhusu kukamatwa kwake na nini amehojiwa nawaahidi kuwapa taarifa hapo baadae.

Aluta continua!!
Update 2:

Msemakweli yupo huru kuongea na simu lakini si kama kaachiwa, mida hii (02:00PM) anaelekea kuandika maelezo.

Update 3:

Wadau habari nilizozipata sasa ni kuwa mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli bado yuko polisi kituo cha Oysterbay na anasubiri kuandika maelezo (2:12 pm); hata hivyo the guy looks so healthy and confident.

Nitafanya naye mahojiano saa 10 na nitawajulisha kipi amehojiwa na kipi ameandika kwenye maelezo huko polisi.

Update 4:
Msemakweli kaweka ngumu kuandika maelezo, kaachiwa... Atarudi Jumatatu kuweza kutoa ushirikiano kwa task force ya polisi inayofuatilia issue ya EPA.

Ndugu wadau, kama mwananchi mzalendo nimeonelea vyema niwape taarifa fupi niliyo ipata kutoka kwenye original source(msemakweli) mwenyewe mala baada ya kuachiliwa na polisi. ni kwamba DPP alimpigia simu tangu jana kwamba anataka waonane ofisioni kwake(kwa DPP) na ilikuwepo appointment na DPP mwenyewe alijua kuwa msemakweli atawasili ofisini kwake leo asubuhi. wakati yuko kwa DPP akaambiwa kuwa tuhuma hizo za wizi zinatakiwa zipitie polisi kama procedure and then further action will commence from thereon. wakati anatoka nje akakutana na polisi wanamsubiri kwa nje akiwemo DCI( director of criminal investigation).

Arrest ilifanyika kama request hivi, according to msemakweli kwani aliombwa akaandikishe maelezo polisi na ndipo wakitumia gari maalum la usalama wa taifa, walipoelekea makao makuu ya usalama wa taifa na pia makao makuu ya polisi kwa nyakati tofauti.

Wakati yuko huko polisi aligoma kuandikisha maelezo, na aliwambia usalama wa taifa na polisi kwa kusema, hapa namnukuu" tangia asubuhi sijapumzika na nimechoka. nina njaa na siwezi kuandika chochote. subirini mpaka ijumatatu." alisema bwana msemakweli. hata hivyo walimshukuru kwa ushirikiano.

Hivyo basi, ameshauriwa asiwe anatembea zaidi ya saa moja kwa usalama wake.

MWISHO WA REPORT.
More updates coming
 
Feleshi alikuwa anajizungusha kuhusu kuwashtaki hawa jamaa...kapelekewa ushahidi na bado anataka kumghasi raia mwema huyu.
wanaostahili kukamatwa hawaoni?
 
Kwa hiyo dola ndio iliyotuhumiwa hapa !! ama dola ipo kwa niaba ya watuhumiwa na hii imeanza lini ?
 
Amekubali kutumika Bila mipango kwa wanasiasa wenye kurushiana makombora katika Kambi mbili za GAMBA...Si mwanaharakati I HATE HIM
 
Itakua mahojiano tu ya kawaida,watamuachia na kuwasilisha ushahidi wake DPP! Nasikia Chadema wamemkasilikia sana Msemakweli kuwa amepola hoja yao ya Kagoda!
 
Sidhani kama jamaa amekurupuka, kama ana ushahidi TOSHA na kafanya utafiti wake wa kutosha huko si kukurupuka. Ngoja tuone yakifika mahakamani ila kila kitu kiwe hadharani. Jamaa ni SHUJAA fupa la Kagoda limewashinda wengi sana.

Bora yeye Amesema ILI haki isije kumhukumu kama akiamua kufa nalo ndani ya moyo wake.
 
Back
Top Bottom