Msemaji wa Serikali: Nimeulizwa kuhusu matamko, hatuoni cha kujibu zaidi kuwatakia Pasaka njema

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
IMG_20180325_165008.jpeg

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi:

"Nimeulizwa sana kuhusu haya matamko, nasisitiza, kwa sasa hatuoni cha kujibu zaidi ya kuwatakia waumini na waamini wote Pasaka njema".

====================

Baadhi ya Matamko:

> WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

> Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...
 
Huyu jamaa huwa ana majibu mafupi lkn yana uzito sana, Lissu alipotaka kuanzisha ligi na serikali jamaa alimwambia " hatuwezi kulumbana na mgonjwa ila tunamtakia matibabu mema" . Tokea siku hiyo Lissu hajawahi kuitisha tena press.
Jamaa huwa yuko makini.Mimi binafsi namkubali
 
Busara ni kuita viongozi wa dini zote viongozi wa vyama vya upinzani vyote wazungumze. Akiendelea kuachilia wajinga fulani wazidi kuijibia serikali, mwisho wa yote utakuwa mbaya sana.
Ukitengwa na kanisa au msikiti umetengwa na Mungu...
 
Pohamba nahisi ungeweza kabisa kuwaza zaidi ya hapa. Nadhani hukutaka tu

Pasaka njema Ndugu yangu!

'...Tangu tupate Uhuru Nchi hii haijawahi kutawaliwa na Mlutheran na hii ndio zamu yenu...'-Edward Lowassa kanisani Tabora 2015
 
View attachment 724914Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi:

"Nimeulizwa sana kuhusu haya matamko, nasisitiza, kwa sasa hatuoni cha kujibu zaidi ya kuwatakia waumini na waamini wote Pasaka njema".
Huo ndio ukomavu wa kisiasa so kuja na vitisho kwa taasisi za kidini.
 
Back
Top Bottom