Msekwa, Lowassa kuonja Ukonga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa, Lowassa kuonja Ukonga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Dec 24, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Habari katika Mtanzania Daima zinadai kuna uwezekano Msekwa, Lowassa, Kisumo na wengine wakaonja Ukonga kwa kukaidi mahakama. Habari zaidi soma hapa chini:

  Lowassa, Msekwa kortini
  • Wadaiwa kukiuka amri ya Mahakama Kuu


   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa mahakama inasubiri nini kujuka hatua?
   
 3. S

  Sammy Sr. Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MNATANIA nyie, halafu nani atanipigia kampeni 2010?
   
 4. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo utakuwa mchezo wa kuigiza tu, SISIEMU kumkamata Lowassa au Msekwa ni ndoto kwa sasa. Kitu cha kwanza wanajua kuwa SISIEMU inakabiliwa na uchaguzi mdogo kule Mbeya Vijijini, na Msekwa ni moja ya nguzo ya SISIEMU inayotegemewa kwenye kampeni zao. Kumkamata Msekwa nani atakwenda Mbeya Vijijini kupiga kampeni? Makamba hapendwi kule na ndiyo maana alipokuwa anafanya ziara zake aliishia Iringa na kurudi Dodoma.
   
 5. J

  Jim Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamna lolote. Msekwa si nguzo ya chochote. The guy is so poor kwenye kujieleza. Halafu busara zake za kijinga kweli. Na angekuwa nguzo si angeisaidia CCM kushinda Tarime.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nani Zaidi: Mahakama au CCM?
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Wakili Mabere Marando amempotosha mshitaki kwa kufungua kesi dhidi ya CCM Makao Makuu wakati issue ni ya CCM Mkoa, wilaya au tawi. Hao ni wadhamini wa CCM Taifa. Ni kawaida ukikifungulia kesi mahakamana, wadhamini ndio wanaowajibika. Bahati mbaya CCM sio Trust Fund, ni Chama. chama ni mali ya Wanachama na sio mali ya wadhamini. Huwezi kufanya attachment ya jengo la CCM Lumumba, kwa ajili ya mali ya Tawi la CCM Kariakoo. Japo jamaa anadai haki yake kisheria kwa mujibu wa katiba, amri hiyo ya mahakama itatulizwa mahali pake na hakimu atagundua amechemsha. Sijajua wakili wa CCM ni nani.
   
 8. K

  Kimbembe Senior Member

  #8
  Dec 25, 2008
  Joined: May 14, 2006
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupe aya mkubwa za kuonyesha hakimu na si Jaji kachemsha .
   
 9. A

  Atanaye Senior Member

  #9
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kichuguu,


  Kama waliendelea na ujenzi, huku wakijua kuna amri ya mahakama sina mengi. Nitasema poleni wazee.

  Kama haya ni majungu ya kisiasa, basi wapigane wanavyoweza.

  Lakini haya...

  "Jumatatu wiki hii, mfanyabiashara huyo aliwasilisha maombi katika mahakama hiyo akitaka wadhamini hao na viongozi wengine wa chama hicho wakamatwe na kufungwa miezi sita kutokana na kukiuka amri ya mahakama"


  Hii inaonesha dhahiri miujiza isiyowezekana, hata kama sheria ipo, sijawai kusikia mdai atake wadaiwa wakamatwe, na kwenda jela miezi sita.

  Atanaye Kijiko
   
 10. K

  Kimbembe Senior Member

  #10
  Dec 25, 2008
  Joined: May 14, 2006
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa madai yeye uelewa wake ni kiasi hicho ndiyo mahakamba haifuati yake bali inafuata sheria na mjuaji ni Wakili na Jaji mengine ni maneno ya kukoleza madai hili nalo mnahitaji elimu ya Oxford ? Jamani nyie JF vipi ?
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hii itakuwa amri ya pili ya Mahakama Kuu kama haitatekelezwa kisa kuna wana CCM wanahusika moja kwa moja .Mara ya kwanza ni kesi ya Mtikila na Mgombea binafsi na sasa hii ya wana CCM.

  Amri kama haitekelezwi neno utawala bora utakuwa hakuna tena na JK atakuwa anaji dharaulisha maana Majaji ni wake yeye kawateua yeye wanatoa amri zina puuzwa na hapa ni pabaya walala hoi si wajinga wako macho wana angalia kuna siku haya tutaulizana kama si hapa Duniani basi hata Mbinguni.I am watching what will be the next move .
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160


  Huyu nani huyu anataka kuharibu jina kubwa!

   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Amri hii ina maana Mkandara wewe ambaye uko hapa JF kumbe wewe ni CCM mkubwa na mdhamini sasa mwisho wako umefika .
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haaa! haaa! haaa!..
  I wish yaani ningefurahi kupanda jukwaani Kisutu maanake ningewamaliza wote!.. mimi noma bob..
  - Merry Christmas!
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wewe wewe Bob kumbe noma kihivyo....daah!! Ngoja makanjanja wa JF wakutafute sasa na deal zako za viwanja ndani ya chama!! lol Ho Ho Ho Ho :)
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  SteveD,
  Mkuu huyu ndiye Hamisi Mkandara.. anasema,
  Wee mwache huyo Mabere Marando namtafuta!.. Alaa tumwemsomesha huyu leo anataka kujifanya mjanja mjini tumemwingiza sisi na mke tumempa..Mwacheee!.. Kibongo bongo atatulia tu.
   
 17. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ujue kuwa SISIEMU ndiyo inaelekea kwenye sanda kabla ya kuanguka kifafa. SISIEMU inaamini kuwa Msekwa ni moja ya nguzo zake, ndiyo maana JK aliamua kumsogeza karibu kwenye uchaguzi Mkuu ndani ya SISIEMU. Kuna baadhi ya wanachama wa SISIEMU wako makini lakini tatizo hawako mstari mmoja na wenye chama. SISIEMU inahodhiwa na wachache na ndiyo maana wale wanachama makini hawapewi nafasi za juu au za maana. Uchaguzi huu wa Mbeya Vijijini ni mtihani mwingine kwa viongozi wa juu SISIEMU. Safari hii wameamua kumuweka kando Makamba, swali linakuja wakishindwa tena Mbeya nani mwingine atawekwa kando??? Uchaguzi huu utakuwa na mtikiso wa aina yake, kuna watu wataweza kupoteza vitumbua vyao. WATCH......
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jaji amuru Kawawa, Warioba, Lowassa wakamatwe
  Nora Damian  JAJI Alice Chinguile jana aliamuru mawaziri wakuu wa zamani, Rashid Kawawa, Joseph Warioba na Edward Lowassa na makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, wakamatwe kwa kukiuka amri ya mahakama.


  Jaji Chinguile wa Mahakama ya Kazi alitoa amri hiyo jana kutokana na wanasiasa hao wakongwe kuwa wadhamini wa CCM, ambayo inadaiwa kuendelea na ujenzi katika kiwanja kinachogambaniwa wakati kesi ya msingi ikiwa mahakamani.


  Jaji huyo pia ametaka wadaiwa hao wapelekewe maombi ya mdai ambaye ni mfanyabiashara, Ibrahim Hussein Alibah yaliyowasilishwa mahakamani hapo dhidi ya wadhamini hao na viongozi wengine wa CCM.


  Mbali na vigogo hao wa CCM, amri hiyo ya kukamatwa inawahusu Ahmed Ameir Ally, Khadija Jabir, Peter Kisumo, Job Lusinde, Hamis Mkandara, Juma Ahmed Juma na Joseph Warioba.


  Wanachama wengine wa CCM ni Ismail Idrisa (mwenyekiti wa CCM, kata ya Gerezani), Fatuma Abubakar (katibu kata ya Gerezani) na Abdulhaman Twalibu.


  Mahakama pia imeagiza wadaiwa hao wasiendelee na ujenzi katika eneo husika linalobishaniwa hadi hapo maombi ya mdai huyo yatakaposikilizwa Februari 4 mwakani.


  Jumatatu wiki hii, mfanyabiashara huyo aliwasilisha maombi katika mahakama hiyo akitaka wadhamini hao na viongozi wengine wa chama hicho wakamatwe na kufungw miezi sita kutokana na kukiuka amri ya mahakama.


  Aidha mfanyabiashara huyo pia anataka mahakama ikamate na kuuza ofisi ndogo za CCM zilizo Mtaa wa Lumumba kama adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa Mei 8 mwaka huu.


  Wadhamini hao wa CCM na viongozi wengine wa chama hicho wanadaiwa kukiuka amri ya mahakama hiyo iliyotolewa Mei 8 mwaka huu na Jaji Chinguile ya kuwataka wasiendelee na ujenzi kwenye plot namba 11 block 53 nyumba namba 107 iliyoko Mtaa wa Sikukuu jijini Dar es Salaam hadi kesi ya msingi iliyo mahakamani itakapokwisha.


  Maombi hayo yameungwa mkono na hati ya kiapo ya mdai huyo ambayo inasema kuwa Desemba 19 mwaka huu alitembelea eneo husika linalobishaniwa na kukuta wadaiwa wameanza shughuli za ujenzi kinyume na amri ya mahakama.


  Pia katika hati hiyo ya kiapo mdai anadai kuwa alipewa taarifa na wakili wake, Mabere Marando kwamba watuhumiwa hao wana mipango ya kukamilisha ujenzi ili waweze kulipangisha jengo hilo.


  Mfanyabiashara huyo alifungua kesi mahakamani hapo Aprili 14 mwaka huu dhidi ya wadhamini wa CCM na viongozi wengine wa chama hicho kwa madai ya kumuingilia katika eneo ambalo analimiliki.


  Katika maombi yake, mfanyabiashara huyo anadai alipwe fidia ya Sh500 milioni na wadaiwa kwa kuwa wameingia katika eneo lake bila idhini yake.

  Source: Mwananchi.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,828
  Trophy Points: 280
  Huu ni upuuzi asema Jaji Warioba

  Mwandishi Wetu Disemba 24, 2008
  Raia Mwema Muungwana ni Vitendo

  WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amezungumzia taarifa za kwamba anatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi akiziita taarifa hizo kuwa za kipuuzi zenye malengo maalumu.

  Akijibu hoja za kuwapo taarifa za kumatwa kwake zilizoenea kwa muda mrefu sasa, Jaji Warioba katika mahojiano maalumu na Raia Mwema wiki hii alisema kwamba amepokea hadi ujumbe wa maandishi ukionyesha kwamba anatakiwa kukamatwa na kushitakiwa.

  "Maneno hayo nimeyasikia. Kusema kweli kwangu mimi naona ni maneno ya kipuuzi," anasema Jaji Warioba, ambaye aliongoza Tume ya Kero ya Rushwa mwaka 1996, tume ambayo hadi sasa imekuwa ikirejewa na watafiti mbalimbali duniani.

  Katika hali ya kujiamini, Jaji Warioba alisema ilifikia mahali aliposafiri watu wakaamini kwamba amekwisha kukamatwa na hivyo baadhi ya watu wakawa wanaendeleza maneno ya kwamba atashitakiwa.

  "Kama mwezi mmoja uliopita nililetewa maandishi yaliyokuwa katika mtandao kwamba mimi pamoja na viongozi wengine watatu tungekamatwa muda si mrefu. Pia nilipigiwa simu nyingi na kuletewa ujumbe wa simu. Baadhi ya watu walifika ofisini kuhakikisha kweli sijakamatwa. Hawakuamini niliyowaambia kwa simu," alisema Warioba na kuongeza:

  "Mwanzo wa mwezi huu nilienda Ghana wakati wa uchaguzi. Nilikuwa huko kwa majuma mawili. Niliporudi nilikuta kuna maneno mengi sana. Baadhi ya watu waliamini tayari nimekwisha kukamatwa kwa sababu hawakuweza kunipata kwenye simu. Wengine waliniambia kwamba wanazo habari za uhakika kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwamba kesi dhidi yangu imekamilika."

  Alisema kwa hakika anaona maneno hayo ni majungu yanayoenezwa na watu wenye ajenda binafsi. Alisema Warioba:

  "Msingi wa jambo hili ni kampuni ya kusafisha dhahabu ya Mwananchi Gold. Mwaka 2006 baadhi ya magazeti yaliandika habari ambazo iliziona kuwa ni kashfa. Tulipeleka kesi mahakamani kushitaki magazeti hayo na maandalizi yote ya mahakamani yamekamilika na kilichobaki ni kupangiwa siku ya kusikilizwa," alisema.

  Jaji Warioba alisema suala hilo lilijadiliwa pia bungeni kupitia kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POC) iliyobainisha kwamba hakukuwa na kashfa yoyote katika mradi huo wa kusafisha dhahabu na hivyo kuendelea kushangazwa na maneno yanayoendelezwa dhidi yake kuhusiana na mradi huo.

  "Kinachonisikitisha ni kwamba mradi wa kusafisha dhahabu ulikuwa na manufaa makubwa kwa taifa. Kama mradi usingevurugwa dhahabu yote ya Tanzania ingekuwa inasafishwa nchini. Tungeweza hata kusafisha dhahabu kutoka nchi jirani. Lakini kwa sababu ambazo mimi sizijui, inaonekana wazi kuna watu wanataka mradi ufe," alisema.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POC), Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amekiri kujadiliwa kwa suala hilo katika kamati yake na akasema kwamba suala hilo lina matatizo ya kitaalamu zaidi ambayo hayamgusi Jaji Warioba na kwamba yuko tayari kumtetea mahali popote mwanasiasa huyo mstaafu.

  "Ni kweli hili suala lilifika katika kamati yetu na kwamba wanaotaka kumshitaki Jaji Warioba kwa hili naona hawako sahihi. Nasema nitakuwa wa kwanza kwenda mahakamani ama popote kumdhamini Jaji Warioba na ikibidi kumtetea," alisema Zitto.

  Habari za ndani ya Kamati ya POC zinaeleza kwamba, suala la Mwananchi Gold lilitolewa ufafanuzi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, ambaye alielezea sababu za kukwama kwa mradi huo ambao ulilenga kusaidia wachimbaji wadogo na pia kusaidia kuongeza thamani dhahabu ya Tanzania.

  Katika kikao hicho, Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Elisa David Mollel, alitaka kujua kuhusiana faida ya BoT katika hisa zake ndani ya kampuni ya Mwananchi Gold, baada ya kuwekeza 272,000,000/- kwa miaka mitatu bila kupata faida na badala yake kampuni hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa hasara.

  Gavana Ndulu alisema madhumuni ya mwanzo Serikali ilipoamua kushiriki kwenye kampuni hiyo ilikuwa ni kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo wakitarajia kuuza dhahabu yao kwa asilimia 85 ya bei ya soko la dunia ili faida itokane na tofauti baada ya usafishaji.

  "Bodi yetu iliamua ya kuwa BOT itasitisha ushiriki wake wa kwenye kampuni hii, itataka ilipwe mkopo wake uliotoa kwa kampuni hii kwa shughuli na imepeleka taarifa hiyo kwa Bodi ya Mwananchi Gold na matarajio yetu ni kwamba hii ni shughuli ambayo tutakuwa tumejiondoa," alisema Ndulu.


  Kuhusiana na sheria kuruhusu BoT kufanya biashara, Gavana Ndulu alikuliwa akisema kwamba wanaruhusiwa kuingia kwenye shughuli zozote za bullion ikiwa ni pamoja na vito vya thamani na dhahabu na kwamba si mara ya kwanza na pia hufanyika nchi nyingi duniani.

  Gavana aliwaambia wajumbe wa POC kwamba walitarajia usafishaji dhahabu ungefanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na kuamini kwamba wananchi watauza dhahabu kwa asilimia 85 ya bei ya dunia.

  "Sasa huyo huyo mwananchi unataka kumsaidia anasema hapana, mimi nataka asilimia 99. Sasa kama faida yako ilikuwa itokane na hiyo difference inakuwa haiwezekani. Kwa hiyo sisi tumeona prospectively ingawa kampuni inaangalia uwezekano wa kupata mwekezaji atakayeingia labda katika down stream ya kutumia dhahabu kutengeneza vito na vitu kama hivyo; lakini hili si eneo ambalo BOT wangehusika," alisema.

  Mbali ya BoT kuwa na asililimia 35 ya hisa katika kampuni ya Mwananchi Gold Limited, kampuni nyingine zenye hisa ni Mwananchi Trust Limited yenye asilimia 30, Chimera Limited asilimia 20 na NDC asilimia 15.

  Mashitaka yanayotajwa tajwa dhidi ya Warioba yanaelezwa kuweza kuwa na mkono wa kisiasa wenye lengo la kupunguza kasi ya "kelele za ufisadi" zinazoendelea kupigwa na wananchi na mwanasiasa huyo mstaafu kuonekana kuwa ‘mwiba' kwa wanasiasa wa sasa hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Hakuna aliyepatikana kuweza kuzungumzia kwa hakika kuhusiana na mashitaka dhidi ya Jaji Warioba, ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Edward Hosea kutopatikana wiki hii.
  Takukuru ndio wanaotajwa kuchunguza mradi wa Mwananchi Gold kwa muda mrefu sasa.

  Kwa upande wake, DPP, Elieza Feleshi, hakuweza kupatikana pamoja na simu yake ya mkononi kuwa inaita mara kadhaa bila majibu na wakati mwingine kupokelewa na hatimaye kukatwa.

  Pamoja na watendaji hao kutopatikana, mmoja wa maofisa waandamizi wa TAKUKURU ameithibitishia Raia Mwema kwamba kati ya kesi kadhaa inazoandaa TAKUKURU kesi ya Mwananchi Gold imo.

  Raia Mwema imewahi kuambiwa kwamba baadhi ya wakurugenzi wa Mwananchi Gold kama Yusuf Mushi wamepata kutafutwa wahojiwe lakini ikashindikana kwa ugonjwa na kwamba Mkurugenzi mwingine, Vulfrida Mahalu katika siku za karibuni amehojiwa mara mbili na taasisi hiyo. Hakuna aliyepatikana kueleza undani wa mahojiano hayo.


  Mwanasiasa mmoja mkongwe ameliambia Raia Mwema kwamba kwa sasa Warioba ni mmoja wa wanasiasa wanaoonekana kuwa mwiba kwa wanasiasa wa sasa kutokana na msimamo wake usiotetereka na kuwa mtu pekee asiye na makundi.

  "Warioba anaonekana kuwa tishio kwa wanasiasa wengi kwa kuwa hatetereki na hana makundi na kwa kuwa kwake na mahusiano na wanasiasa wa makundi yote na hata wa upinzani na wasomi wengi anawatisha zaidi. Hilo inadaiwa haliwapendezi wengi na kwa kweli wanaweza kutafuta kitu cha kumdhibiti kabla ya mwaka 2010," alisema mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya chama tawala kwa miaka mingi.


  Habari zinaeleza kwamba kesi zilizokwisha kufunguliwa mahakamani na nyingine zitakazofunguliwa zitalenga kushusha joto la kisiasa lililopanda kutokana na kuonekana kana kwamba watawala hawachukui hatua thabiti juu ya tuhuma za ufisadi zinazowakabili wanasiasa na matajiri kadhaa walio karibu na chama tawala wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Kesi hizo, zinatakiwa ziendelee hadi hata baada ya 2010 ili kutoa picha kwamba utawala umedhamiria kupambana na ufisadi hata kama kesi hizo zitakuwa zikitajwa tu na watuhumiwa, hasa wale wa EPA wakiwa wanaendelea na kesi hizo.

  Kesi hizo zitakuwa zikiendelea tu mahakamani kama ambavyo imekuwa ikiendelea nyingine ya aina hiyo ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, bila ya kuwa na mwisho.

  Kesi za hivi karibuni, ambazo nazo zimeibua mjadala ni zile zinazowahusu mawaziri wa zamani wa Mkapa, Daniel Yona na Basil Mramba pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja. Wote watatu walishitakiwa kwa mambo waliyoyafanya wakiwa serikalini na walisota rumande kwa siku kadhaa kabla ya kupata dhamana.
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa nini matokeo ya kamati au tume ya Warioba kuhusiana na Rushwa haiwekwi wazi? Kina Zitto na Dr. Slaa, tumieni mamlaka yenu kama Bunge kuitaka hii ripoti iwekwe wazi!
   
Loading...