MSD washindwa kusambaza reagents za kupima HIV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MSD washindwa kusambaza reagents za kupima HIV

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzito Kabwela, Aug 11, 2011.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kushangaza na kusikitisha jiji la mwaza linakabiliwa na hali mbaya baada ya Mamlaka inayohusika na usambazaji wa Dawa nchini kushindwa kusambaza dawa na vifaa vya kupimia virusi vya ukimwi katika hospitali zote za jiji la Mwanza. Makundi kadhaa ya watu hasa vijana kwa zaidi ya wiki moja sasa wamekuwa wakienda kwenye vituo vya kupimia bila mafanikio.

  Inasadikiwa kuwa MSD hawana stock ya hizo dawa ambapo hilo limetokana na ufinyu wa bajeti kwenye wizara ya afya. Wote wanaotaka kupimwa wanashauriwa kwenda hospitali ya SEKOU TOURE au Bugando.
  Nawasilisha
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Pesa za global fund zimetumikaje?maana hakuna wizara inayofisadiwa ki ulaini kama afya na misitu!
   
 3. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mzito Kabwela, MSD wanajulikana kwa uzembe uliokithiri na bahati Mbaya madaktari walioimgia Bungeni wa,eshindwa kulisemea kwa nguvu suala hili. Hata hivyo kinachotokea sasa hivi kuhusiana na kukosekana kwa vipimo (test kits) za HIV wa kulaumiwa ni Wizara ya Afya kwa kuwa wao ndio hununua hizi test kits kwa hela kutoka GLOBAL FUND FOR MALARIA, TB and AIDS(GFTAM).

  Habari za uhakika ni kuwa GFTAM hawakuipa serikali fedha za Round 10 kutokata na wizara kutoa ripoti isiyoroshisha ya matumizi pamoja na makosa mengine ya kiutendaji. tattizo hili limeanza kuanzia mwezi wa Oktoba mwaka jana, na mikoa iliyoathirika sana ni Kanda ya ziwa kwa kuwa huko ndio kuna population kubwa na prevalence ya UKIMWI iko juu, approx 7%.

  Sasa wahanga wakubwa ni kina mama wajawazito ambao ni muhimu wajua hali zao ili kama wameathirika wapewe dawa za kuwakinga watotot watakaowazaa (PMTCT) Ndugu, hili ni suala kubwa, na ni jambo ambalo waziri anapaswa alitolee taarifa kwani maelfu ya kina mama wamekosa kujua hali zao na statistically, unaweza kusema ni watoto wangapi ambao tungeweza kuwazuia kuambukizwa HIV tumewakosa! Ukieelewa hii vizuri, INAUMA SANA!
   
 4. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,353
  Likes Received: 2,405
  Trophy Points: 280
  Nasikia kale kamkurugenzi kake kanakula 20m/= + per month!
  Kwa biashara gani? Wakati hili ni shirika la umma!
  Haya mambo ndio yanayowafanya watu kupata ma ban kwa kusema ma frustrations yao humu ndani!
   
Loading...