Msemaji Mkuu wa Serikali asema taarifa ya kuongezeka deni la Taifa ni potofu na iliyokosa weledi wa kiuandishi

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Msemaji wa Serikali anaandika kwenye ukurasa wake wa twitter

Taarifa ya awali: Hii habari ni potofu, iliyokosa weledi kiuchumi na kiuandishi. Wakati BoT wanaandaa ufafanuzi wa kina tuipuuze.

Habari anayoizungumzia ni ile iliyowekwa na akaunti ya mwananchi ikisema:- "Kwa robo ya kwanza mwaka huu, Deni la Taifa limeongezeka kwa zaidi ya Sh. 12 Trilioni na kufikia takribani sh 60 trilioni, Ripoti ya Benki Kuu inaonesha"

Capture1.PNG

Pia soma > Kafulila: Kwa mujibu wa Benki Kuu (BoT), deni la taifa limeongezeka kwa trilioni 3 sio trilioni 12
 
Toka Dr. Ryoba alipoenda TBC nikajua kwisha habari yake
[HASHTAG]#CaseStudy[/HASHTAG]
 
Tatizo ni kwamba Mficha jipu, litamuumbua. Likiisha iva, hujitumbua lenyewe. Ukweli haupingani. Data hazisemi uongo.
 
Watanzania tuna shida, sasa kila siku tunazua jipya na serikali inakanusha mpaka yale walio yasema au kuyaandika wenyewe. Bahati mbaya wakikanusha wanaibua maswali mengi zaidi. Sijui ni yupi wa kumuamini.
 
Back
Top Bottom