Msekwa atinga Igunga kwa kishindo; Akomba vigogo wa CHADEMA

uhuru hilo EEETI CHADEMA YASUSIWA ARUSHA
HAHAHAHAHHA SIJUI MHARIRI WAKE KASOMEA WAPI!???

mbona huwa mnaandika source: mwananchi, raia mwema, east african, sasa mbona hii haijaandikwa source? Mwenye akili anajua litakuwa aidha uhuru, jambo leo ama habari leo

Au imetungwa na aliyeileta.

Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.

Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga

Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.
Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga

Mpuuzieni huyu mpuuzi na kilaza wa JF

Hii inaonyesha wazi kuwa Mkurugenzi na Madiwani waliofukuzwa kazi wana lao jambo. Kwa nafasi za kisiasa kama Udiwani, ubunge, uwaziri na nadhani hata rais, kwa katiba yetu akipokonywa uanachama wa chama kilichompa ticket nadhani anakuwa kapoteza na nafasi yake serikalini.

Sasa huyo mkurugenzi ataendeleaje kuwatambua hao?? hembu wanasheria mtusaidie kwenye hili!

Baada ya kulalamika sana jana na kuomba muongozo,hatimae leo wamekuja na bandiko lao lisilo na mashiko ili mradi waonekane wamepost upupu wa CCM, karibuni sana wazee wa kulialia mmeshapata chai?

Ili gazeti li-qualify kuwa la udaku, moja ya sifa zake ni heading kuwa tofauti sana sana sana na content pia habari inakosa mtiririko wa logic katika content yake!!! Hivi ofisi ngapi za serikali zinanunua gazeti la uhuru? ofisi yangu ambayo ni ya serikali haina bili ya gazeti la uhuru ila Mwananchi, Nipashe na Daily News. Kuna siku nilipata lift ya gari ya CCM mkoa dereva alinunua magazeti kama manne lakini si Uhuru.

Library ya mkoa haina gazeti ka uhuru kwa sababu lina-fall under category ya udaku!! Ptyuuuuu!!!

Mods mtu akileta upupu wake hapa kama hauna source msiubandike, watu tumebaki kuspeculate tu, labda ni yeye ametunga huu ujinga

Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.

Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga

Tena kama wewe usiombe ukutane na mimi kukuzaba vibao ni sekunde tu,kwa ujuha wako wa kupost uongo,uchochezi na uchonganishi,MNOKO MKUBWA WEE.

Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.
Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga

Wacha uchochezi wewe ni mnafiki wa wana maghamba, tunakujua saana kwa post zako za ki CCM!

Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!

Kwa mtanzania mwenye kuona, Jina Msekwa ni sawa na failure, ni bora mtu uhame chadema kuijiunga na CCM kwa kushawishiwa na Sitta au Nape, si Msekwa, kwanza anayekaa na kumsikiliza Msekwa anaweza kuwa ***** sana. Sidhani wanasingida ni mabwege hivyo.

[h=2][/h] Thursday, 11 August 2011 20:28 newsroom

amsekwa.jpg
* Akomba vigogo wa CHADEMA
* Mbowe maji ya shingo Arusha

Na mwandishi wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeisambaratisha CHADEMA baada ya kuzoa vigogo wake wanne mkoani Singida. Vigogo hao walijiunga na Chama wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alipokuwa akiwasalimu wananchi katika kijiji cha Shelui, akiwa njiani kuelekea wilayani Igunga.

Waliojiunga na CCM ni wenyeviti wa wilaya za Iramba, Emmanuel Ntundu na Nakamia Wazaeli (Singida Mjini), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Iramba, Ela Dyelu na Katibu Mwenezi wilaya ya Iramba, Enelly Kingu. Msekwa aliwapongeza viongozi hao kwa uamuzi wa kujiunga na CCM na aliwataka kutimiza ahadi yao ya kuleta wanachama wengine 90. Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema kitendo cha wanachama hao ni salamu kuwa CCM inakubalika. Kutoka Arusha, Lilian Joel, anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika hali isiyo ya kawaida ameendelea kuwachochea wananchi kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Changa.

Akihutubia mkutano wa hadhara jana katika viwanja vya NMC, Mbowe alisema baada ya siku 30 atarudi Arusha kushirikiana na wananchi kuvamia ofisi za manispaa. Mbowe alisema sababu za uvamizi huo ni kupinga kitendo cha Changa kuwatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA.

"Tumesikia mkurugenzi ametamka anawatambua madiwani tuliowatimua, nawaomba wananchi, kesho tunarejea bungeni, baada ya siku 30 tutarudi kwa kazi moja tu ya kuandamana hadi katika ofisi za mkurugenzi na tutalala hapo na kushinda,’’ alisema. Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, kujiandaa vyema kwa kukusanya askari kutoka mikoa ya jirani siku ya maandamano hayo.

Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho walifika Arusha kwa ajili ya kujisafisha kwa wananchi, baada ya kuwafukuza madiwani watano wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha kutoafiki kauli na wito uliotolewa na Mbowe wa kuandamana.

Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Marando, aliwasihi madiwani waliofukuzwa wasiende mahakamani, kwa madai hakuna atakayewatetea.
Madiwani waliofukuzwa ni Naibu Meya, Estomih Mallah, ambaye ni diwani wa Kimandolu, John Bayo (Elerai), Rehema Mohamed (Viti Maalumu), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rubeni Ngowi (Themi).

Last Updated ( Thursday, 11 August 2011 20:35 )

Kweli alyebandika habari hii alikuwa na usongo!
Maana inaonekana hata gazetini ilikuwa haijatoka,yeye kabandika hapa! 20:28 newsroom

Back
Top Bottom