Msemaji wa waasi Rwanda akiri kufanya ugaidi na uhaini Mahakamani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Nsabimana Callixte maarufu Sankara aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi la National Liberation Front amefikishwa mbele ya Mahakama mjini Kigali na kukiri mashtaka dhidi yake

Mwendesha mashtaka amesoma mashtaka 16 dhidi ya mshtakiwa huyo ambayo yana uhusiano na ugaidi, ujambazi wa kutumia silaha na ushirikiano na nchi ya kigeni kwa lengo la kuishambulia Rwanda

Sankara amekiri kushirikiana na Burundi pamoja na Uganda katika kuishambulia Rwanda na ameomba msamaha kwa Serikali pamoja na familia zote zilizoathirika kutokana na uhalifu alioufanya

Pia amekiri kundi hilo kuhusika na shambulizi la mwaka 2018.

Callixte alimakatwa Aprili nchini Comoro na kusafirishwa kwa siri kwenda Rwanda,
 
Hivi yule mwasi wa Drc Laurent Nkunda aliyesemekana amekamatwa na Rwanda alipotelea wapi? Au ni siasa za maziwa makuu zinachezwa hapa.
Nkunda yuko Kigali anakula pension yake kwa kazi 'nzuri' sana aliyowafanyia, wkt Bosco Ntaganda alipelekwa ICC.
 
Nsabimana Callixte maarufu Sankara aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi la National Liberation Front amefikishwa mbele ya Mahakama mjini Kigali na kukiri mashtaka dhidi yake

Mwendesha mashtaka amesoma mashtaka 16 dhidi ya mshtakiwa huyo ambayo yana uhusiano na ugaidi, ujambazi wa kutumia silaha na ushirikiano na nchi ya kigeni kwa lengo la kuishambulia Rwanda

Sankara amekiri kushirikiana na Burundi pamoja na Uganda katika kuishambulia Rwanda na ameomba msamaha kwa Serikali pamoja na familia zote zilizoathirika kutokana na uhalifu alioufanya

Pia amekiri kundi hilo kuhusika na shambulizi la mwaka 2018.

Callixte alimakatwa Aprili nchini Comoro na kusafirishwa kwa siri kwenda Rwanda,
Maigizo hayo.. huyu hakua muuasi.. aliwekwa na kagame mwenyewe kama gelesha.

Sio huyo tuu wapo wengi.
 
Alipopewa nafasi Sankara ameiambia mahakama kwamba hana mengi ya kuzungumza isipokuwa kujutia yaliyotokea.

''kile ambacho sikutekeleza mwenyewe, kilitekelezwa na wapiganaji wa kundi nililokuwa msemaji wake'' ameeleza Sankara.

Amesema kwamba wapiganaji wake walimtelekeza na kufanya kinyume na malengo yake wakati wa shambulio dhidi ya vijiji vinavyopakana na msitu wa Nyungwe kwa kuuwa raia wa kawaida.

''kutokana na sababu hiyo,kwa moyo mkunjufu naomba radhi wananchi wa Rwanda waliopoteza watu wao katika mashambulio hayo na kuuwa raia kinyume na malengo niliyokuwa nayo.''

Kwaiyo mzunguko wote huo PK alikuwa anataka kuichafua Uganda na burundi tu sasa sijui ili iweje
 
Hahahaha, huwa ni pasua kichwa
Mwisho wa siku raia wa Drc wanateseka na vita visivyokwisha miaka nenda rudi huku nchi jirani zikiteseka kwa kupokea mzigo wa wakimbizi! Ila hawa majamaa lazima watalipia haya mateso wanayosababisha kwa raia kabla ya mauti kuwakuta.
 
Alipopewa nafasi Sankara ameiambia mahakama kwamba hana mengi ya kuzungumza isipokuwa kujutia yaliyotokea.

''kile ambacho sikutekeleza mwenyewe, kilitekelezwa na wapiganaji wa kundi nililokuwa msemaji wake'' ameeleza Sankara.

Amesema kwamba wapiganaji wake walimtelekeza na kufanya kinyume na malengo yake wakati wa shambulio dhidi ya vijiji vinavyopakana na msitu wa Nyungwe kwa kuuwa raia wa kawaida.

''kutokana na sababu hiyo,kwa moyo mkunjufu naomba radhi wananchi wa Rwanda waliopoteza watu wao katika mashambulio hayo na kuuwa raia kinyume na malengo niliyokuwa nayo.''
Katika waasi ambao kesi yao inaendeshwa
Na media huyu jamaa ni wa kwanza pia sankara ndio muasi pekee ambae pamoja na kushikwa lkn bado afya yake ipo imara

Pia ndio muasi wa kwanza kusema kuwa wanapambana kijeshi na muda huohuo kuna wenzao tena wanapambana kisiasa

Mshangao zaidi now anadai kuwa burundi na Uganda walikuwa nyuma yake dah
 
Kwani Burundi na Uganda kua nyuma ya kundi lake umeona kuna uajabu wowote hapo?

Mbona hio inajulikana kwa kila mtu.

Kwani huyo anayejiita major Sankara na kundi lake waliposhambulia msitu wa nyungwe walikimbilia wapi?Si ni burundi.

FLN pamoja na kikundi cha Yule jamaa wa SA mbona hapo Uganda wanaenda kila siku na hata mwaka huu M7 aliumbuliwa baada ya passport za hao jamaa kuwekwa hadharani wakitumia za Uganda.

Sawa lkn sidhan kama kuna msaada wowote wa kijeshi ambao hao jamaa wanaupata kutoka Uganda

PK kachukua hatua gani dhidi ya hicho chama cha siasa ambacho sankara anadai ni washirika wake ?

Kumbuka pia niyombare aliyetaka kumpindua Nkurunzinza kapewa hifadhi Rwanda na furebu yake
 
Kwani hufahamu kwamba CMI wa Uganda akishirikiana na wakina Nyamwasa wanachukua watu Uganda kwenda kuwatrain huko Congo na Burundi?Mbona hio inajulikana boss.

Na btw CMI huyo wa Uganda mwaka jana walimkosa kosa kidogo tu kummaliza sa hivi ulinzi alionao ni balaa yeye na General Salim(Mdogo wake M7) walikua targeted sa hivi wanaishi kama kuku.

It's a fair game huku PK anafadhili waasi wa Burundi,huku Burundi inahifadhi waasi wa PK wala hakuna tatizo kwenye hilo.
Sawa lkn sidhan kama kuna msaada wowote wa kijeshi ambao hao jamaa wanaupata kutoka Uganda.

Nadhani kumkamata Huyo Mrembo anayejiita major ni hatua mojawapo ya kuwatumia salamu hao FLN.

PK kachukua hatua gani dhidi ya hicho chama cha siasa ambacho sankara anadai ni washirika wake ?

Kumbuka pia niyombare aliyetaka kumpindua Nkurunzinza kapewa hifadhi Rwanda na furebu yake
 
Watajijua huko ni Uganda, burundi wanataka kumtoa nishai Mr slim

Kwingine ni Kenya vs Somalia

Safi saana nadhani hii migogoro yao itatunufaisha kiuchumi wacha watwangane

Pia huyo CMI wa Uganda sidhani kama ana baraka za m7 kusaidiana na hao waasi

Back
Top Bottom