Msanii wa Filamu "GABO" apata ajali

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,375
MWIGIZAJI wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo' amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Kiwalani jijini Dar. Kwa mujibu wa chanzo makini, Gabo aliyekuwa katika gari binafsi, aligongana na gari lingine na kupata jeraha mguuni hivyo kulazimika kulazwa kwa takriban wiki tatu kisha kuruhisiwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Mwigizaji wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo'

Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutoka hospitali, Gabo aliyeitendea haki Sinema ya Majanga ya Mahsein Awadh ‘Dk Cheni', alieleza mazingira ya ajali. " Nilikuwa naendeshwa na rafiki yangu lakini ghafla tukagongana uso kwa uso na gari lingine, nashukuru magari hayakuumia sana lakini mimi nililazwa kwa wiki tatu kutokana na jeraha nililolipata mguuni, " alisema Gabo.

attachment.php
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom