nimesikitika sana kuona vituo vya kutolewa huduma za afya kukosa dawa kizembe hivi. Me ni mjumbe wa kamati ya afya ya zahanati iliyopo kijiji kimoja ndani ya mkoa wa manyara.hapa zahanati kwangu kulikuwa na ukosefu wa dawa kwa muda mrefu kiasi kwamba watu walikosa imani na serikali yao.
Leo niliitwa kwa ajili yakupokea dawa zilizoletwa na gari la MSD. Katika eneo hilo kulikuwa na wagonjwa ambao walikuja matibabu wengi mno. gari hili lilileta matumaini makubwa sana kwa wagonjwa na watoa huduma maana walisema ukosefu wa dawa sasa basi kwa sababu kipindi cha nyuma serikali ilishatangaza kuwa imetoa pesa za kutosha kwenye akaunti zaa kila kituo kwa ajili ya bohari ya dawa (MSD) kuwanunulia dawa. miezi ya nyuma vituo hivi vilikuwa havipati dawa kwa sababu ya kutokuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kununulia dawa na vilikuwa vinaandikwa kwenye sales invoice zao kuwa kituo hakina fedha za kutosha kwa ajili ya kununulia dawa na kweli vituo vilikosa dawa. kwa bahati mbaya tena walisisitiza tuzibandike kwenye mbao za matangazo.
kinachonisikitisha leo baada ya kupokea dawa niliangalia sales invoice zao tumeletewa dawa zenye thamani ya shs 293,500/= nikamuliza daktari kuwa dawa ulizoletewa zinatosha? daktari alinihesabia kuwa amociline moja tu. vingine vyote ni blaablaa .
Nikaendelea kumhoji daktari kuwa kama kweli aliagiza dawa kutosha? kweli nilihakikisha kwa macho yangu dawa ziliagizwa zenye thamani ya shs 2,320,000/=kwenye kitabu kimoja kimeandikwa FOMU 2A: TAARIFA NA MAOMBI YA DAWA MUHIMU NA VIFAA HUSIKA VYA TIBA KWA ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA. . nikasema kulikoni..... nikamuliza kuna karatasi ulilopewa imeandikwa statement of account iko wapi? kuiangalia kituo kina salio lenye thamani ya tshs 3,980,000/=matumaini yangu yaliishia hapo....... matumaini ya watoa huduma pia yaliishia hapo...... wanasema msd tumeshawazoea......
Wagonjwa walikosa matumaini yakupata dawa katika kituo chao chakutolea huduma za afya. Mara nyingi tulikuwa tunawashambulia watoa huduma kuwa wanauza dawa.... kumbe tatizo lipo kwingine.hivi kweli MSD mmeshindwa kuhudumia wananchi?
serikali imetoa fedha na akaunti ina salio la shs 3,980,000/= dawa zilizoagizwa kwenye hiyo fomu ya kuagizia dawa zina thamani ya shs 2,320,000/= MSD inaleta dawa za 293,500/=ambazo ni sawa na asilimia 7.4. kwa hiki kituo.tutafika kwa hali hii? nimekosa kabisa imani na MSD. ninaiomba serikali na waziri wa afya kama me ni mwongo kw hili waje wafanye audity upya waangalie kila akaunti ina shs ngapi na wangalie pia MSD wameleta dawa za shilingi ngapi?.
Vielelzo ninavyo vyakulinda ukweli huu. pia naishauri wizara badala ya kuweka fedha kwenye akaunti za vituo ambavyo MSD wanayafaham. fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti ya vituo ili tuweze kuagiza dawa kama tunavyofanya kwa fedha ICHF na vingine. vinginevyo tutaendelea kuilaumu serikali, wizara na wewe waziri wa afya.
Nimeumia sana wananchi walioniomba kusimamia huduma zao kama mjumbe wa kamati kuona wanakosa dawa kizembe hivi. natamani nijiuzulu uongozi huu...nimemaliza na ujumbe wangu umewafikia wote hata MSD kama watakwepo humu