Msanii wa Nigeria Burna Boy amejumuishwa katika orodha ya wanamuziki ambao album yake itakayochezwa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa Joe Biden

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
Kwanza unaweza kufikilia inakuwaje asichukuliwe mwanamuziki wa Marekani au mataifa mengine yaliyoendelea, pili ni kiasi gani cha pesa analipwa mwanamuziki huyo kutoka Afrika ya kaskazini?

Burna boy -Nigeria singer.jpg

Lakini ni kwamba orodha ya nyimbo zipatazo 46 zimeandaliwa katika sherehe ya kuapishwa kwa Biden, taarifa za ndani zimesema.

Msanii wa Nigeria Burna Boy amejumuishwa katika orodha ya wanamuziki ambao album yake itakayochezwa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden.

Nyimbo ya Burna kwa jina Destiny itakuwa miongoni mwa nyimbo za wasanii wengine wa kimataifa.

"Wasanii na nyimbo zilizochaguliwa ujumuisha taswira ya kila mmoja nchini Marekani, hii inafungua ukurasa mpya na kusaidia kuleta watu pamoja wakati utawala wa Biden na Harris unao anza kazi yake muhimu ya kuunganisha taifa hilo.

Nyimbo nyingine zilizochaguliwa ni pamoja na wasanii wakubwa kama Beyoncé na nyimbo yake Find Your Way Back, Kendrick Lamar na Mary J. Blige‘s na wimbo wao Now Or Never, Bob Marley na Wailers na nyimbo yao Could You Be Loved pamoja na Levitating hit ya Dua Lipa

Source:
BBC Swahili
 
Vizuri kwake maana mama yake yupo busy kumtafutia deals wakati wa kwetu mama yake yupo busy kumpatia mababa wapya
Wakati mwingine tusilaumu ujue hata shule ya uzeeni inasaidia sana, sasa mtu hana hata mshale unategemea nini?
 
Tukiwaambia wasanii wa Tz acheni kuimba matusi ooh mashabiki ndio wanataka, haya wenzenu wanazidi kupasua anga tu, tena hawaombi wao ndio wanamuomba, Go Burna Goooooooooo.

Ukisikiliza hiyo ngoma ya Destiny na ile Monsters you made daaah jamaa ana focus sana na kazi yake.
 
Vipi yule msanii wetu ambae mpaka sasa anatambulishwa baba zake wapya jee yy hayumo
Moja ya scandal ya kipuuzi sana kwa yule dogo, japo inasadikika mama ana programu katika maendeleo ya dogo but afrika tunaendelea kuwa black continental kwa taswira ya watu 'muundo wa hicho kizee'
 
Wasanii wetu kwa sasa wanakula tu mafao yao waliyo vuna miezi michache iliyopita. Baada yaa hapo ni kupigika na kulialia tu mpaka 2025!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom