canular
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 858
- 813
Wakuu bila Shaka wote muwazima ,naomba niende moja Kwa moja ktk mada husika, jaman MSD fuatilieni hili suala.
Iko hivi hapa Serengeti kuna Mzee mmoja ni pharmacia wa Wilaya, akiwa na timu yake huyu Mzee amefungua famasi nyingi tu za kutosha sasa basi amekuwa akichukua dawa na vifaa tiba kutoka MSD na kuvifanyia biashara ikiwemo, magodoro ya hospital, dawa kama artesunate inakwanguliwa maandishi yote ya not for sale alafu inauzwa kama kawaida.
Ni kwamba vitu ni vingi anavyoiba huyu mzee anajiita Nyabutika (jb) pia kuna AC imefungwa pale duka lake kubwa linaloitwa green light pharmacy ni mali ya serikali ile nayo amehujumu na kingine kwakuwa ana mamlaka anafungia wafanyabiashara ya madawa kwa kivuli kuwa hayana vigezo alafu anafungua maduka yake, fuatilia mji mzima wa Mugumu ni yeye ndio mwenye duka kila kona ya mji watu wamekosa pa kusemea.
Kwa sababu Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi amewaweka kiganjani unaambiwa imeshatolewa amri Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wakifika pale wapewe huduma yoyote wanayohitaji bure kabisa pasipo kulipizwa hela yoyote ndio maana anakuwa na kiburi na wizi wa mali za umma na pia ofisini hakai muda mwingi yupo kwenye maduka yake unakuta mtu unatoka kijijini mbali kwenda kuchukua dawa na vifaa vinavyohitajika kituoni kwako ukifika hukuti mtu alafu ukimpigia simu aje kukupa vifaa vinavyohitajika kituoni anakujibu hovyo. Suala jingine upande wa bima nao anahusika yeye pia
Mzee huyu achunguzwe tatizo wakaguzi mkienda huwa mnapewa maneno na virushwa ila hamchunguzi inavyotakiwa mkitaka kujua maozo ya huyu Mzee nendeni kila duka lake lilipo mfanye ukaguzi wa maana na msisahau kwenda kwenye godown yake anayotunzia madawa mtabaini mengi. Jamani wahusika wa MSD fuatilieni hili mnawaumiza wana Serengeti mnaleta madawa wenye mamlaka zao wanachukua na kuyaweka kwenye biashara zao.
Sorry kwa atakaye kwazika Ila ukweli ndio huo ana maduka mpaka kijiji kimoja kinaitwa natta kule kuna magodoro Mali ya serikali yametunzwa tu ndani