Msekwa: Aliposaini hati ya muungano, Nyerere alipiga wine kwa furaha. Asema muungano ulitawaliwa na siri kubwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
61,885
92,409
Mzee Msekwa amesema wakati muungano unaasisiwa yeye alikuwa ni Katibu wa bunge na ndiye aliyeupeleka Ikulu muswada huo baada ya kupitishwa na bunge ili ukasainiwe na iwe sheria.

Mzee Msekwa anasema alipofika Ikulu na kumweleza Rais kuwa wabunge wote kwa kauli moja wamepitisha mswada wa muungano Mwalimu Nyerere kwanza alikunywa glass ya Wine kwa furaha kisha akausaini pale pale kuwa sheria.

Mjadala unaendelea.......

Source: Star tv

Aliyekuwa katibu wa Bunge wakati Tanganyika na Zanzibar zinaungana leo kwenye sherehe ya kumbukumbu ya muungano ameelezea yaliyojiri kwenye matukio na historia ya muungano.

Msekwa amesema chimbuko la Muungano wa Tanzania ni mapinduzi kwani Nyerere asingeweza kuzungumza na Sultan Jamsheed kuhusu muungano na wakati huo ilikuwepo haja ya kuyalinda mapinduzi hayo.

Msekwa amesema Jamsheed aliongoza kwa hila kwani inaaminika chama cha Afro shirazi kilishinda uchaguzi na Jamsheed kuiba matokeo.

Msekwa amesema jambo ambalo wengi hawalijui ni usiri mkubwa uliotawala mazungumzo baina ya marais wawili, Nyerere na Karume. Sababu kuu ikiwa hofu kubwa iliyokuwepo kwamba yangejulikana mapema, zingetengenezwa njama za kuhujumu.

Makubaliano ya Muungano yalisema Rais wa kwanza wa Jamhuri atakuwa Nyerere na makamu wake atakuwa Abeid Karume ili kuondoa haja ya kufanya uchaguzi kwasababu tayari wamewekwa na sheria.
 
Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,108
5,965

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,745
26,514
Hiyo mbona kawaida kaka. Kuna levels za majukumu kama upigi udrink kidogo unaweza kurukwa akili. Ukitoa propaganda za kidini, udrink wa kiasi ni muhimu sana ki afya.

Baada ya kazi mzaramo ( The spirit of the nation) ni muhimu sana kuiweka sawa akili na kesho
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
61,885
92,409
Hiyo mbona kawaida kaka. Kuna levels za majukumu kama upigi udrink kidogo unaweza kurukwa akili. Ukitoa propaganda za kidini, udrink wa kiasi ni muhimu sana ki afya.

Baada ya kazi mzaramo ( The spirit of the nation) ni muhimu sana kuiweka sawa akili na kesho
Hakika bwashee!
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
12,446
10,038
Hapa ndipo Mimi huwashangaa sana viongozi wa CCM.Yaani Mzee Msekwa anatoka hadharani kuja kusema uongo! ASP kama vyama vingine vilivyokuwepo Zanzibar wakati ule ,vikimtambua Sultan kama sovereign wa Zanzibar na ndiyo maana vilipewa usajiri na kuendesha shughuli za siasa.Jamshid yeye alikuwa ni WA wote na kusema aliiba kura ni uongo wa mchana kweupe.ZNP na ZPPP walikuwa wameungana na wakashinda majimbo Mengi.Kama Kuna swala la WIZI wa kura basi watuhumiwe akina Mohamed Shamte,Ally Mukhsin Barwan na wenzao ila siyo Jamshid.
 
Wewe unadhani wizi wa kura ulianzia Ufipa walipokwiba kura za Nyalandu?

Uhuni huu ni wa siku nyingi!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom