Mtyela Kasanda
JF-Expert Member
- Oct 13, 2018
- 554
- 818
Ivori wana condiments nzuri sana kwa muonekano, na labda zina muonekano mzuri kuliko condiments nyingine zote zinazozalishwa hapa bongo. Lakini bwana zina ladha mbaya, tomato sauce ya ivori ni kama imewekwa vinegar ina uchachu wa ajabu sana. Ukila tomato sauce ya dabaga hutamani kurudia ivori, kuna kauchachu kabaya kwenye ivori kanakufanya ule chipsi kwa shida. Chili nayo hivo hivo, nje ya ukali wa pili pili ambao mashaallah ni kali kweli kweli ila ladha yake mbaya. Hivi mnazalisha bidhaa mbaya ndomana bei zenu ndogo? Kama ni kweli tbs wawashughulikie aisee, bidhaa zenu zipo kila kona na bei ni ya kitanzania ila ladha ni mbayaaaaa kwakweli. Fanyeni tafiti zile ketchup za mbele kule wanafanyaje mpaka utamu unakua vile?