Msekwa atinga Igunga kwa kishindo; Akomba vigogo wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa atinga Igunga kwa kishindo; Akomba vigogo wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Thursday, 11 August 2011 20:28

  uhuru
  newsroom


  [​IMG]


  * Akomba vigogo wa CHADEMA
  * Mbowe maji ya shingo Arusha


  Na mwandishi wetu

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeisambaratisha CHADEMA baada ya kuzoa vigogo wake wanne mkoani Singida. Vigogo hao walijiunga na Chama wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alipokuwa akiwasalimu wananchi katika kijiji cha Shelui, akiwa njiani kuelekea wilayani Igunga.  Waliojiunga na CCM ni wenyeviti wa wilaya za Iramba, Emmanuel Ntundu na Nakamia Wazaeli (Singida Mjini), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Iramba, Ela Dyelu na Katibu Mwenezi wilaya ya Iramba, Enelly Kingu. Msekwa aliwapongeza viongozi hao kwa uamuzi wa kujiunga na CCM na aliwataka kutimiza ahadi yao ya kuleta wanachama wengine 90. Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema kitendo cha wanachama hao ni salamu kuwa CCM inakubalika. Kutoka Arusha, Lilian Joel, anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika hali isiyo ya kawaida ameendelea kuwachochea wananchi kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Changa.

  Akihutubia mkutano wa hadhara jana katika viwanja vya NMC, Mbowe alisema baada ya siku 30 atarudi Arusha kushirikiana na wananchi kuvamia ofisi za manispaa. Mbowe alisema sababu za uvamizi huo ni kupinga kitendo cha Changa kuwatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA.  "Tumesikia mkurugenzi ametamka anawatambua madiwani tuliowatimua, nawaomba wananchi, kesho tunarejea bungeni, baada ya siku 30 tutarudi kwa kazi moja tu ya kuandamana hadi katika ofisi za mkurugenzi na tutalala hapo na kushinda,'' alisema. Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, kujiandaa vyema kwa kukusanya askari kutoka mikoa ya jirani siku ya maandamano hayo.  Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho walifika Arusha kwa ajili ya kujisafisha kwa wananchi, baada ya kuwafukuza madiwani watano wa chama hicho.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha kutoafiki kauli na wito uliotolewa na Mbowe wa kuandamana.


  Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Marando, aliwasihi madiwani waliofukuzwa wasiende mahakamani, kwa madai hakuna atakayewatetea.
  Madiwani waliofukuzwa ni Naibu Meya, Estomih Mallah, ambaye ni diwani wa Kimandolu, John Bayo (Elerai), Rehema Mohamed (Viti Maalumu), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rubeni Ngowi (Themi).
  Last Updated ( Thursday, 11 August 2011 20:35 )
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nngu007

  gazeti gani hili ....?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Gazeti la Magamba, nina hakika. Uhuru!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  hili gazeti gani? mwe. kweli pesa mwanaharamu
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  must be uhuru!
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, unaweza kushitakiwa kwa kubandika habari ya wenyewe bila kuakinoleji source.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Watano kwa mpigo? Wameshikwa pabaya.
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  source: gazeti la uhuru, pg1
   
 9. REBEL

  REBEL Senior Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  uhuru sio gazeti.hata mleta habari anaogopa kutaja source yake.juzi nililisoma hili gazeti karibu nitapike.
   
 10. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mwandishi ni mwongo jana uwanja mzima uliitikia kwenda manspaa baada ya siku 30 sikuona mtu aliokataa labda kama ccm walikuwepo pamoja na huyu mwaandishi.  <br />
  <br />
   
 11. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Udaku mtupu!
   
 12. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kuna watu waongo dunia hii labda alihadithiwa tu na mwanaccm sisi tuliokuwepo hatudanganywi na huyu mwandishi mpuuuuuuuuuuuzi.
   
 13. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  mbona huwa mnaandika source: mwananchi, raia mwema, east african, sasa mbona hii haijaandikwa source? Mwenye akili anajua litakuwa aidha uhuru, jambo leo ama habari leo
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ukiona article ya gazeti isiyo na chanzo basi ujue ni uhuru kwani wahusika washadai siku za nyuma wakiandika UHURU uwa hamsomi.
  kwahiyo siku nyingine ukiona article imepachikwa na headline kali kama hizi basi ujue ni uhuru gazeti ambalo nafungiaka mavi ya mbwa
  wangu kwa ajili ya kwenda kutupa.
   
 15. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gazeti uhuru tunachambiaga na kufungia samaki au tumbaku.
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli viongozi wa CCM wanafikiri kwa kina kweli? Unawezaje kwenda kupiga kampeni kwenye jimbo liloachwa wazi na mwanachama wenu ambaye ameachia ngazi kwa sababu ya "siasa uchwara" na "siasa za maji taka"?

  Je, huko ni kukubaliana na maneno ya Rostam kuwa wao ni viongozi wa siasa uchwara, hivyo ni viongozi uchwara, wa chama cha siasa uchwara (yaani chama uchwara) ambacho kimeunda serikali uchwara?!!
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Uhuru source????

  Puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,640
  Likes Received: 4,747
  Trophy Points: 280
  Kumbe habari zenyewe zimetoka kwenye hiyo toilet paper inayoitwa uhuru, upuuzi mtupu
   
 19. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watu wengine bana!
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!
   
Loading...