Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by fangfangjt, Apr 20, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima

  Elias Msuya
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa amesema ni vigumu kwa mtu asiye na taaluma ya sheria kuliongoza Bunge akiwa Spika.Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2000 hadi 2005, aliyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), hivi karibuni akizungumzia utendaji wake akiwa na wadhifa huo. Pia alizungumzia miaka 50 ya Uhuru.

  Katika mahojiano hayo, Msekwa alisema alilazimika kurudi shule, kusomea shahada ya sheria ili aweze kuliendesha vyema Bunge.

  Kauli hiyo ya Msekwa imekuja wakati Bunge la sasa likishuhudia mivutano ya kisheria baina ya wabunge na Spika wa Bunge hilo la 10, Anne Makinda.

  Katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo uliomalizika Jumamosi ya wiki iliyopita, Mbunge wa Singida Kusini (Chadema), Tundu Lissu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba alionekana kuipa wakati mgumu Serikali alipokuwa akipinga kifungu cha sheria kinachowaruhusu wanasiasa kuingilia uhuru wa mahakama.

  Katika mvutano huo ambao pia ulimhusisha, Spika Makinda, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimuunga mkono Lissu licha ya muswada huo kupitishwa.

  Katika Bunge la 10 pia kumekuwepo malumbano yanayoashiria wabunge wengi kutozijua vyema Kanuni za Bunge na sheria mbalimbali hivyo kujikuta wakivutana wao kwa wao, wakati mwingine na Spika Makinda.

  Hata hivyo, baadaye akizungumza na Mwananchi, Msekwa alirejea kauli hiyo akisema: "Bunge ni la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

  "Ni kweli walinihoji TBC, ilikuwa ni kuhusu miaka 50 ya Uhuru. Ndiyo lile ni Bunge la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

  Msekwa ambaye aliwahi pia kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1962-1970, Katibu Msaidizi wa Bunge kati ya mwaka 1960-1962 na Spika wa Bunge kati ya mwaka 2000-2005 alisema suala la Spika kusoma sheria ni la uamuzi binafsi siyo lazima.

  "Huwezi kulilinganisha Bunge la wakati wangu na Bunge la sasa. Ni kweli kazi za Bunge ni zilezile, lakini wabunge wa sasa ni wengine. Siyo lazima kwa Spika kusoma sheria, ni uamuzi wa mtu binafsi," alisema na kufafanua:

  "Adam Sapi Mkwawa hakuwa mwanasheria, Chifu Mang'enya hakuwa mwanasheria. Hata mimi nilipoanza sikuwa mwanasheria, lakini baadaye niliona umuhimu wa kusoma sheria."

  Bunge aliloongoza Msekwa lilishuhudia mawaziri wakilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa. Hao ni pamoja na Profesa Simon Mbilinyi, Dk Juma Ngasongwa na baadaye Idi Simba wote hao kutokana na nguvu ya Bunge.
  Akizungumzia kauli hiyo ya Msemwa, Spika Makinda licha ya kukiri kutosomea sheria moja kwa moja, alisema uzoefu alioupata Bungeni tangu alipotoka shule ndiyo unaomwezesha kuliendesha kwa ufanisi.

  "Nimekulia na kuzeekea bungeni, taaluma yangu ni uhasibu, lakini mimi ni kati ya wabunge wakongwe. Tangu nimetoka shule niko bungeni," alisema.

  Alipoulizwa iwapo ana mpango wa kusomea sheria ili kumudu vyema zaidi uendeshaji wa Bunge, Makinda alisema kuwa amesomea sheria katika taaluma yake ya uhasibu ambayo inamsaidia pia kuzielewa Kanuni za Bunge.

  "Kwani mimi sijasoma sheria? Mimi ni ‘accountant by professional', (mhasibu kitaaluma) na huko nimesomea sheria. Ni kweli sina ‘bachelor' (shahada) ya sheria, lakini, nina uelewa wa sheria," alisema.
  Makinda alijigamba: " Nimekuwa mbunge, 'chief whip' (mnadhimu) kwa muda wa miaka minane, nimekuwa mwenyekiti wa Bunge, yote hayo yamenipa uwezo."

  Kuhusu changamoto anazokabiliana nazo katika nafasi hiyo, Spika Makinda alisema kuwa hilo jambo la kawaida kwake, lakini akasema tatizo na jambo kubwa ni wabunge kutokuelewa kanuni.

  Hata hivyo, alisema anajitahidi kuwafundisha Kanuni za Bunge ili waendane na mwenendo wake.

  "Unajua kipindi hiki wabunge ndiyo wamekuja, wengi wao hawajui Kanuni za Bunge, wanafanya makosa na utundu mwingi. Lakini tutawafundisha kanuni, naamini, Bunge litakuwa ‘smart' siku zijazo," alisema na kuongeza:

  "Kwa mfano, sasa kuna kitu kinachoitwa ‘adjourn motion' ambapo mbunge anamtaarifu Spika pale anapokuwa akiahirisha Bunge kuwa ana hoja ya kulitaarifu Bunge, basi Mbunge anapewa dakika 15 za kujieleza. Yote hayo tutawafundisha na wengi wameshaleta maoni ya kufanya hivyo."

  Akizungumzia tukio la hivi karibuni ambalo Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje alitoa kauli iliyosababisha wabunge kurushiana maneno, Spika Makinda alisema kuwa tukio hilo lilikuwa ni kinyume cha Kanuni za Bunge.

  "Kanuni zinakataza wabunge ku-shout hovyo (Kupayuka). Ile ilikuwa ni makosa. Unajua wabunge bado wanajifunza na tutafanya ‘amendments' (marekebisho) ya kanuni ili kuwawezesha wabunge kuzoea Bunge. Kwa mfano, sasa kuna kitu kinaitwa "Committee of supply," yaani wakati wa mbunge kutoa shilingi Bungeni. Hilo nalo tutawafundisha ili waelewe," alisema.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  spika aliyetokana na nguvu za mapacha watatu hatufai
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  Heee! Anajiita accountant by professional! Ana CPA huyu? Maneno wa NBAA unasikia? By the way wahasibu wanasoma business law na sheria zingine za taaluma kama taxation na international financial reporting standands n.k sasa sijui hizi zimsaidie nini kutunga sheria! Spika ni vema awe mwanasheria hakuna mjadala hapo.
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  It was only the matter of time, now we are continuing to see what was being initiated by three people
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nchi hii bwana. Kuwa speaker wa Bunge ni kujua kanuni na uelewa wa kanuni una tokana na kuwa bungeni na kuzi soma. Sasa ina chekesha na kwa kweli kusikitisha unapo ona mtu ni mbunge miaka nenda rudi lakini hajui kanuni za Bunge.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Spika si mwanasheria, Naibu wa Spika si mwanasheria, na hata Katibu wa Bunge naye si mwanasheria!. Kukaa Bungeni tangu Adam & Eve Mama Makinda hakukufanyi wewe uwe mwanasheria na hata kuwa Chief whip hakuwezi hata kidogo kugeuza taaluma yako ya uhasibu kuw she Sheria. Historically at least, CCM imekuwa na desturi ya kuteuwa watu kwa utashi wa siasa na wewe ni zao la hiyo mis-match tendency.

  Tofauti na nyakati hizo za 'zidumu fikra za mwenyeki' kwa sasa kitendo cha kuwa na spika, naibu wake na katibu wa bunge kusimamia utungwaji wa sheria ili hali wakuu hawa hawa taaluma hii ni kudhalisha Taifa. You do not to be a brain surgen kuona mapungufu ya hii top team ya 'wavamizi' na inawezekana kabisa kemea-kemea ya Mama Makinda ni mojawapo ya jitihada zake -to intimidate wanasheria wabunge mahiri kama Lissu ili wasimvue magamba. Binafis nimekuwa naudhika sana tena sana pale Mh. Mizengo Pinda na huyu mama Makinda wanaposema maneno kama ' ...kama Spika atakavyoona inafaa...!!! Bunge linatikuwa liendeshwe kwa kufuta sheria, kanuni na taratibu zilizokwa na sio kulingana busara ya kada mmoja mmoja wa chama cha siasa. Katiba mpya inakuja na ni vizuri iwekwe kabisa kwenye hiyo katiba kwamba nafasi za Spika, Naibu na watendaji wakuu LAZIMA WAWE WAMESOMEA SHERIA. Na kusomea sheria huku ni kule kupata walau Bachelors na sio haya majigambo ya kisomo cha elimu ya watu wazima al-maarufu kuwa chief whip. Mambo ya hovyo kabisa haya.
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  wakati ccm wanampendekeza makinda kuwania uspika na kumwengua sita msekwa hakuwepo??

  aache unafiki huyo mzee.. kama alilijua hilo angewashauri hao wenzake vizuri, wameshatuwekea mzigo pale ndio anakuja kuongea hadharani
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Leo ndo wanaona? Madhara yake ni makubwa na yatawagharimu watanzania wote bila kujali chama
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Sitta ndiye aliyembwaga Msekwa 2005
   
 10. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  ni CPA Holder wa zamani sana miaka ya 70's tatizo hajaipracts alipata cpa akahamia bungeni
   
 11. m

  mataka JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mnashangaa nini? Hamfahamu Tanzania kama its matter whom you know and nt wat u know? Kwa hiyo sishangai kumwona spika c mwanasheria ilihali anaongoza chombo cha kutunga sheria. That refrect wat Tz real iz, unaenda kufanya kazi sehemu usiyo usiyo na ujuzi nako, c 2nayaona maoficn mwe2 au nadanganya?
   
 12. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mtazamo! Mama makinda ni mmoja wa CPA holders wa mwanzoni kabisa..wengine ni John Cheyo..Mustafa Mkulo! Source NBAA
   
 13. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Walio muweka spika sasa awapo madarakani.Kazi anayo huyo mama lakini acha waipate furaha kwa upinzani.Mtu asiyejua kusoma unamtanguliza aingie kwenye geti lililoandikwa KUNA MBWA WAKALI.Mwisho wake ni kutafunwa tu.
   
 14. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sawa ana CPA sasa kuwa na CPA kunahalalisha kuongoza chombo kikubwa cha kutunga sheria? Yaliyotokea zamani ilikuwa sahihi kwani kulikuwa hamna wanasheria wengi. kweli karne hii bado tunaruhusu hali iendelee. Shame up on waliomchagua
   
 15. K

  Kabathe Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sinahakika kama wausika wanapata nafasi ya kutembelea JF!
  Turudi kwenye topic
  Kuna umuhimu mkubwa wa spika kuwa na taaluma ya sheria na si sheria tu bali hata PS-PA, kwani pamoja na kwamba bunge linatunga sheria lakini spika ni kiongozi/mtawala ndani ya bunge. Kwa Makinda hana hata sifa mojawapo, sheria hajui, utawala hawezi kilichobaki ni kaachini bila ya kujenga hoja. Kigezo cha kwamba amekulia bungeni hata siku moja haimpisifa ya kuijia sheria, kwa mtazamo wa Makinda akipata nafasi ya kufanya kazi MOI kwa miaka mitano siku moja atataka kumpasua mtu kichwa!!!!
  Aache ubishi wa kijinga, achukue ushauri wa Msekwa ajiunge hata na open Univ!
   
 16. N

  Ntandalilo Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipoona hii thread kitu cha kwanza kujiuliza ni hiki cha uwepo wa Msekwa wakati wa kumpendekeza huyu mama........................ Thanks Samora kwa kuwahi.........
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  SASA SI NDIO MAGAMBA YENYEWE YANATOKA NA WEWE??? we huoni mapacha watatu ndio wanapigwa zengwe ?? na bado....
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Makinda hana kitu hapo, kama hataki kwenda shule kwa maswala yanayohusu ''sheria'' ni bora asiwe ana ''shout'' hawachie waliopiga umande kisawasawa watoe views zao.
   
 19. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Parliament of Tanzania. Pitieni hii profile link ya speaker Anne Makindi. Anaposema yeye ni professional accountant anaamanisha nn? Profile inasema alipomaliza Kilakala Girls Sec in 1970, alisoma Advanced Diploma ya ADMINISTRATION at the former Institute of Development and Management, currently Mzumbe University. Kwanini hayupo specific kama alisoma Advanced Diploma of Public Administration au hiyo ya finances, aitaje............ Na since hakuna sehemu inayoonyesha Mhe. Speaker since a-graduate IDM 1975 amesoma course yoyote, whether a short course or a long one. Labda wahasibu mnijuze, isn't finance a changing discipline? Just keen to know, nawasilisha....
   
 20. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni kweli, akiwa kama makamu mwenyekiti alikuwa na nafasi kubwa ya kushinikiza hilo kwenye chama chake, Labda tuambiwe CCM hawana wanasheria wanawake ambao ni wabunge
   
Loading...