Msemaji wa Ikulu anasema hajui kama Raisi kapewa Ripoti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msemaji wa Ikulu anasema hajui kama Raisi kapewa Ripoti!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kuhani, Jul 18, 2008.

 1. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sakata la EPA: Mambo mazito!

  2008-07-17 19:11:17
  Na Mwandishi Wetu, Jijini


  ...Leo asubuhi, Alasiri lilipojaribu kuwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ili kujua kama timu iliyoundwa na Rais mwezi Januari mwaka huu imeshawasilisha ripoti yake kama ilivyotakiwa, lilijibiwa kuwa mhusika yuko safarini.

  Hata hivyo, Afisa aliyejitambulisha kama Kaimu Msemaji wa Ikulu, ameiambia Alasiri kuwa hadi sasa, yeye hajui kama ripoti hiyo imeshamfikia Rais au la.

  ``Binafsi, hadi sasa sijajua kama ripoti hiyo imekabidhiwa kwa rais au la. Lakini wasiliana na Msemaji Mkuu baadaye ili uweze kujua zaidi ... hivi sasa yupo ziarani,`` akasema.

  Source: Alasiri/Ippmedia


  Msemaji wa Rais kama hujui kitu ambacho inabidi ukijue inabidi usema nipeni muda kidogo nifuatilie, nita get back to you with that information. Msemaji wa Raisi inabidi ajue details zote za Raisi. Sio kwamba apayuke kila siri ya Ikulu, ila kama ni kitu ambacho Waandishi wanaweza kuuliza inabidi huwezi kusema hujui kama Raisi kapokea Ripoti.

  Halafu jamaa hajui kaimu maana yake nini. Wewe ndio ume step up to the plate wakati mwenyewe hayupo. Huwezi kusema subirini mwenyewe arudi. Sasa kaimu maana yake nini, kupokea simu na kuchukua message zake?

  Yani Bongo hata mimi nisiejua chochote naweza kuwa a better msemaji wa Raisi jamani! Yani kwa kuangalia press conference za Whitehouse kwenye C-SPAN tu jamani!

  Mnaona Wakuu wetu walivyokuwa incompetent? Sijui ni generation yao haina exposure ya Kimataifa?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawa ni mafisi hawana wakati na kushugulika na mambo muhimu yanayohusu sehemu zao za kazi wao wapo hapo kutazama dili zinazoangukia pembeni ili wapate mlo ,aidha kama una matatizo na ikulu au mambo yako inabidi yapate saini na mihuri ya ikulu basi hao ndio watu wa kuzungumza nao. Lakini sio kuwaendea na kuwauliza kama Rais amepokea ripoti ya mahujaji au leo ameandaliwa Chakula gani watakwambia kama mhusika hayupo au wao sio wazungumzaji wakuu.Tena atakuona umempa kazi kubwa sana ambayo yeye hahusiki nayo kabisa kama haitoshi anaweza akakwambia kazi yake ni kuhakikisha mifugo na mapambo ya ikulu yanafanyiwa ukarabati.
  Yaani utapewa jibu wewe mwenyewe utashangaa na kuridhika kabisa kama umefika na kumuuliza mtu ambae hahusiki kumbe anahusika na ndio mkuu.
   
 3. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145


  Mwiba Acha Hasira Kaka......lakini Nakubaliana Na Wewe Inakera Sana, Sasa Mtu Huyo Huyo Kesho Utasikia Kapewa Kazi Ya Usemaji Mkuu...atasema Kweli
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kazi za kuangalia sura na kujuana ndio majibu yake haya
  inakuwaje mtu kama huyo hajui maana ya kukaimu, haya bwana watu wanaofaa hizo nafasi wanazikosa wanapeana mafisadi na watoto wao

  yale yale kumtoa balali na kumuweka Ndulu wakati alikuwa ndani hapo hapo akijua kila kinachoendela, mtasikia huyu ndiye mrithi wa myeyushaji na mropokaji Salva siku moja.

  Hiyo ndio Tanzania chini ya anayejifanya Bubu siku hizi, asemi kitu wala hasikii kitu
   
Loading...