Chama chetu sisi tunashangilia kila nchi inapopigwa mkuu.Sio uzalendo katika mambo makubwa na ya kitaifa kuweka ushabiki wa kivyama. Hofu ya Mungu iko wapi katika mchango wako? Kilichojadiliwa bado hakijabadilika; madai yetu ni trilioni 108, tumelipwa 700 bilioni sawa na asilimi 0.65. Tunachokisema hiki tunachokidai tungeweza kukipata bila ya kuwaita washirka wetu "majizi"! Hebu fikiria lugha yetu wakati ule na ya sasa!
Ilipokamatwa Bombadier tulisherehekea na vigelegele. Kamanda Tundu Lissu aliitisha waandishi wa habari kwa mbwembwe. Sasa hawa Barricks vipi?
Kwa nini wanatusaliti sisi ambao tunawatetea kiasi hiki?
Yaani wanatulipa wakati sie tulikuwa tukiwapigania watushitaki ili tuwalipe kama wale jamaa wa Bombadier?
Kamanda Lissu akisikia hili anaweza pata vidonda vya tumbo kwa mawazo.