GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,518
- 108,793
Mara baada ya kufungiwa jana Gazeti la Raia Mwema kwa Siku 90 niliweza kufuatilia mijadala mbalimbali ya Wadau na Watanzania wa kawaida tu ambapo mwishowe nikaja kugundua kwamba kumbe nchin Tanzania kuna Watu hawana hata hizo PhD au Elimu yoyote kubwa lakini pengine wanaweza wakawa wanajua Kufikiri kuliko wenye PhD zao.
Huyu Mdau mmoja ndiyo ama hakika amenifanya sasa niamini kwamba kweli Tanzania ni nchi ya Watu wenye akili, maarifa na upeo mkubwa sana kutokana na jinsi alivyomjibu Kihoja kabisa mwenye PhD yake hasa baada ya huyo mwenye PhD yake ambaye ni Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi hasa pale aliposema kwamba Kufungiwa kwa Gazeti la Raia Mwema kunatokana na Kosa la Kitaaluma.
Ifuatayo ni nukuu ya huyu Mdau ambapo aliamua kumjibu mwenye PhD yake pale tulipokuwa Kijiweni Kwetu jana jioni..." kama Serikali kupitia huyo Msemaji wao Dkt. Hassan Abbasi wanasema kwamba wamelifungia Gazeti la Raia Mwema kwa Kosa la Kitaaluma wakati ukweli wa Sheria hii mpya ya Vyombo vya Habari iliyosainiwa tulikubaliana kwamba kama ni Kosa la Habari basi adhabu iende moja kwa moja kwa huyo Mwandishi ila Gazeti liachwe. Mbona miaka kadhaa iliyopita kuna Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili walifanya Oparesheni ndivyo sivyo ambapo mmoja alifanyiwa ya Kichwa badala ya Mguu na mwingine ya Mguu badala ya Kichwa lakini baadae waliochukuliwa hatua walikuwa ni wale wale Madaktari na si Hospitali nzima ya Muhimbili? Je ni kwanini haki hii hii isiendelee pia hata katika Tasnia nzima ya Uandishi wa Habari ambayo hata na yenyewe ina hadhi sawa na Tasnia ya Udaktari? "
Wenye PhD zenu kama ya Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi karibuni katika uzi huu ili nanyi pia muweze kujibu hoja za huyo Mdau ambaye kiukweli Elimu yake ni ya Kiwango cha chini ili Sisi wanajamvi sasa tuweze kupima kati ya Watanzania wenye PhD na wasio na PhD nani ukweli wana akili na uwezo mkubwa wa kujenga hoja zenye mashiko.
Mimi nisiye na PhD GENTAMYCINE nawasilisha.