Charliemic
JF-Expert Member
- Feb 17, 2019
- 585
- 919
Msemaji wa Tanzania Dkt Hassan Abbas amesema Tanzania inakabiliana na janga la corona kwa kutumia dawa za asili.
DKt Abbas alimwambia mwandishi wa habari wa BBC,Salim Kikeke kuwa Tanzania haitapuuzia chanjo iliyokubalika kimataifa kuwa salama kutumia kama kinga.
Pia Ameeleza kuwa hakuna ambaye ameshawahi kusema Tanzania ni Corona free, kwani Tanzania ni sehemu ya dunia na kila siku inapokea wasafiri!
Amesema nchi ilichokataa ni kuwa sehemu ya majaribio ya chanjo ya UVIKO-19
Chanzo: BBC
======
Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema Tanzania haijawahi kusema hilo akifafanua, Tanzania ni sehemu ya dunia na kuna raia wa kigeni wanaokuja Nchini na wapo Watanzania wanaoenda nje hivyo muingiliano upo
Katika mahojiano na BBC, ameeleza Serikali inachosema ni Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti maambukizi ya COVID19 kwa njia za kisayansi na za asili. Pia, Serikali ilikuwa makini tangu mapema
Aidha, amesema Tanzania haijadharau chanjo za Corona na kufafanua chanjo nyingi zipo katika majaribio, hivyo ni vema zikaendelea kufanyiwa majaribio ili usahihi wake wa kisayansi uweze kuthibitika
Amesema, "Dunia nzima kuna kelele, yapo maeneo hizo Chanjo zimeleta athari kubwa kwenye Afya ya binadamu. Sisi kama Nchi hatuwezi kuwa sehemu ya majaribio"