Msemaji wa Serikali: Serikali imeelekeza, imeonya na kusamehe vya kutosha. Sasa kuvichukulia hatua vyombo vya habari vinavyosambaza taarifa za uongo

Masiya ndio kitu gani hicho wewe? Asiyekufahamu wewe kuwa upo under cover- yaani mnoko, ndiye atapata shida. Tunao kufahamu hatupati shida. Wewe ni kalai tu kama Katambi
Hata Wayahudi walishusha credibility ya Masiya na wakamsulubisha, itakuwa kapuku mimi kushushwa credibility na Bibi Kalamba?.
P
 
Its never too late for anything, better late than never!.
Makanjanja walishamiri kwasababu ya uwepo wa mazingira wezeshi kuwawezesha kustawi, ukiwemo ukosekanaji wa viwango vya udhibiti, sheria mpya ya habari inaanzisha bodi ya ithibati ya waandishi wa habari, kiwango cha chini ni diploma, kiwango cha juu ni degree, makanjanja wengi watakuwa kicked out of system wenyewe, kama sisi wapiga dili tunavyoisoma number ya awamu hii ya JPM.
P

Inabidi kazi kubwa ifanyike bila kuangalia kanjanja anaandika ya kupendezesha serikali or not
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
He's such a disgrace
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
Paskali,
Naona sasa unapanda chart haraka sana. Wewe ni mtu uliyekuwa unatuliza mzuka kwanza kabla hujachangia ndipo uliposhusha andiko likawa la kumaliza mizozo. Ila kwa siku za karibuni, nadhani umeshadokezwa kuwa kuna ka Tuzo flani hivi kanaweza angukia njiani kwako. Yoote sawa ila kumbuka, njaa ikizidi huwa maafa. Usikimbizwe na njaa Paskali. Utakuja kula hata na yasokufaa. Mwanadamu kula magunzi si afya. Vile vyeo vizuri vishachukuliwa na waliounga mkono juhudi. We utapata nini??
Jiulize kwanza, Je, huyu msemaji aliyaandika hayo kwa lengo gani?? Je ni nani anashushiwa rungu?? Usiunge mkono tu ila jiongeze kidogo Paskali. Sote ni wazalendo ila uzalendo usiuondoe utu wetu
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
Kama kweli anaongea kutoka ndani ya moyo wake, basi tutegemee gazeti la Tanzanite kufungiwa la kwanza,kwa kuwa ndiyo limekuwa kinara wa kuzushia viongozi uongo
 
Msisitizo wa taaluma, haki, wajibu, weledi, misingi na sheria unakumbukwa tu pale kunapokuwa ukosoaji dhidi ya serikali na viongozi wake. Wale praise team (TBC na nduguze, kina Musiba nk) haya maonyo hayawahusu kabisa! Ni unafiki kwa kwenda mbele.
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
Mm nauliza hivi P! Je! Mitandao ya kijamii nayo ni taaluma?
Manake unless unaongelea tv na redios lkn huku tunakoskiliza kauli tukiwa tunarekodi af tukarusha u tube na jamii forum nako tusemeje?
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
You sound terrified ,sasa hapa ume add nini mkuu
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio ametoa onyo hilo kwa kusema;

"Katika siku za karibuni kumeibuka tena tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kushabikia, kutumika na kuwa mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi yetu kutoka mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje."

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo, Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua HATUA KALI za kisheria."

"Vyombo vya habari; vya ndani na nje ya nchi vilivyosajiliwa, kupewa ruhusa ya kutekeleza majukumu yao hapa nchini vinakumbushwa tena kwamba uandishi wa habari ni taaluma; ina haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria zilindwe, zisibanangwe"
Aanze na TAZANA TANZANIA,JANVI LA HABARI NA TANZANITE ili tujue kama ni mweledi na anasimamia weledi wa vyombo vya habari. vinginevyo ni ujinga tu wa bwana abasi
 
Kweli Mkuu Pascal, hasa kwa vyombo vya habari vinavyotoa habari kipropaganda badala ya kitaaluma na kupotosha mambo kimakusudi kwa manufaa binafsi ya watu fulani fulani. vinastahili adhabu! Vingekuwa Trump tunge vi-impeach!
kama vya Musiba
 
Naunga mkono hoja ya Dr. Abbas, uandishi wa habari ni fani, ni kipaji na pia ni taaluma, ina miiko yake, haki zake, wajibu wake, misingi yake na zaidi sheria zake. Sheria, taratibu na kanuni za uandishi zifuatwe na maadili yazingatiwe na yalindwe.
P
P! Magazeti ya Msiba Ni msiba kwa Vyama vya upinzani
Je wahariri wa magazeti ya Msiba msemaji wa Serekali haruhusiwi kuyaonya?
 
Tanzania ya sasa hakuna waandishi wa habari mahiri,
tutawakumbuka sana.hawa:

Benjamin mkapa.
Muhingo rweyemamu.
Jenerali ulimwengu.
Johnson mbwambo.
John rutayisingwa.
Pascal mayalla.
Faraji katalambura.
Eddie ganzel.

List ni ndeeefu,labda na wengine mnisaidie kuongezea kwenye list.

hawa wa sasa hivi wapo wengi wazuri lakini viwango vyao havikidhi mahitaji ya wakati tulionao.

Hawajishughulishi na kuongeza viwango vyao vya kielimu,lakini pia lugha na uwezo wao wa kuhoji watu mbalimbali tunawaona kabisa wakipwaya.

wengi wao ni wafukuzia bahasha kila wanapoitwa kwenye watoa taarifa mbalimbali, kwa ujumla wengi ingawa si wote.
wanatumikaaaa!

Tena hata lugha zao zinazotumiwa ni za kihuni.

mfano,mwandishi anatumia neno *kimenuka! au *kudadeki!,au *akinukisha

huu ni mfano mdogo sana,lakini kwa ujumla makanjanja kwenye tasnia hii ni kufuru!
 
Back
Top Bottom