Msanii wa CHADEMA aliyehongwa na CCM awatosa

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Msanii Mapunda aitosa CCM




na Agnes Mlundachuma



MSANII wa muziki wa Kiafrika, Fullgency Mapunda 'Mwana Cotide' ameamua kujitoa katika bendi ya Tanzania One Theatre inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na kujivua uanachama wa chama hicho baada ya kushindwa kumtekelezea mahitaji yake kulingana na makubaliano.
Mwana Cotide, ambaye awali alikuwa akifanya sanaa binafsi na pia uhamasishaji katika shughuli mbalimbali za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amefikia uamuzi huo baada ya kutolipwa mshahara wake kwa miezi mitatu kwa madai ya kuchunguzwa kwa madai kuwa ni mpinzani.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, iliyopatikana jana jijini Dar es Salaam, na nakala yake kusambazwa kwa Katibu Mkuu wa CCM na Mkurugenzi wa TOT Plus, Kapteni John Komba, anaeleza kuwa alijiunga na CCM, Agosti 28, mwaka jana kwa sharti la ujira mnono na kukabidhiwa kadi namba AB 1621644 na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, wakati huo, Kapteni Jaka Mwambi.

Mwana Cotide alisema Oktoba 6 mwaka jana, aliajiriwa na TOT akiwa kama msanii msaidizi chini ya Kapteni Komba, kwa barua yenye kumbukumbu namba CCM/PT36 155/5 akiwa na ngazi ya mshahara wa CMWK2M ambao ni sh 310,000.

Msanii huyo aliongeza kuwa, lakini hajawahi kulipwa mshahara tangu kipindi hicho, hivyo kuamua kubwaga manyanga.

"Ninajitoa CCM kwa kuwa msingi wa mimi kujiunga na chama hicho ulikuwa ni ajira na si sera wala itikadi, kwa kuwa wamekiuka makubaliano yetu nimeamua kujitoa rasmi, sharti letu lilikuwa ajira nono na huo ndio ukweli ambao Sekretarieti ya CCM inautambua," alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na sababu hizo na nyingine nyingi ambazo atazieleza baadaye anajitoa katika chama hicho
.
 
Ndugu yangu Asha ahsante kwa mtundiko, lakini inaonekana unakata issue ilhali tayari umeshaegemea upande mmoja, je unadhani kunajadilika jambo kwa ukweli bila ya kuwa bias?
 
haitoshi kujitoa TOT na CCM aende mahakamani.

a. Hakuna sheria inayomkata mpinzani kujiunga na bendi ya TOT au ya chama chochote kama ipo sheria hiyo ni ya kibaguzi na ni kinyume na Katiba.

b. Kama alikubaliwa ujira na yeye alifanya kazi yake kama ilivyotakiwa basi hakuna mtu anayeweza kuzuia mshahara wake, kwani ujira wa kazi siyo hisani ya muajiri bali ni haki ya mwajiriwa.

c. Akienda mahakamani badala ya kudai hizo laki tisa na ushee, adai gharama za usumbufu, kutwezwa, kudhalilishwa na kunyanyaswa ambayo yote tukiiweka kwenye gharama za fedha ni kama shilingi milioni 300 na kuomba mahakama itoe adhabu kwa waajiri kama TOT ili iwe fundisho.. !

d. Awasiliane Lissu haraka iwezekanavyo na kama kuna makubaliano yoyote nje ya mahakama yasipungue shilingi milioni 50!!
 
haitoshi kujitoa TOT na CCM aende mahakamani.

a. Hakuna sheria inayomkata mpinzani kujiunga na bendi ya TOT au ya chama chochote kama ipo sheria hiyo ni ya kibaguzi na ni kinyume na Katiba.

b. Kama alikubaliwa ujira na yeye alifanya kazi yake kama ilivyotakiwa basi hakuna mtu anayeweza kuzuia mshahara wake, kwani ujira wa kazi siyo hisani ya muajiri bali ni haki ya mwajiriwa.

c. Akienda mahakamani badala ya kudai hizo laki tisa na ushee, adai gharama za usumbufu, kutwezwa, kudhalilishwa na kunyanyaswa ambayo yote tukiiweka kwenye gharama za fedha ni kama shilingi milioni 300 na kuomba mahakama itoe adhabu kwa waajiri kama TOT ili iwe fundisho.. !

d. Awasiliane Lissu haraka iwezekanavyo na kama kuna makubaliano yoyote nje ya mahakama yasipungue shilingi milioni 50!!

Mwanakijiji

Hili sakata linasura nyingi. Huko nyuma gazeti la UHURU lilitoa picha kwamba huyu msanii alikuwa anatumbuiza kwenye kongamano la wanavyuo katika siku ya wanafunzi duniani lililoandaliwa na CHADEMA. Wakati huo tayari alishaingia CCM toka miezi mingi kabla. Labda ndio maana waliamua kumsimamisha. Inaelekea huyu jamaa alihongwa na CCM lakini bado mapenzi yake yalikuwa kwa CHADEMA. Na kwenye mahojiano alikiri kuwa CCM walimhonga fedha zaidi ya hiyo ahadi ya mshahara. Tukio hili linaweza kuwa ushahidi wa wazi wa jinsi ambavyo CCM inanua wapinzani.

Asha
 
Kuna mtu anaweza kumkataza Muislamu kuingia kanisani na kusali kama anajisikia hivyo, au nini kitamkataza Mkristu ambaye ameamua kwenda na rafiki yake Muislamu kuswali na akafuata mambo yote? Mkatoliki akienda kusali kwa Mlutheri basi atimuliwe?

Kama alikuwa ameajiriwa na Chadema na wakati huo huo ameajiriwa na CCM basi kuna wezekana kuwepo mgongano wa aina fulani lakini kama ameajiriwa na CCM (Kazi) na mapenzi yake ni Chadema hakuna kosa as long as kwamba alipokuwa anafanya shughuli za CCM alizifanya jinsi wanavyotaka na siyo kuzisabotage.. sijaona hilo..
 
Kuna mtu anaweza kumkataza Muislamu kuingia kanisani na kusali kama anajisikia hivyo, au nini kitamkataza Mkristu ambaye ameamua kwenda na rafiki yake Muislamu kuswali na akafuata mambo yote? Mkatoliki akienda kusali kwa Mlutheri basi atimuliwe?

Kama alikuwa ameajiriwa na Chadema na wakati huo huo ameajiriwa na CCM basi kuna wezekana kuwepo mgongano wa aina fulani lakini kama ameajiriwa na CCM (Kazi) na mapenzi yake ni Chadema hakuna kosa as long as kwamba alipokuwa anafanya shughuli za CCM alizifanya jinsi wanavyotaka na siyo kuzisabotage.. sijaona hilo..

Mwanakijiji

Umesewa vizuri. Lakini hebu jaribu kufikiri, Msanii ameajiriwa kuimba CHADEMA tuwachane tuwatupe kama amavyoimba Komba. Halafu msanii huyo huyo anakutwa akiimba jukwaa lingine kuwa CCM ni Chama Cha Mafisadi

Asha
 
Bi. Asha.. kazi ni kazi hasa kama ni kazi halali! Kama walimchukua msanii huyo ili kumzima na yeye akakubali akijua kuwa anapokea rushwa ili kunyamaza basi kama hayo ni makubaliano alikuwa na haki ya kutimiza makubaliano hayo.

Siyo ajabu katika ulimwengu wa biashara, watu kujaribu kuibiana vipaji. Na ni kweli katika mikataba ya sisi wengine unaambiwa kabisa wakati uko katika ajira hii huwezi kufanya, kutoa ushauri n.k bila kuijulisha kampuni yako na bila ya baraka zao.

Unless huyo msanii alikuwa na kitu kinamkataza kwenye mkataba kujihusisha, kuonekana, n.k katika majumuisho ya wapinzani hatakuwa amevunja sheria yoyote. Kama yote alikuwa nayo na alijua alitakiwa kufanya hivi au vile basi wanauwezo wa kumfukuza.

Hata hivyo, hayo yote hayahusiana na yeye kulipwa malipo yake kwa miezi yote hiyo kama alifanya kazi aliyotakiwa kufanya. Mshahara wa mtu siyo hisani au huruma!
 
Bi. Asha.. kazi ni kazi hasa kama ni kazi halali! Kama walimchukua msanii huyo ili kumzima na yeye akakubali akijua kuwa anapokea rushwa ili kunyamaza basi kama hayo ni makubaliano alikuwa na haki ya kutimiza makubaliano hayo.

Siyo ajabu katika ulimwengu wa biashara, watu kujaribu kuibiana vipaji. Na ni kweli katika mikataba ya sisi wengine unaambiwa kabisa wakati uko katika ajira hii huwezi kufanya, kutoa ushauri n.k bila kuijulisha kampuni yako na bila ya baraka zao.

Unless huyo msanii alikuwa na kitu kinamkataza kwenye mkataba kujihusisha, kuonekana, n.k katika majumuisho ya wapinzani hatakuwa amevunja sheria yoyote. Kama yote alikuwa nayo na alijua alitakiwa kufanya hivi au vile basi wanauwezo wa kumfukuza.

Hata hivyo, hayo yote hayahusiana na yeye kulipwa malipo yake kwa miezi yote hiyo kama alifanya kazi aliyotakiwa kufanya. Mshahara wa mtu siyo hisani au huruma!


"NINAJITOA CCM kwa kuwa msingi wa mimi kujiunga na chama hicho ulikuwa ni ajira na si sera wala itikadi, kwa kuwa wamekiuka makubaliano yetu nimeamua kujitoa rasmi, sharti letu lilikuwa ajira nono na huo ndio ukweli ambao sekretarieti ya CCM inautambua."
Hii ni kauli iliyotolewa wiki hii na msanii wa muziki wa Kiafrika, Fulgence Mapunda (Mwana Cotide), akieleza hatua yake ya kujiengua kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni mmoja wa 'maelfu' ya wanachama wapya waliojiunga na CCM kwa mbwembwe katika mwaka uliopita.
Ni tunda mojawapo la jitihada za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, katika kuongeza idadi ya wanachama na kuimarisha chama.
Mapunda alikuwa mmoja wa mavuno ya CCM; bidhaa iliyonunuliwa kutoka upande mwingine ili kudhoofisha upinzani na kuijenga CCM.
Ni ushahidi mwingine kwamba CCM imekuwa 'inawanunua' wanachama kwa pesa na ahadi nono, ingawa mara kadhaa imeambiwa hivyo, na imekana.
CCM imekuwa inatumia shida za watu kujinufaisha kisiasa. Wakati mwingine, ni vema kusema kwamba imekuwa inasababisha hali duni ya maisha ya wananchi, ili iyatumie hayo hayo kuwanunua.
Huyo ni mmoja. Amekuwa jasiri na kusema walichokubaliana. Huyo ni mmoja, hakutekelezewa ahadi yake. Amerejea 'uraiani.'
Wapo wengi wa aina hiyo ndani ya CCM, walionunuliwa kwa ahadi nono lakini hazijatekelezwa. Wamo waliotekelezewa kiasi, lakini bado wananung'unika chini chini.
Tukitaka tunaweza kuwataja hapa. Kwa kuwa ni wengi, tutawataja wale wanaosikika wakilalamika mara kwa mara juu ya 'kutotendewa haki' na CCM. Vyovyote jamii inavyowaona, nao tutawatetea, wapewe haki zao.
Wamo kina Tambwe Hizza, Thomas Ngawaiya na Shaibu Akwilombe.
Katika kundi la kina Mapunda yumo pia Amani Kabourou. Yamo mamia ya walalahoi wa Tanga na Kigoma na kwingineko, walioitikia wito wa Makamba.
Tofauti ya Kabourou na Mapunda ni moja. Kabourou aliwabana mapema, akapewa alichotaka.
Kinachowaunganisha wote hawa, kama alivyosema Mapunda ni njaa. Urafiki wao wa ghafla na CCM haukujengwa katika sera wala itikadi.
Mioyo yao haiko na CCM. Akili zao haziko na CCM. Uhusiano wao na CCM umejengwa katika tumbo.
Maana yake nini? Watu wa namna hii si msaada kwa CCM. Wana haki ya kuwa popote wanapotaka, wakati wowote; lakini haituzuii kusema kwamba wanatangatanga. Na kwa kuwa mioyo na akili zao havimo ndani ya CCM, viko pengine.
Sasa tumuulize Makamba. Kama hii ndiyo mbinu yake ya kuongoza chama, anadhani CCM ina muda gani kabla ya kuangushwa na wale wale walio ndani yake?
Makamba anaweza kuwaeleza wana CCM kwa nini anatumia pesa nyingi za chama kupandikiza wapinzani wa chama chao miongoni mwao?
Wana CCM wana haki ya kuhoji matumizi ya pesa za chama katika ununuzi wa wanachama bandia, wakati wamo wanachama halali na waaminifu wa muda mrefu wanaendelea kusota lakini wanaendelea kukitetea chama chao.
Wamuulize Makamba, kwa mfano, inawezekanaje watumishi wa CCM walipwe mshahara wa sh 30,000 kwa mwezi, huku chama kikiwa tayari kumlipa 'mamluki' mmoja sh 300,000 kwa mwezi?
Inawezekana Makamba haoni kwamba sh 300,000 ni nyingi, kwa kuwa kiasi hicho wala hakitoshi kwa gharama ya vocha za simu yake kwa wiki moja!
Hakitoshi kwa mafuta ya gari lake kwa mwezi! Kiasi hicho hicho ni kidogo ya kile anachojilipa kwa siku moja kama masurufu ya safari anapokuwa nje.
Anajua si nyingi kwa kuwa CCM inapata takriban sh 1,000,000,000 kutoka serikalini kama ruzuku kila mwezi. CCM ina miradi mingi nchi nzima, vikiwamo viwanja vyetu vya michezo ambavyo imeshindwa kuviendesha.
Hakika, kama kuna chama kinapaswa kuwa tajiri ni CCM. Lakini kimeshindwa kutawala miradi yake, ukiwamo mradi mkuu wa Shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania (SUKITA).
Anapokuwa anawanunua kina Mapunda, Makamba anajiona mjanja. Lakini lipo jambo moja la dhahiri.
Ununuzi huu wa wanachama ni ishara kwamba CCM inakufa. Nguvu yake sasa imebaki katika pesa na hadaa.
Sasa ona, hata huyu walimuahidi masilahi manono, wameshindwa kumtimizia! Na ni wale wale wanaojitapa kuwa chama chao kinatimiza ahadi zake kwa wananchi milioni 40!
Laiti Watanzania milioni 40 wangekuwa jasiri kama Mapunda huyu, yangesemwa mengi, na ungekuwa mwanzo mpya wa siasa za Tanzania.
Vile vile, huu ni ushahidi mwingine wa tuhuma dhidi ya CCM kuhusu ununuzi wa kura wakati wa uchaguzi ili wapate ushindi wa kishindo!
Bahati mbaya ni kwamba baadhi ya hawa wanaonunuliwa hawasemi hadi yanapowakuta mambo kama haya yaliyomkuta msanii Mapunda.
Kwa muda sasa, na hili limekuwa zaidi katika Serikali ya Awamu ya Nne, pesa imekuwa ndiyo sera na itikadi ya CCM.
Nguvu pekee waliyobaki nayo ni pesa. Wanakoitoa wanajua wenyewe. Na ndiyo maana yalipoibuka mambo ya ufisadi Benki Kuu ya Tanzania, yakihusisha pia makampuni hewa yaliyoundwa na kuchota pesa kipindi cha uchaguzi, halafu yakafutwa usajili mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, wenye akili walijua kwa nini tangu awali serikali ilikataa Bunge kuunda tume huru ya kuchunguza ubadhirifu huo.
Sasa wamechunguza moja ya kumi ya ubadhirifu wa Benki Kuu, na tayari gavana amefukuzwa kazi.
Kama wangechunguza ubadhirifu mzima, si ajabu hata serikali ingepinduliwa! Na hili ndilo waliloogopa, kwani walijua nani anahusika wapi, hata kabla ya wapinzani kutangaza hadharani tuhuma zao.
Nasema sera na itikadi ya CCM (na serikali sasa) ni pesa. Ndiyo hiyo inayotembezwa kila kona, si kununua tu wanachama, bali hata watu wenye taaluma zinazoweza kutumika vema kuijengea CCM sifa nzuri mbele ya umma.
CCM mnakazania kutufundisha siasa za kununiana na kuuzana. Inatufundisha ufisadi. Imeacha kuwafundisha wanachama wake siasa, imeacha sera na itikadi. Sasa inawafundisha ufisadi!
Haya yanaturejesha kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, hayati Horace Kolimba, na mmoja wa wanachama wa muda mrefu wa chama hicho, Joseph Butiku.
Miaka zaidi ya 10 iliyopita Kolimba alisema CCM imepoteza dira na mwelekeo. Kuna kitu alikiona. Kabla hajawasaidia kukirekebisha chama chao, wakamweka kiti moto, akapoteza uhai.
Mwaka jana, mzee Butiku ameibuka na kurejea kauli ile ile ya Kolimba. Akasisitiza kwamba CCM imepoteza mwelekeo. Wakambeza, lakini wakaogopa kumchukulia hatua.
Tunao mashahidi wengi walio hai, ndani na nje ya CCM wanaoyasema haya. Hatuwezi kuwapuuza. Hata hatua na kauli hii ya Mapunda, vinaingizwa katika kumbukumbu.
Pole pole, tutaanza kukubaliana kwamba CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuf Makamba ni CCM ya ufisadi. Tafuta tafsiri yoyote ya ufisadi. Huu ununuzi na uuzaji wa binadamu wenzetu ni ufisadi wa viwango vyake.
Ni mbinu mpya ya kuwatumia binadamu wenzao. Ni udhalilishaji na utumwa! Na ipo siku Makamba na wenzake watatueleza kwa nini wanaendeleza 'biashara ya utumwa' katika siasa za Tanzania.
ansbertn@yahoo.com +447828696142 www.ngurumo.blogspot.com
 
Mwanakijiji kwa kweli mungu awrehemu kama imefikia stage hii duh hakika tunapoelekea ni pabaya,,,,jamani hata kwenye uchaguzi unambiwa wkaileta hela kula kura unaruhusiwa kupiga unaemtaka bila kuangalia aliekup hela ,,,
 
Hili ni fundisho na changamoto kwa Mwakatobe au Paparazi Muwazi .Hii ndiyo CCM .Wanacheka juu akina JK lakini mambo yao chini kwa chini .
 
nimemuona huyo msanii...ccm wamefanya kitu kibaya sana kumtumia sanaa yake anayoitegemea kumpatia kipato...kitapeli .

ukweli ni kuwa baada ya makamba kuitambua kazi yake ya uhamasishaji alianzimia kumuiba ili atumike kwenye kazi kama hizo ccm..alimnyakua kwa ahadi ya TSH milioni 5..ALIMPA TASLIMU NA MSHAHARA KAMA ALIOUTAJA....ILA KATIKA VITABU VYA KUMBUKUMBU CCM JAKA MWAMBI ALIRIPOTI KUWA ALITUMIA ..TSH MILIONI 25 ..KWA KAZI YA KUMNUNUA HUYU MSANII WA CHADEMA...TSH MILIONI 20 WAMEGAWANA NA MAKAMBA AU INAWEZEKANA JAKA ALIZITIA KWAPANI ZOTE...KWA HIYO WANA CCM MJUE HUU MRADI MAKAMBA NA SEKRETARIAT YAKE KUNUNUA WAPINZANI KWA GHARAMA NA KUWAPA KIDUCHU ...UNAGHARIMU SANA...NASHAWISHIKA KUAMINI KUWA CCM WANA PESA ZA MAFISADO NDIO MAAANA WANAZITUMIA HOVYO NAMNA HII...

TAARIFA NI KUWA TAARIFA ZOOTE ZA NAMNA CCM INAVYONUNUA WAPINZANI .,PRICE TAGS ZAO...[WALIZOLIPWA NA ZILIZODAIWA KUTUMIKA ] WAPINZANI WANAZO ,,..NA SIKU YOYOTE WATAZIMWAGA...

....MFANO MTU KAMA HIZA PESA ZILIZOTOLEWA KUMNUNUA NI MILIONI 40[SIJUII YEYE KAPEWA NGAPI??} AKWILOMBE MILIONI [KAPEWA MILIONI 3 TU]..WOTE WALIPEWA NA AHADI ZA AJIRA....KABOUROU ALIPEWA 30 MILIONI CASH...[NADHANI MAKAMBA ALIPEWA ZAIDI KWA KAZI HIYO]..NA PIA AKAAHIDIWA KAZI NONO....

KWA KWELI SASA HIVI KUNA NYETI NYINGI MNO....X FILES ZIPO WAZI..KULIKO WAKATI WOWOTE WA UHAI WA TAIFA LETU....INAONEKANA KILA IDARA SASA KUNA WAZALENDO WALIOCHOKA!!!!
 
Duuuu??? kaaazi kweli kweli, yaani milioni 40? kubadili tu itikadi ya chama?? wakati mama wajawazito mammia kwa mamia wanapoteza maisha kila siku kwa kukosa chandarua na mlo kamili kwa siku??

Nimeisha sema jamani, CCM kaputi, inacho jua ni kuwekeza kwenye siasa tu ili waendeleee kutawala na wachache kujineemesha, haitumikiii wananchi katu!
 
Kuna mtu anaweza kumkataza Muislamu kuingia kanisani na kusali kama anajisikia hivyo, au nini kitamkataza Mkristu ambaye ameamua kwenda na rafiki yake Muislamu kuswali na akafuata mambo yote? Mkatoliki akienda kusali kwa Mlutheri basi atimuliwe?

Kama alikuwa ameajiriwa na Chadema na wakati huo huo ameajiriwa na CCM basi kuna wezekana kuwepo mgongano wa aina fulani lakini kama ameajiriwa na CCM (Kazi) na mapenzi yake ni Chadema hakuna kosa as long as kwamba alipokuwa anafanya shughuli za CCM alizifanya jinsi wanavyotaka na siyo kuzisabotage.. sijaona hilo..

Hebu tuache masuala ya uanachama au imani, tuzungumzie ajira yenyewe. Ubaguzi wa ajira haupaswi kuwepo, naweza nikawa mwana-CCM na bado nikaajiriwa kwenye bendi ya CHADEMA and vice versa. Ilimradi nitimize majukumu yangu ya kuimba. Na hata shule za kikristo zinaajiri waalimu waislamu, alimradi anafundisha vizuri hiyo physics, history etc na kuzingatia masharti ya kazi, hata mimi mkristo nilishawahi kufundisha kwenye shule ya kiislamu mwaka mzima na hakuna aliyezungumzia dini yangu hata siku moja. Majuzi nimepata habari kuwa headmistress wa hiyo shule sasa hivi ni mkristo mlokole. Mambo yanapaswa kuwa hivyo.

Sasa hicho hao TOT walichomfanyia huyo kijana msanii ni ubaguzi wa dhahiri, mosi, na pili ni unyanyasaji kumnyima mtu mshahara wake wakati kazi yake ameifanya. Hata kama ni kumchunguza mtu (wengine tunaita probation), katika kipindi hicho anapaswa kulipwa mshahara na stahili zake zote. Hakuna excuse ya kumnyima mtu mshahara ati bado unamchunguza! Achukue hatua za kisheria huyu kijana, hao jamaa wakome kabisa tabia hiyo ni mbaya na ni ufisadi mwingine!
 
Bado nangoja kujua Gwandumi karudi CCM kwa kiasi gani maana alitupwa nje kama mbwa aliyekula mboga .

Kwa mkasa huo huo wa kuwanunua ndiyo maana Tambwe kashindwa kupata kura kuanzia wilayani hadi Dodoma .Ila uzuri ni kwamba kapewa eneo la tenda na BET pale Sabasaba ana supply sijui nini vile anakamua na hiyo pesa nyingine aliyo pewa kuhama CUF so anaganga njaa sasa .
 
wakati makamba anahangaika kuhonga wanasiasa wa upinzani..wale wana ccm wa kweli amabao wameajiriwa wanalia njaa njaa ..
 
Halafu ukiangalia CCM THINK Tank wanaorubuni wapinzani hawana thinking capacity ya maana. Kwanini umuhonge mtu ambaye kuondoka kwake Upinzani hakuleti ATHARI zozote?
Naungana na wengine kwanini utumie X millions kuhonga watu wakati wangetumia hizo pesa kuijenga MIOYO ya Watanzania kuwajengea MIUNDO MBINU mbalimbali..hospitali,shule, vifaa muhim huko, barabara...masoko ya wamachinga etc...Manyuzi na wenzako badilikeni...
 
Msanii wa CHADEMA aliyehongwa na CCM awatosa Msanii Mapunda aitosa CCM

MSANII wa muziki wa Kiafrika, Fullgency Mapunda 'Mwana Cotide' ameamua kujitoa katika bendi ya Tanzania One Theatre inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na kujivua uanachama wa chama hicho baada ya kushindwa kumtekelezea mahitaji yake kulingana na makubaliano.


Heshima mbele mkuu Asha,

Kichwa cha habari mkuu hakifanani na habari yenyewe, exactly effect yake ndani ya CCM na kutoka kwake kweli unaweza kusema ni worthy hiku kichwa cha habari?

2. amefikia uamuzi huo baada ya kutolipwa mshahara wake kwa miezi mitatu kwa madai ya kuchunguzwa kwa madai kuwa ni mpinzani.

Okay, this makes a sense tena a big one kwa sababu huyu hakulipwa mshahara wake on time, ni matatizo ya ajira na malipo lakini sidhani kuwa ni ya national politics, na pia huwa yanatokea upinzani na CCM pia, mara kwa mara na yanaishia kutatuliwa, wapiga mziki ni kawaida yao kuhama hama, Hamza Kalala "Komandoo" alipotoka bendi ya UV-CCM alisema sana haya maneno na kuingia kupigia upinzani, na sasa amerdui tena bendi ile ile ya UV-CCM,

kuna ishus nyingi sana za taifa jamani ila this one is not one of them, kama ni argument, ni kwamba binafsi nimeisikia sana kwamba Komba, ana tabia ya kuchota hela za CCM na kuzitumia kwa faida yake huku CCM brass wakifumbia macho, hilo tayari sasa linazungumzwa sana ndani ya CCM na limeshamfikia Muungwana, najua it a matter of time, maana ninajua for a fact kuwa kwenye uchaguzi wa Tunduru, mkuu huyu alipewa shillingi millioni 50, akaishia kuzila zote bila kuwapa wenziwe, huku akiwanunulia watoto wake magari na kumfanyia mtoto wake mmoja harusi ya kifahari sana ambayo hailingani na uwezo wake Komba kipesa, hilo lipo na limshafika kwa wanohusika wakuu,

Lakini la huyu kijana kutoka, not a national political ishu please, ni mwanamuziki kuhama bendi moja kwenda nyingine, tusiikuze sana bila sababu, najua TOT inakaribia kufanana na BOT kwa jina, lakini please TOT ni bendi tu ya kuburudisha wananchi kwa muziki.

Ahsante Wakuu!
 
..nakubaliana na wewe mkuu..lakini national issues hapa ni pesa nyingi za watanzania kutumika kununua mamluki..ambao hawana mapenzi na chama..wakati kuna njia za kisomi za kujenga chama kikubwa kama ccm ..kinachoheshimika afrika....

si halali hata kidogo..kama sekretarieti ya chama chini ya makamba imeishiwa mbinu ...iondoke...ni aibu!!
 
unawezekana mtu ukawa umeajiriwa kwengine na mapenzi yako yako kwengine.

yawezekana kwamba alifanya kazi chadema kama volunteer :) na hakupokea mshahara kwa maana hiyo hajavunja mkataba wake na ccm.
 
Yangu mimi ni Macho .Ila najua hata kama JK kapata habari kwake ni sawa maana CCM kwa JK ni namba moja zaidi ya Tanzania na Watanzania we all know that hata wewe Mzee Es unajua .Kipimo cha Utaifa wa CCM kwa mara ya mfululizo ni issue ya BOT baada ya kushindwa ya Buzwagi .
 
Back
Top Bottom