Msekwa: Membe siyo mtu maalumu, afuate tu taratibu

Mati Mkenda

Senior Member
Mar 4, 2018
171
211
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Pius Msekwa amesema kuwa Membe asijione kuwa yeye ni maalum sana, bali anapaswa kufuata taratibu zote ambazo wenzake waliofukuzwa kabla yake wanazifuata.

Amesema Membe siyo mtu wa kwanza kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu kwani kuna watu waliofukuzwa kabla yake wakewemo Maalim Seif na Oscar Kambona ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Amesema kuna kanuni zinazoongoza chama, ambazo ziko wazi kabisa na kila mtu anajua kuwa iwapo hatazifuata basi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Amedai kuwa kanuni zilezile zilizotumika kuwafukuza wengine, ndizo hizo zilizotumika kumfukuza yeye, hivyo hakuna jipya linalopaswa kuongelewa sana kwa sasa haoni umaalum wote wa Membe kama ambavyo waandishi wa habari wanataka kumpa.

MY TAKE
Mzee Msekwa katoa ufafanuzi mzuri sana kwani wengi wameona issue ya Membe kama kubwa kuzidi zilizopita. Membe hajawa Kiongozi Mkubwa ndani ya Chama kama ilivyokuwa kwa Kambona hivyo hana umaalum wowote. Isitoshe yeye mwenyewe anasema alijua atafukuzwa, so kanuni zipo wazi kama Msekwa alivyosema. Serikali imwangalie tu kwa jicho la tatu maana yawezekana alifanya hivyo ili apate sababu ya kuingia msituni kwa ufadhili wa mabeberu wanaompa kichwa.
 
Msijifsnye hamnazo,

Membe kafukuzwa kwa sababu ya shinikizo la mwenyekiti wenu,na acheni kufananisha kufukuzwa kwa Kambona na Membe,

Kipindi Kambona anafukuzwa,nchi ndio ilikuwa inapata uhuru,usalama wa nchi upo tete,mamluki kibao,ukombozi kusini mwa Afrika umepamba moto,Nyerere alikuwa anajaribu kujenga nchi,

Sasa sasa hv,mmemfukuza ili boss wenu apumue,mnalinda uraji wenu tu.
 
Huo mfano sio sahihi.

Wakati Kambona ana fukuzwa nchi ilikuwa na chama kimoja tuu cha siasaTANU na hadi Kambona ana fariki hakurudi Ccm/TANU hivyo kumtolea Membe huo mfano inadhihirisha Babu kachoka akae kimya alee wajukuu.

Kwa Maalim Seif hali ni hiyo hiyo aligukuzwa kwenye chama na hadi leo yuko nje ya chama. Sasa mnapo muomba aandike barua ya kuomba msamaha wasiwasi wenu ni nini? Membe ni mtu mzima mwenye akili timamu muacheni muda utaongea. Kina Lowasa wakiondoka na wamerudi japo mliwatukana sana walipo ondoka, kwa Membe shida ni nini mna mbembeleza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zezeta mkubwa wewe kwann tusione kubwa akati tunamuhtaji lakini vyombo vyahabari vikojuu hasa vya kimataifa kutujuza....sasa akati anafukuzwa maalif seif na osca kambona hata TBC mlikua Nayo kama ilijuwepo kaziyake ilikua nn?....dunia ya leo bado mnakanuni zakumbana mpinzani wa mgombea kweli nyie matahira ndomana mnawahoji au kutumia mawazo ya mzee kama huyo ambae anashindwa kuchambua maswala kulingana na muda uliopo....membe ameamua kutenganisha zama eleweni hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom