MSD: Hamna dawa zilizopo njiani kutoka MSD kwenda Muhimbili tokea 2012

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.JPG

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.


Bohari ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.

Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.

"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.

Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.

Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.

Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.

Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.
 
Hii nchi bana ...kwani CAG hakuwaandikia MSD hizo queries ili kupata management response? Kama walishindwa kujibu ipasavyo wao ndio jipu ....
 
Watanzania siku tukiacha ujinga tutaendelea..
Walikuwa wapi kuwapa nyaraka wakati wa ukaguzi...??
Mkuu hapo zimepikwa fasta ili kuokoa jahazi lisizame! Ila mwanzoni vitabu vya Muhimbili vinaonesha hizo dawa hazijapokelewa, je hizi kumbukumbu amezitoa wapi kama sio za kupika?
 
waandishi wa habari ndio wakaguzi angepeleka iyo taharifa huko ofisi za CAG ndio wao waseme na si kuita waandishi wa habari...
 
Kwanza mwenyewe kasema hazikuenekana Muhimbili kama zimepokelewa kwasababu ilibidi wasaini (delivery) sasa kama haipo CAG asemaje? si zipo njiani bado mpaka watakapo saini asee...
 
"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.

Ni sawa na kusema nililipa lakini sina risiti, sasa sisi tutajuaje? Ndio maana tuna utaratibu, usipofuatwa kutakuwa na anarchy
 
Km zilipokelewa na hazikuwekwa kwenye hesabu ya muhimbili zilienda wapi km sio zilipitiliza kwengine maana km kweli zilifika na hazikuonekana kwenye vitabu ina maana vifaa na dawa halisi muhimbili vingeonekana vimezidi ukilinganisha na kwenye vitabu vyao
 
Limekaribia kufika. Hahaaa..hahaa. hii picha sijui nani aliitengeneza.
 

Attachments

  • IMG-20160427-WA0000.jpg
    IMG-20160427-WA0000.jpg
    32.8 KB · Views: 43
Siku zote nilikua namuona huyu jamaa kuwa ni kilaza fulani. Sasa hivi ndiyo nimepata uhakika kuwa ni bonge la KILAZA.
Maelezo yoote aliyotoa yamesaidia kuthibitisha kilichoandikwa kwenye report ya CAG.
 
Hilo dili kati ya Mhimbili na MSD. Kilichotikea ni Mhimbili walisau kufuta kumbukumbu zinazoonesha waliangiza sawa.
Kwa hiyo kati ya hao wawili yaani Mhimbili na MSD mmoja anamruka mwezeke. Ili ukweli ufahamike kwa sasa kumbukumbu za Mhimbili ndizo zihesabike ni sahihi. Kama MSD walipele basi Mhimbili waseme dawa na vifaa tiba hivyo hilifika wapi. Atayepatika na kosa awajibike kwani alikuwa anaficha taarifa hebu kushiriki kwenye wizi au ufisidi. Kama Anna Kilango aliwajibishwa kwa nini hao nao wasiwajibishwe.
 
Hapo Mchezo umekwisha.
Muhimbili watajifanya zilifika, wanatafuta orodha feki kwa waliowahi kufika kutibiwa kuanzia 2012 mtapewa magonjwa ya Figo kwenye Mafaili yenu muonekane mliuguwa Migonjwa ya hizo dawa halafu mkapewa mkatumia Mkapona,

kama wanavocheza dili kwny Bima za Afya, unatibiwa then unaambiwa saini kabla hawajaorodhesha dawa ulizopewa, ukisaini tu, wanakujazia Migonjwa yote ya zile dawa walizopiga, Busha, TB, Upungufu wa Damu, Homa ya ini n.k

Majipu aliyonayo Mgonjwa wetu yatakauka kwa kumnywesha Sumu tu Mgonjwa mwenyewe!
 
Mbona swala ni dogo tu, Muhimbili hizo dawa hazipo hata kama nyie mlizitoa bado kauli zake zinadhibitisha hivyo.
Muhimbili (Receiver) ndio walitakiwa kuja na document kuonyesha kuwa dawa wanazo na zilifika na CAG (namkubali sana) katundanganya. Wewe unaweza kuzituma lakini uliowatuma wakakimbia nazo au wakazihujumu.
Bado kwa kauli hizo CAG yuko sawa tu
 
Back
Top Bottom