Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Rais na CCM ni wabaguzi sana umoja wetu uko mashakani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,568
2,000
Habari za jumapili!

Kwa taifa lolote au familia yoyote lazima kuwe na umoja ndio taifa au familia kuendelea au kupata mafanikio na maendeleo.

Katika hili linaloendelea nchini kwa raisi anaesema yeye ni mpenz wa Mungu mie kwa mtazamo wangu sio kweli hafanyi mapenzi ya Mungu bali mapenzi ya binadamu.

Katika matamko yake tofauti kaonyesha yeye ni CCM na kipaumbele chake ni watu wa CCM hata kadiliki kusema kwenye serikali yake lazima uteuzi ufanywe na makada wa CCM tu.

Juzi kaingilia vyombo huru kama mawakili na kudai kama hawatamchagua mtu toka CCM hatawapa ushirikiano sasa huyu ni mpenzi wa Mungu?

Haiwezekani unahubiri kuna watu wanawagawa wananchi wakati yeye ndo wakwanza kuwagawa wananchi kwa misingi ya chama na unawanyoshea kidole wale wakati vinne vinarudi kwake.

Sio siri bado kiongizi huyo anaonekana kubagua baadhi ya watu na kupendelea wakutokea kwake kanda ya ziwa na mbaya zaidi anaonekana anapendelea na kuwateuwa watu wa kabila lake na dini yake.

Ndio maana nasema rais na chama chake ni wabaguzi ila likitibuka wanawanyoshea kidole wapinzani lakini ukweli utabaki kuwa ivyo wabaguzi ni CCM na idara zake.

Tujikumbushe Zanzibar kwenye umoja wa kitaifa ilikuwa na umoja na utengamano huwezi kusema mpenzi wa Mungu then unawabugua watu wa Mungu au ni Mungu gani anaye mtumikia?
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
27,223
2,000
Wasukuma miaka yote tulikuwa tunachunga ng'ombe leo tumeingia maofisini imekuwa nongwa.yeeh!
 

mtafiti05

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
956
1,000
Sioni haja ya mtu kujihesabia sifa kwa mungu, hakna mpenz wa mungu ktk awamu ya 5, hakna mungu mwenye roho mbaya, chuki, fitina, ubaguzi, majgambo nk, mwenye hivi vitu ndani yake ni shetani! Hivyo tusilitaje bure jina la bwana wetu(Mungu) wa viumbe vyote!
 

Transcend

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
20,280
2,000
Inasemekana ! Inasemekana lakini...

Hata mkipewa nafasi serikalini mtaenda kufanya hujuma kwa chama tawala...

Sasa sijui ni kweli..
 

kiogwe

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
3,696
2,000
Mimi huwa simuelewi anavyolazimisha tumuombee huyu atakuwa na ushetani ndani yake mtu gani ana roho mbaya kiasi hiki hana huruma Kazurumu michango ya wana kagera sasa hivi wanaishi maisha magumu sana.huyu baba tukampime
 

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,372
2,000
wp_ss_20170205_0004.png
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Sasa hao TLS watakuwa wanasheria wapumbavu ambao hawajawahi kutokea.Hivi unamchagua MTU kulingana na performance au Itikadi yake??Kama TLS ni CCM ni bora kuvunja huo umoja wa mawakili hauna maana tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom