Msemaji wa Serikali: Nyaraka za Makanisa TEC na KKKT hatuna cha kujibu bali Serikali inawatakia Pasaka njema

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Kayajibu hayo mara baada ya kutafutwa na mwandishi wa BBC kujua kama serikali nyaraka za makanisa mawili ile ya Katoliki (TEC) na KKKT kama Serikali wanazungumziaje yaliyoanishwa kama wameyachukua na kuyafanyia kazi au la.

Abbasi amejibu nenda ukurasa wangu wa twiter nimeshajibu na katika ukurasa wake imeandikwa hivi "kwa sasa hakuna cha kujibu bali wanawatakia Pasaka njema".

Hii ni dalili ya kiburi cha kulewa madaraka au malaika mkuu katoa direct order. Tutarajie wasiojulikana zaidi kama majibu ya nyaraka hizo.

Haki ya kupata habari haipo walio na madaraka wanaamua watakavyo.
 
Kayajibu hayo mara baada ya kutafutwa na mwandishi wa BBC kujua kama serikali nyaraka za makanisa mawili ile ya Katoliki (TEC) na KKKT kama serikali wanazungumziaje yaliyoanishwa kama wameyachukua na kuyafanyia kazi au la.

Abbasi amejibu nenda ukurasa wangu wa twiter nimeshajibu na katika ukurasa wake imeandikwa hivi "kwa sasa hakuna cha kujibu bali wanawatakia Pasaka njema".

Hii ni dalili ya kiburi cha kulewa madaraka au malaika mkuu katoa direct order. Tutarajie wasiojulikana zaidi kama majibu ya nyaraka hizo.

Haki ya kupata habari haipo walio na madaraka wanaamua watakavyo.

Serikali iache unafiki. Imeshajibu sana humu jf kupitia watu wao waliowamwaga kama ndezi. Wengine wamemwagwa na Lumumba kwa buku 7.
 
Hoja hazijibiki zile waache usanii. Yote yaliyoongelewa mle ni kweli tena kweli tupu; ujumbe murua kabisa wa Mungu mwenyewe kwa watu wake kupitia kwa watumishi wake. Hata kama siku za nyuma walikosea au walichelewa KUONYA ili taifa lipate kupona (maana ndio wito wao mkuu), but at last sauti imesikika kutoka "nyikani".

TAIFA LINAANGAMIA ndicho nilichokielewa kutoka katika nyaraka zile za kinabii za Wahashamu Maaskofu. Mwenye kushupaza shingo na aendelee kushupaza maana anguko li mlangoni kwa mpumbavu asiyejua kuzisoma nyakati na majira.
 
Ujumbe wa Kwaresima toka Baraza la Maaskofu Katoliki na Ujumbe wa Pasaka toka Baraza la Maaskofu Kiluther wanatukumbusha kudumisha uhuru na umoja huku kila mtu akiwajibika kwa nafasi yake bila kuathiri shughuli zetu za maendeleo. Wenye Masikio wamesikia na wenye Macho wameona.!
 
Safi saana dr abas, tafsiri yake kile kikundi cha ukawa kimepuuzwa...badala yake serikali iendelee kukamatia pale pale bila kubadili hata nukta moja!!!.
Serikali haiwezi kuyumbishwa na vitamko uchwara.
 
Zile hoja ni ngumu kwao kujibu,kwa namna walivyoiseti nchi kwa sasa,watapiga chenga tu,kama hivyo ambavyo wameshaanza
 
kutunga uongo ni kazi sana, tuwape mda wapo wanaandaa movie yao mpya!

ikumbukwe ya abdul nondo haijaisha
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom