Msemaji wa Serikali: Serikali imeelekeza, imeonya na kusamehe vya kutosha. Sasa kuvichukulia hatua vyombo vya habari vinavyosambaza taarifa za uongo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
Rejea.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
Huyu jamaa bure kabisa, ni wazi kaandika hii twit akitumaini Magufuli ataisoma, maana sidhani kama haya yeye mwenyewe ndani ya moyo wake anakubaliana na alichosema! Ndicho kilichobaki kwa hawa viongozi wa Tanzania!
 
na wa kenya rwanda na burundi ,uganda,amerika na trump wake je?

ACHENI ujinga vijana wa kibongo!
nguvu kazi yoote inawaza fiesta na tweeter tu.
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yalindwe.
P
Mkuu nakuheshimu sana,siwezi kuongea jambo baya litakalokukwaza,ila nikushauri kitu kimoja,wewe ni mtu unayeheshimika sana humu,ila tabia hii mpya uliyokuwa nayo siku hizi hapa jukwaani,ya kila lifanywalo na mamlaka liwe baya au zuri wewe kwako yote yanakuwa mema sio njema.

Simamia haki,pigania kweli,utashi binafsi unapozidiwa na tamaa ya mali,madaraka au hata wadhifa unaharibu personality yako.

Just be Paschal who we used to know.

Heri sifa njema kuliko marijani.

Ushauri kutoka kwa mdogo wako.
 
Asante sana kwa ushauri.

Naye kajiunga chama cha waimba mapambio sikuhizi.
 
Samahani kaka,hivi una Degree ya Mass Communications kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali??
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko take, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
 
Hata Wayahudi walishusha credibility ya Masiya na wakamsulubisha, itakuwa kapuku mimi kushushwa credibility na Bibi Kalamba?.
P
Hapana Mkuu kubali mashauri usikatae maonyo,haijalishi umeambiwa na nani,hii abrupt change inaacha walakini kwa watu wenye imani na wewe,simaanishi usiunge mkono wala kupinga,ila simamia kweli kwa dhati kabisa,haijalishi nani atakwazika,masihi hakulamba miguu ya watawala dhalimu,kina Herode,Pilato, Anasi na Kayafa.
 
Back
Top Bottom