Msekwa chunga mdomo wako; Inakuwaje unalaumu Katibu Mkuu kumuita mwanachama kupitia jukwaani lakini hauongelei mwanachama kumjibu kupitia mitandaoni?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Spika na Makamu wa CCM Mstaafu, Pius Chipanda Msekwa, akihojiwa na Mwananchi, amemlaumu Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kwa kitendo cha kumuita Ofisi I kwake kada wa CCM, Bernard Membe juu ya tuhuma za kumuhujumu Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

Msekwa alidai kuwa, njia aliyotumia Dk. Bashiru iko nje ya utaratibu wa CCM pale kinapohitaji kushughulikia tuhuma dhidi ya mwanachama wake. "Hii approach sijaipenda."

Msekwa alidai yeye aliwahi kuwa Katibu Mkuu, hakufanya hivyo na kwamba kama alitaka kuonana na mwanachama fulani alikuwa akimuita kwa simu ofisini kwake. "Kutangaza hadharani haina maana yoyote. Kuna taratibu za kazi, sasa kukiuka siyo jambo jema hata kidogo."

Hata hivyo, katika namna ya ajabu, Msekwa hajaongelea majibu ya Bernard Membe kupitia akaunti yake mitandaoni akionyesha dharau kwa Katibu Mkuu, Dk. Bashiru.

Ni vyema, Msekwa asilinganishe ukatibu mkuu wake wa miaka ya 1960s, kipindi ambacho Nchi ilikuwa katika Mfumo wa Chama kimoja na hakukuwepo teknolojia ya mawasiliano kama ilivyo leo ambako hujuma inaweza kufanyika na kuleta damage kubwa tofauti na zamani ambako ilikuwa ngumu kuwasiliana kwa niia yoyote.

Aidha, Msekwa anapaswa kutambua udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na Membe katika kumjibu Katibu Mkuu wake. Hata kama ametumia njia isiyo sahihi, Membe ni nani kumjibu kwa kumdunisha Bashiru kuwa ni mgeni wa kazi?

Mbona Edward Lowassa akina CCM alikuwa akitukanwa majukwaani kila siku na watu wa Membe akiwemo aliyekuwa Katibu Mwenezi, Nape Nnauye ambaye baadaye alipewa zawadi na Membe kwa kuachiwa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi? Mbona Msekwa hakujitokeza kuongelea hizo taratibu? Je ni nani alianza kuvuruga utaratibu wa kuwawajibisha Viongozi wakosaji kwa kufuata taratibu?

Ukiangalia kwa undani tabia za baadhi ya makada wa CCM, wakiwemo Membe, Nape Nnauye, Bashe na wengine kibao, hauhitaji kuelimishwa kuwa, wako busy kumkwamisha Rais Magufuli. Fuatilia Gazeti la Hussein Bashe la Mtanzania, utadhangaa kama hili ndilo Gazeti la kada anayeitakia mema CCM.

Njia aliyotumia Dk. Bashiru kumtaja wazi wazi Membe ni bora na muhimu sana na indeed imekuja kwa kuchelewa sana.

Ni wakati wa karma kuchukua nafasi yake. Ulisaidiwa na utawala uliopita kumhujumu Edward Lowassa ili aonekane mbaya na wewe ni mzuri, now it's your turn. "What goes around comes around."

IMG_0292.JPG
 
Mateso aliyoyapata Lowassa tangu kumalizika kwa Uchaguzi wa ndani wa CCM, mwaka 2012 hayana kipimo. Alitaka kufukuzwa kupitia Kampeni ya kujivua gamba mpaka pale alipolazimika kujipigania mwenyewe dakika za mwisho mwisho mwaka 2013.

Na kungekuwepo fair game ndani ya CCM ya akina Nape Nnauye, kamwe Membe asingeingia hata katika top 3. Kilichofanyika ni kuwatisha Makada wa CCM kutofanya kampeni ama kutangaza nia mapema lakini wakiwaachia wale waliowataka kuendeleza kampeni.

Chozi la aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nani wa kulifuta? Ni nini alichokuwa ameahidiwa ama ameaminishwa na utawala uliopita? Kama wengi walianguka na hawakutoa machozi why Pinda?
 
Wewe jamaa ni kiazi sana , unajiabisha kama mwanaume
Kiazi ni yule anayetukana bila kueleza kiweledi sababu ya matusi yake. Vilaza hukimbilia kutukana kama njia ya kujiliwaza coz wanayoyasoma na kuyaona yanawauma.
Ukweli utamuweka mtu huru.
Kosoa hoja kupitia hoja we kilaza. Usitumie hoja ya nguvu ila nguvu ya hoja, or no sina uhakika kama unajua hata tofauti ya maneno hayo, sorry!
 
Pius Msekwa officially endorsed Bernard Membe For 2020 presidential election!
Hata akimu-endorse haitasaidia chochote as long as majority ya wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ni watu wa Magufuli. Kama hujapita CC nani atakutambua?

Hata Msekwa akimu-endorse haitaleta tofauti yoyote.
Angalia hapa jinsi anavyomu-endorse Rais Magufuli.

 
Katibu katumia Twita, Membe katumia Twita.Msekwa anamshutumu Katibu pekee kuwa kakosea bila kumshutumu Membe
Katibu Mkuu ana ofisi Membe hana ofisi ilitakiwa katibu mkuu amwandikie barua ya kiofisi ampelekee nyumbani kwake.

Membe haishi twitter au kwenye mikutano ya hadhara, ana kwake. Kama hakujui angempa hiyo barua hata mwenyekiti wa CCM wa wilaya au mkoa ampelekee. Angeandika care of mwenyekiti wa wilaya au mkoa.

Membe si wa Kuitwa kienyeji vile. Huwezi ita viongozi wastaafu wa hadhi ya Membe like Dogs
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom