Msechu (NHC): Natekeleza ilani ya CCM

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Wandugu nimeona news muda huu na nimemsikia Msechu anasema kwa kusisitiza anasema ayafanyao yeye huko NHC anatekeleza ilani ya CCM.

Kindly guys help me to understand, hii imekaaje?
 
Mkuu Lunyungu, hii ilani ya CCM inahusu nini ilitolewa lini? kwenye kampeni za uchaguzi wa 2005 au 2010?
 
Ukimkanyaga
Simba,unampulizia kidogo wewe unataka asemeje wakati Ikulu ndiyo imemweka hapo.
 
Namimi pia nipo curious kujua ni kipengele gani cha ilani anachoreffer na kwa kutetea hatua gani anazochukua sasa...
 
Ametaja kipengere husika lakini hajakosea kabisa. Mtumishi yeyote wa serikali anatekeleza sera na ilani ya chama kilichopo madarakani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Code of Ethics and Conduct for Public Service chini ya kipengere kinachohusu "Loyalty to the Government" subsections:
1. Public Servants shall be loyal to the duly constituted government of the day
2 " Public servant shall therefore implement policies and lawful instructions given by their Ministers and other government leaders"Ndio maana serikali inapochemsha watu wanakilaumu Chama cha Mapinduzi
 
Umeukata mzizi wa fitna!!
 
Wandugu nimeona news muda huu na nimemsikia Msechu anasema kwa kusisitiza anasema ayafanyao yeye huko NHC anatekeleza ilani ya CCM.

Kindly guys help me to understand, hii imekaaje?

Mchechu hajakosea Serikali iliyoko madarakani ni ya CCM hivyo mikakati waliyokuwa wakiwaeleza wananchi wakati wa kmuomba ridhaa ya kuongoza nchi na kuikubali hadi kuwachagua kuwa madarakani wanatakiwa kuitekeleza. Hivyo wanasiasa na watendaji Serikalini wanatakiwa kutekeleza Ilani waliyoiuza kwa wananchi wakainunua.
 
Yeye amefanya kusema tuu kiuwazi, wengine hawasemi but thats how it is and actually, what they do!
 
Msechu my hero,

Aliwatumia vijana wa chadema pale UDSM walikusanywa na Dr mkumbo wawape pressure wahindi...

Angalizo vijana wa chadema are very cheap..to organize
 
Ametaja kipengere husika lakini hajakosea kabisa. Mtumishi yeyote wa serikali anatekeleza sera na ilani ya chama kilichopo madarakani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Code of Ethics and Conduct for Public Service chini ya kipengere kinachohusu "Loyalty to the Government" subsections:
1. Public Servants shall be loyal to the duly constituted government of the day
2 " Public servant shall therefore implement policies and lawful instructions given by their Ministers and other government leaders"Ndio maana serikali inapochemsha watu wanakilaumu Chama cha Mapinduzi
Hapo nimekuelewa. kwa hiyo imekaa kisheria zaidi? Kwa hiyo hata mbunge kama mch. msigwa hapa iringa anatekeleza sera za chama cha mapinduzi?
 
Lunyungu... cha maana ni kuperuzi ilani na kuoanisha, the guy is good but the best thing for him is to stay out of politics
 
Ametaja kipengere husika lakini hajakosea kabisa. Mtumishi yeyote wa serikali anatekeleza sera na ilani ya chama kilichopo madarakani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Code of Ethics and Conduct for Public Service chini ya kipengere kinachohusu "Loyalty to the Government" subsections:
1. Public Servants shall be loyal to the duly constituted government of the day
2 " Public servant shall therefore implement policies and lawful instructions given by their Ministers and other government leaders"Ndio maana serikali inapochemsha watu wanakilaumu Chama cha Mapinduzi

Kipengele ilikua muhimu kukitaja ili tujue kama kweli tafsiri ya hicho kipengele inaendana na mambo yanayofanywa na NHC.
Mfano, kutengeza forms za kutaka kujua rangi ya ngozi ya wapangaji(racial profiling) imeandiakwa kwenye hiyo ilani? Huku tukijua
jinsi waasisi wa taifa letu walipingana na ukaburu kwa kila hali?

Na je serikali ya CCM inayosema haiwezi kupandisha kima cha chini cha mshahara kufikia laki tatu na nusu mpaka kurisk migomo
inapata wapi ujasiri wa kubariki viwango vipya vya kodi anavyopendekeza bwana Mchechu vya laki 5 kwa mwezi? Je sababu kuu
ya uanzishwaji wa NHC inazingatiwaje hapa ya kuwapatia affordable housing wananchi.

Isije kuwa "Natekeleza Ilani ya CCM" ikawa ni tired slogan isiyokuwa na mashiko yeyote.
 
Sasa kama hivyo huko NHC si lazima uwe na kadi yao ndiyo upate kazi na huduma zingine kwa mwendo huu ?
 
Ametaja kipengere husika lakini hajakosea kabisa. Mtumishi yeyote wa serikali anatekeleza sera na ilani ya chama kilichopo madarakani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Code of Ethics and Conduct for Public Service chini ya kipengere kinachohusu "Loyalty to the Government" subsections:
1. Public Servants shall be loyal to the duly constituted government of the day
2 " Public servant shall therefore implement policies and lawful instructions given by their Ministers and other government leaders"Ndio maana serikali inapochemsha watu wanakilaumu Chama cha Mapinduzi

Hapana, yeye kama mtumishi wa shirika la umma anatakiwa atekeleze sheria iliyounda shirika lile, siyo ilnani ya chama au tamko la kiongozi yeyote aliyeko madarakani. Ilani ya CCM haijawa sheria ya nchi na wala haitambuliki kisheria. Ni muhimu kwa CCM kupeleka ile ilani yao bungeni, kwa vile ni wengi waipitishe kuwa kitu kama "Sheria ya Mweleko wa Taifa kwa Kipindi cha 2011 hadi 2015", hapo ndipo vyombo vingine vya umma vitakapotakiwa kuifuata kwa mujibu wa sheria, na vinapoifuata havisemi kuwa vinafuata ilani ya CCM bali vitakuwa vinatekeleza sheria iliyopitisha na bunge kutokana na ilani hiyo.
 
Wandugu nimeona news muda huu na nimemsikia Msechu anasema kwa kusisitiza anasema ayafanyao yeye huko NHC anatekeleza ilani ya CCM.

Kindly guys help me to understand, hii imekaaje?
hapo kwenye red anaitwa Mchechu sio Msechu, msechu ni mwanamuziki aliyeshiriki Tusker firm. kuhusu yeye kutekelezwa ilani ya ccm hiyo ni kweli kabisa kwani kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma; watumishi wa umma watatekeleza sera, mipango na mikakati ya serikali ilyopo madarakani. nafikiri kila mtu anajua wazi kwamba serikali iliyopo madarakani ni ya chama cha mapinduzi, ambayo ina ilani yake ya uchaguzi, ndani ya ilani hiyo tukapata mipango mbalimbali, na kwenye mipango hiyo tukapata mikakati mabalimbali ambayo inatekelezwa katika nyanja mbalimbali. upo hapo mkuu?
 
Hekima na busara nyingine watu sijui wanazitoa wapi, eti anatekeleza ilani ya chama cha serikali inayotawala kwa kuivua nguo serikali tawala hadharani. Busara yangu inanituma ni mshauri huyu bwana Nehimia anze kutafuta kazi sehemu nyingine, maana hapo NHC kwa wenye akili ndio kibarua kimeshaisha hivyo, hayo mengine ni suala la muda tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom