Msemaji Mkuu wa Serikali: Zaidi ya watu 300,000 wapata chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Zaidi ya Watanzania 300,000 wamepatiwa chanjo ya UVIKO -19 huku mikoa ya Kanda ya kaskazini ikiongoza kwa idadi ya watu wengi.

Idadi hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 31 ya dozi zililoletwa awamu ya kwanza mwezi Julai ambazo zilikuwa 1,058,400 zilizosambazwa katika vituo 550 nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma juzi, Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema wataalamu wameanza kupeleka huduma hiyo katika maeneo ambayo hakukuwa na vituo baada ya kuona mwitikio wa wananchi wanaotaka kuchanjwa.

Msigwa alisema bado kuna msisitizo wa uhiyari katika kuchanja, lakini akaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa ya huduma hiyo ya bure ili kujikinga na maradhi hayo.

“Taarifa zinazotoka kwa wataalamu zimeonyesha waliochanja wanapofika hospitali wakiwa na maradhi hayo wanatibiwa na kupona haraka kuliko wasiochanja ambao huelekea kwenye dalili mbaya, hivyo pamoja na kwamba bado tunasisitiza chanjo hii ni hiyari, lakini niwaombe wananchi muendelee kujitokeza,” alisema Msigwa

Mwananchi
 
Duh! Watz wengine wanasubiri hadi ifike idadi ya waliochanjwa iwe milion hamsini ndo nao wakachanjwe aiseee...
 
Tulifanya siasa ilipoingia mwaka jana bila kusikiliza wataalamu wa Afya,awamu hii tunatapatapa,idadi ni ndogo sana waliochanja mpaka sasa,tuache siasa nyepesi nyepesi ili usifiwe kumbe unaangamiza watu..
 
Back
Top Bottom