Msemaji wa Serikali: Serikali imeelekeza, imeonya na kusamehe vya kutosha. Sasa kuvichukulia hatua vyombo vya habari vinavyosambaza taarifa za uongo

P! Magazeti ya Msiba Ni msiba kwa Vyama vya upinzani
Je wahariri wa magazeti ya Msiba msemaji wa Serekali haruhusiwi kuyaonya?
Musiba huwa magazeti yake yamesimamia ukweli bila kumuogopa mtu awe ni kigogo au la!
so ni lazima yawe mwiba kwa kundi kubwa la wapigaji wa nchi hii waliozowea kukutana mahotelini na kupanga mikakati na mitandao yao ya kipigaji nchini.

musiba amewaumbua mpaka raha,kuna watu ukimtajia jina musiba wanakosa usingizi kabisa.

viva Musibaaaa
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

✕ Powered by Exploreads"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
kabisa vyombo vya habari vimejisahau sana badala ya kripoti taarifa vinaripoti udaku
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
Tutakupa wilaya ya karatu!
 
Kwani propaganda nazo si habari? Waachieni watu wasome wanachopenda kusoma na waamini watakachotaka kuamini. Hamuwezi kuwalazimisha watu wote waimbe Xmass Carols wakati wakuimba Dirge msibani!
 
Hawa waandishi muwapige ban kwenye press conference yoyote inafanywa na viongozi wa kiserikali kuanzia Rais hadi viongozi Wandamizi wa chini kama jinsi Trump alivyompiga ban moja ya wandishi wa CNN
 
Naamini hii twit haijatoka bure! Kwani kuna habari gani mjini hapa! Chombo gani kimetoa habari iliyowakera wakubwa? Na ni habari gani hiyo?
 
Sasa unapata wapi ujasiri wakusema wewe ni mwandishi wa habari??

Nilidhani utakua wa kwanza kutumia kalamu yako,kuonyo uandishi wa habari wa Musiba,namna gani anatoka nje ya taaluma ya uandishi na gazeti lake la Tanzanite... Lakini leo hii unasifu nakuabudi, kweli??
No mimi sina kabisa degree ya mass comm. Sikusomea mass comm, nilimaliza tuu form IV nikajiunga RTD, ndio mpaka leo. Kwani vipi kuanza kuulizana elimu humu?.
P
 
Hivi sio kwamba uwongo unakanushwa? Kwa nini kufungia chombo cha habari badala ya kukanusha kinagaubaga?
 
Vigazeti vya kijinga vya Musiba kila siku vinaandika uzushi na kudhalilisha watu hivyo haviguswi, hizi double standard za Serikali hii zinakera sana.
 
Kwa sababu anaona umeanza kuwa Musiba sio Mayalla.Uandishi wako humu wa kinafki but low key it hurts inside u.But u can't speak cause 'em will portray as radical.
No mimi sina kabisa degree ya mass comm. Sikusomea mass comm, nilimaliza tuu form IV nikajiunga RTD, ndio mpaka leo. Kwani vipi kuanza kuulizana elimu humu?.
P
 
Vipi kuhusu musiba, naona vipeperushi vyake vinatamba tu
 
Back
Top Bottom