Msechu 'kachakachuliwa' Tusker Project? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msechu 'kachakachuliwa' Tusker Project?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Rutashubanyuma, Dec 7, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Msechu 'kachakachuliwa' Tusker Project?


  na Andrew Chale


  [​IMG] KILE kitendawili cha atakayenyakua taji la Tusker Project Fame 2010 kiliteguliwa juzi baada ya Mganda Davis kuibuka kidedea huku mshiriki wa Tanzania Peter Msechu akiambulia nafasi ya pili. Tangu kuanza kwa shindano hilo ambalo lilikuwa likirushwa kila wiki na kituo cha TBC1, Msechu alionekana kung’ara vilivyo hadi kufanikiwa kuingia hatua ya fainali.
  Hata hivyo, awali kulikuwa na tetesi za shindano hilo kuingiliwa na itikadi za kisiasa, huku baadhi ya Watanzania wakilalamikia ‘kuchakachuliwa’ kwa kura zao walizokuwa wakimpigia Mtanzania huyo.
  Hata hivyo, katika fainali hizo Msechu aliibuka nafasi hiyo ya pili, baada ya kupambana vilivyo hadi kufikia hapo kwa nyimbo zake ambazo ziliweza kuteka mashabiki wengi.
  Msechu ambaye alipewa nafasi kubwa kushinda, alikuwa akishangiliwa kila alipopanda jukwaani na kukonga vilivyo mashabiki, huku akiwa anatumbuiza na msanii raia wa Burundi, Kidumu ambaye walirandana vilivyo.
  Wakati wa kutumbuiza mmoja mmoja, Msechu aliimba wimbo wa ‘Nipate Nafasi’ ulioimbwa na gwiji wa zamani Ahmad Kipande, ambapo aliweza kuongeza vionjo vyake huku akimsifia mtoto Juliana, ambaye anasema tangu aende Kenya alitokea kumpenda.
  Lakini alishindwa kusema na ameamua kumwambia mbele za watu, “…Juliana naumiaaaaa” ndio kilikuwa kiitikio cha wimbo huo na mashabiki wote walilipuka kwa furaha na mayowe.
  Baada ya kumaliza, Msechu aliulizwa na Jaji Juliana; “…Msechu ni Juliana yupi huyo unayemzungumzia?” aliuliza Juliana huku akiwa ameweka shingo upande na kuonyesha kuguswa na ujumbe wa Msechu.
  Kwa kujiamini, Msechu alijibu ni ‘Wewe’. Jibu lililofanya Jaji Ian aangue kicheko.
  Kwa ushindi huo, Mganda Davis amejinyakulia kitita cha zaidi ya sh milioni 30, sambamba na kujipatia mkataba wa kurekodi albamu na kampuni kubwa huko Afrika ya Kusini.
  Hata hivyo, kwa ushindi huo watu mbalimbali walionekana kushikwa na simanzi huku wengine wakipinga matokeo hayo wakiwemo waliokuwa wakifuatilia katika mitandao, Mwanasiasa kijana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alikuwa mmoja wa watu walioonyesha furaha zao kwa hatua ambayo Msechu amefikia na kumpongeza.  [​IMG]
   
 2. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mi naona it was a fair play,davis mkali jamani,ni kweli msechu kakua sana frm wat he was in bss to wat he is now.but davis bado yuko juu
   
 3. M

  MZEE SERENGETI JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Binafusi naona Mchakato ulikuwa sawa kabisa,Davis kashinda hakuna uchakachuaji wowote ulio fanyika.Hongere Davis hongere Msechu.
   
 4. F

  Fikra Pevu Senior Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuchakachuliwa. Ukimsikiliza Davies vizuri utakubali anamzidi Msechu. LAKINI Nampongeza Msechu kwa umahiri katika Stage Perfomance.
   
 5. p

  posh77 Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabongo bwana kila kitu kinachakachuliwa?mimi sikubaliani na hilo kabisa davis mkali na alistahili,msechu nae yuko vizuri lakini hakumshinda davis,all in all wote ni washindi ila kwa sababu haiwezekani wote kushika namba moja basi davis alipaswa kushika namba moja na msechu namba mbili,big up msechu umetuwakilisha vizuri.
   
 6. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Jamani dogo Msechu yuko tight...!! Mi namkubali sana kijana yule, anaujua muziki vilivyo, habahatishi..!! Ukiona anavyoweza kuchezea nyimbo za watu na kuweka vionjo vyake, utakubali bila ubishi. Kama kuna mdau mwenye clip ya juzi, aiweke jamvini watu tuburudike..!! Ilikuwa sooooooo...!!
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  UONGO, UONGO

  [​IMG]
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
   
Loading...