Msekwa aamuliwa kulipa deni la mil.7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa aamuliwa kulipa deni la mil.7

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 20, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, ameamriwa kulipa kiasi cha sh 7,072,000 ndani ya miezi mitatu kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.

  Amri ya kulipa fedha hizo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo wakati alipokutana na viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Cheyo alisema fedha hizo zilichukuliwa na Msekwa kutoka kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kati ya mwaka 2003 na 2004 kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake.

  Mwenyekiti huyo aliwaeleza waandishi wa habari ndani ya Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge Dar es Salaam baada ya kumaliza kikao na wizara hiyo kuwa kamati yake ilielezwa malipo hayo yalitakiwa kufanyika ndani ya kipindi cha miezi 10.

  “Kamati imeelezwa kwamba Msekwa alikopa fedha hizo kwa ajili ya matibabu ya kijana wake aliyeugua ghafla huko Ufaransa, akaahidi kulipa deni hilo kwa kiasi cha sh milioni moja kila mwezi.

  “Lakini mpaka leo ulipaji wa deni hilo unasuasua, ndiyo maana tumeiagiza wizara kuwasiliana na mdeni wao ili kurudisha fedha hizo katika kipindi kisichozidi miezi mitatu,” alisisitiza Cheyo ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki na kuongeza kwamba kinyume cha hapo kamati itajua nini cha kufanya.

  Awali, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sazi Salula aligoma kumtaja mdeni huyo kutokana na wadhifa wake ndani ya CCM, akimwelezea kuwa ni kigogo hivyo hakustahili kutajwa mbele ya waandishi wa habari na kwamba si muajiriwa wa serikalini.

  Hata hivyo, Salula alisema kigogo huyo ameandikiwa barua akikumbushwa kuhusu deni lake mara kadhaa ingawa mpaka sasa amelipa sh milioni tatu tu.

  Katika maelezo ya wizara hiyo kwa kamati ya Bunge, inadaiwa Msekwa alikopeshwa kiasi cha euro 5,924 sawa na sh 10,072,000 mwaka 2003/04 na kwamba ulipaji wake umefanyika kwa stakabadhi tofauti.

  Stakabadhi zilizotumika katika malipo ya fedha hizo ni zenye namba 33065088 ya Januari 15 na 33065118 ya Aprili 20 zote za mwaka jana.
  “Mheshimiwa tumejitahidi kufuatilia fedha hizi, ndiyo maana hata Januari 8 mwaka huu tumemwandikia barua yenye kumbukumbu namba BA43/518/79 kumkumbusha kuhusu deni la sh 7,072,000,” alisema Salula bila kumtaja madaiwa kwa msisitizo kuwa wadhifa wake alionao hastahili kutajwa mbele ya vyombo vya habari.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Arusha, Msekwa alilithibitisha kudaiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kiasi cha sh milioni sita na si saba kama inavyodaiwa.

  “Ni kweli mwanangu anayefanya kazi London alipata matatizo, nikaomba Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje inilipie gharama za matibabu pale Ufaransa nikakubaliwa, hivyo sikuona kama ni kosa,” alisema Msekwa.

  Alisema baada ya kupata fedha hizo, mwanaye ambaye hakumtaja kwa jina aliendelea kupata matibabu hadi alipopona na kurudi kazini Uingereza bila tatizo.

  “Kuanzia hapo nikiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano sikudaiwa hata siku moja na mimi nilinyamaza nikitambua kwa vile mwanangu ni mfanyakazi wao, basi atakuwa amelipiwa fedha hizo ambazo ni sh milioni 10, lakini haikuwa hivyo.

  “Nikiwa sijui kinachoendelea nilishutukia naletewa barua na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na kunieleza kwamba wamefanyiwa ukaguzi wa mahesabu na kukuta kiasi hicho hakipo… sasa nikashangaa nikijua wazi wanalipa wao kwa vile ni mfanyakazi wao, basi nilikubaliana nao,” alisema.

  Alisema baada ya taarifa hiyo, alianza kulipa deni hilo kama alivyotakiwa kufanya.

  “Nalikubali deni hili ni langu. Tulikubaliana kila mwezi niwe nalipa sh milioni moja, mpaka sasa nimebakiza milioni sita tu, sina ubishi ni kweli hata risiti zote ninazolipa deni ninazo. Pia kumbuka mimi ni Spika mstaafu hivyo nalipa kutokana pensheni yangu ninayopata,” alisema Msekwa.
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mwaka huu tutasikia mengi! Taratibu zinasema kuhusu matumizi ya pesa za umma? Anaweza kweli kupewa (hatusemi kukopeshwa maana halipi interest wala hatutegemei atarudisha katika euro) pesa ya serikali kirahisi hivyo? Halafu anayemdai kupata kigugumizi! Tunasubiri.

  Amandla.......
   
 3. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ndiyo uhuni wa wazi wazi, yaani uombe pesa ya serikali halafu ufikiri deni lilisamehewa? Na kama mwanae ni mfanyakazi wa Wizara husika kwanini aombe matibabu kupitia kwa baba yake, kwa nini asiwambie mabosi wake? This is ridiculous
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hawa wazee bwana wanatia hasira sana..eti lilikaa kimya nikijua nimesamehewa?pumbavu kabisa
   
 5. w

  wasp JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mkereketwa, tunaposema Sisiem ni chama cha mafisadi unafikiri tunawasingizia? Ona toka 2003/04 jamaa kaomba mkopo wa Euro ambao hauna riba toka ubalozini halafu analipa kwa Tsh bila hata kujua kama exchange rate ambayo inayotumika nayo inabadilika! Eti Msekwa anataka huruma kwa kuwa anatumia pensheni yake kulipia hilo deni. Kuna maswali mengi ya kujiuliza:

  1) Je pensheni ya Msekwa inafanana na ya walalahoi hata tumwonee huruma?

  2) Kwanini huyo mtoto wake ambaye anafanya kazi huko majuu asilipe deni hilo?

  3) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje hawezi kumtaja mdaiwa kwasababu ni Kigogo! Huu ni uoga wa kazi uliopindukia.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh, kumbe ubalozini kuna mikopo?? Basi mwenzetu nilikuwa mgeni. Hawa watu wamezoea kuchuma kwenye shamba la bibi sasa bibi kidogo naona anakuwa mkali. Sijui ni sarakasi za uchaguzi au ni kweli wapo siriaz.
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Teh teh..... kigogo nimepanda sana hii ya "nikijua nimesamehewa". hawa watu wamezoea kula tuuuu...... si wanajua wadanganyika tulivyo...
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Mfanyakazi wao wa wapi? Ubalozini/ Usalama wa Serikali ? na kwa nini matibabu Ufaransa na Sio Uingereza?
  Na wakumlipia alitakiwa kuwa Nani?
  “Kuanzia hapo nikiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano sikudaiwa hata siku moja na mimi nilinyamaza nikitambua kwa vile mwanangu ni mfanyakazi wao, basi atakuwa amelipiwa fedha hizo ambazo ni sh milioni 10, lakini haikuwa hivyo.
  “Nikiwa
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa nini pesa hii haikukatwa kwenye mafao yake ya mwaka 2005 alipokuwa anakurupushwa toka kwenye Uspika na wanamtandao?
   
 10. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni mifano michache inayodhihirisha jinsi viongozi wetu walivyolewa madaraka na kujiona wanamiliki nchi hii na watanzania wote. Ilikuwaje akapewa hizo hela na aliyempa ni nani, je watanzania wengine wanaweza kupata hela kirahisi namna hiyo hata kama anaumwa na amekaribia kukata roho? Huyu Msekwa na aliyempatia hizo hela wanastahili kufunguliwa mashitaka ya wizi wa hela za umma na kutumia madaraka vibaya.
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  tusimlaumu sana ilo ndio limetajwa ni kwamba ashazoea kuchukua bila kuuliza, cha kujiuliza usamehewe kama nani? je serikalini kuna kipengele kinachoruhusu mtu kuchukua pesa ya umma then akafanya jambo fulani na akasamehewa? uyu si ndio alikua spika na mkewe waziri kwa mpigo, na walishindwa kulipa ilo deni, ivi inaingia akilini then anaongea kwa kebehi eti sikuwai kukumbushwa? kwani wakati anapewa loan hakukua na time frame ya yeye kurudisha? ama kweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni
   
 12. A

  Alpha JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ridiculous! he needs to pay back the principle + interest

  :mad:
   
 13. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Jamani watz mbona tunakuwafooled kiasi hicho?
  Nimesoma original news kwenye gazeti la Mengi.
  Maswali yangu ni haya:
  1.Kijana mwenyewe anaitwa Julius Msekwa,wakati anaugua,gazeti limesema alikuwa anafanya kazi ubalozini kama Trade Office??????kama ni kweli basi angekuwa na Insurance kwa watu wanaoishi ufaransa,unless alienda private hospital!Ndio tatizo la hawa watu .kama angekuwa amesettle uingereza ,NHS ni free,kama angetoa NHS card na kwenda hospitali ya serikali huko ufaransa.

  2.Huu ni ufisadi wa hali ya juu ,mkikumbuka kuwa mabalozini ulaya,kila mtu anajua ni playground kwa viongozi wetu.Mnakumbuka Costa Mahalu huko Italy,nafikiri mke wa Kitine if alivyoforge medical bills huko huko Ufaransa.

  3.Sidhani Msekwa alikuwa tayarui kulipa hili deni!Miaka 6 mingi,wanamahesabu mcalculate kiasi gani cha interests angekuwa amelipa kama hizo pesa zingekuwa benki.Msekwa ni greedy,amekuwa muda mrefu kwenye ulaji,per diem moja tu ya kwenda kwenye mabunge ulaya,ingelipa.

  tupeni CV ya Julius Msekwa
   
 14. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara :D
   
 15. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #15
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  “Baada ya kuwasiliana na wizara na kukubaliana kuhusu fedha hizi, hawakuwasiliana nami hadi nilipostaafu mpaka nikadhani nimesamehewa, lakini niliwaomba msamaha na kuanza kulipa, sikuwa na nia ya kuirusha Serikali hata kidogo, kwani hata katika taarifa ya mali zangu kama kiongozi nimelitaja deni hili.” - Pius Msekwa

  ...............................................................
  Sakata la kudaiwa na serikali shilingi milioni 7
  Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=5317
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Kazoea vya kunyonga, vya kuchinja ataviweza?

  Viongozi wa bongo jambo la aibu wanalifanya la kawaida, ukadhani umesamehewa? Ukadhani umesamehewa? Ulidhanije? Nani alikuandikia kukuambia umesamehewa? Au unataka kusema ukadhani watalifuta kwa kukuogopa wewe Msekwa?

  Aibu aibu aibu.

  Wenzetu hata ukimpeleka sehemu ukamnunulia kitu kama hamna uhusiano wa kueleweka atakazania kila mmoja alipe kwa proportion yake.George Bush mkubwa alivyokuwa anafanya campaign ya urais, kuna mama mmoja mshabiki wake huko Texas alimnunulia kitu cha kula, George Bush akawa anamlipa back hela yule mama, mama akakataa, George Bush akawa kama anamlazimisha, mama akaendelea kukataa, George bush akasema "The record will show that I tried to pay back" yaani aliona ni lazima alipe, ikamuuma kwamba huyu mama kampa deni.deni linauma. Sio Msekwa, usipom harass kwenye makamati ndio usahau.

  Wangapi kati yetu tuna madeni ambayo hatujayalipa na wala hatuna mpango wa kulipa?
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  sasa wale wanafunzi wanaodaiwa mikopo itakuwaje kama na wao wanadhania "wamesamehewa"?
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Umekumbusha mbali sana Mwanakijiji, sijui lini nitaanza kulipa, maana nami nahisi nimesamehewa teh teh teh teh
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  I believe unamuongelea Pius Msekwa na si Julius Msekwa.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Haya maneno kutoka kwa mtu kiongozi na mwansiasa wa muda mrefu, mwenye kuheshimika ktk duru za uongozi na siasa Tz na nje ya mipaka ya Tz, tena mmojawapo wa nguzo za chama twawala. Baba wa familia na haidhuru ana watoto wakubwa tu, wajukuu na pengine na vitukuu na vilembwe.

  Kazi tunayo.
   
Loading...