Msanii wa bongo flavor timbulo anacopy nyimbo za x-maleya wasanii wa camroon

Halafu kuna mijinga hapa inayo sisitiza tuwaenzi wasanii uchwara wa bongo.
huyu jamaa afungwe gerezani kwa wizi.
sasa unakuta mwenzie katumia vyombo halisi halafu yeye kaiga kutumia beats zao za kitoto!

Hawa wakameroon wakistukia na ku-msue dogo sijui itakuaje maana nyimbo mbili daa huu ni wizi kabisa wa kazi zao
 
Shingongo haijamfikia habari hii...

Shigongo anajua sema nae dogo ni miongoni mwa wale wasanii walioko kwenye payroll yake(kuleta kashafa za mapenzi za uongo wauze magazeti ya shigongo kwa malipo)
 
Taratibu jamani......
Mwancheni dogo naye atusue. Maadamu remix zake zinabamba, sioni shida. Hata MwanaFA walisema anatafsiri nyimbo za Fedrostar, lakini tunaona hadi leo ni mkali. Hata T.I.D kwenye Nyota Yako tunajua ilikuwaje.

Lakini mbona kucopy nyimbo hata mamtoni kupo, tumesahau mkasa wa Haiti, akina Jimmy Fox, Wyclif Jean, Lionel Richie na wenzake akina Celin Deon wameimba wimbo wao. Na ktk kundi kubwa lote ni Lionel Richie pekee aliyekuwa kwenye original version ya wimbo ule.

Mbona tunawabania madogo, au tunataka waingie vichochoroni wakafanye ujasiriamali wa roba za mbao? Let's be serious. Mi dogo namkubali.

Nilikua namkubali ila kwa hili kaniangusha sana haikatazwi hyo style yake maybe manager wake kawalipa x-maleya kwa kuzifanyia remix nyimbo zao kama ni hvyo sion tatizo ila sidhani,,,,kajitahidi sana kuzichakachua ana kipaji cha copy paste
 
kesho wafu fm ina mhoji tena kagusia ishu hii ya kuiba nyimbo za watu,kwahiyo majibu yatapatikana kesho.
 
hiyo ngoma wa leo wa kesho naikubali sana!!!kacopy ila kajitahidi kutufikishia ladha sisi tusiowasikiliza wanamuziki wa cameroon
 
mwalimu huyo wa english medium school,ambaye umaalufu wake unapanda kwa kasi amekili leo ku copy nyimbo zake kali waleo wa kesho na domo langu zito
amesema alikua anatafuta style ya kumtambulisha vyema,sasa ameipata hivyo basi ataendelea na style hiyo
amesema amefanya mawasiliano na wale jamaa wenye original version,na wamemkubali soon atafanya nao ngoma.
Amesema fans wake waendelee kumsupport wasikatishwe tamaa na maneno ya watu.
Source: clouds.
 
tuwapende wasanii wetu,yeye sio wa kwanza kuigilizia nyimbo za watu,katoa mfano wa wimbo 'malaika' umeimbwa na watu kibao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom