Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Msechu 'kachakachuliwa' Tusker Project?
na Andrew Chale
KILE kitendawili cha atakayenyakua taji la Tusker Project Fame 2010 kiliteguliwa juzi baada ya Mganda Davis kuibuka kidedea huku mshiriki wa Tanzania Peter Msechu akiambulia nafasi ya pili. Tangu kuanza kwa shindano hilo ambalo lilikuwa likirushwa kila wiki na kituo cha TBC1, Msechu alionekana kungara vilivyo hadi kufanikiwa kuingia hatua ya fainali.
Hata hivyo, awali kulikuwa na tetesi za shindano hilo kuingiliwa na itikadi za kisiasa, huku baadhi ya Watanzania wakilalamikia kuchakachuliwa kwa kura zao walizokuwa wakimpigia Mtanzania huyo.
Hata hivyo, katika fainali hizo Msechu aliibuka nafasi hiyo ya pili, baada ya kupambana vilivyo hadi kufikia hapo kwa nyimbo zake ambazo ziliweza kuteka mashabiki wengi.
Msechu ambaye alipewa nafasi kubwa kushinda, alikuwa akishangiliwa kila alipopanda jukwaani na kukonga vilivyo mashabiki, huku akiwa anatumbuiza na msanii raia wa Burundi, Kidumu ambaye walirandana vilivyo.
Wakati wa kutumbuiza mmoja mmoja, Msechu aliimba wimbo wa Nipate Nafasi ulioimbwa na gwiji wa zamani Ahmad Kipande, ambapo aliweza kuongeza vionjo vyake huku akimsifia mtoto Juliana, ambaye anasema tangu aende Kenya alitokea kumpenda.
Lakini alishindwa kusema na ameamua kumwambia mbele za watu, Juliana naumiaaaaa ndio kilikuwa kiitikio cha wimbo huo na mashabiki wote walilipuka kwa furaha na mayowe.
Baada ya kumaliza, Msechu aliulizwa na Jaji Juliana; Msechu ni Juliana yupi huyo unayemzungumzia? aliuliza Juliana huku akiwa ameweka shingo upande na kuonyesha kuguswa na ujumbe wa Msechu.
Kwa kujiamini, Msechu alijibu ni Wewe. Jibu lililofanya Jaji Ian aangue kicheko.
Kwa ushindi huo, Mganda Davis amejinyakulia kitita cha zaidi ya sh milioni 30, sambamba na kujipatia mkataba wa kurekodi albamu na kampuni kubwa huko Afrika ya Kusini.
Hata hivyo, kwa ushindi huo watu mbalimbali walionekana kushikwa na simanzi huku wengine wakipinga matokeo hayo wakiwemo waliokuwa wakifuatilia katika mitandao, Mwanasiasa kijana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alikuwa mmoja wa watu walioonyesha furaha zao kwa hatua ambayo Msechu amefikia na kumpongeza.