Msanii Rashid Makwiro "Chid Benz", amshauri Makonda "Boresha Segerea ukute pazuri ukienda"

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,929
2,000
Sikuwa namtilia maanani sana msanii huyu awali lakini baada ya kumsikiliza nimegundua ana akili sana tofauti na wanavyo mchukulia watu wengi.

Mwishoni mwa mahojiano yake katoa ushauri Kwa Makonda aache kujiingiza mambo mengi yasiyo maana ikiwemo wasanii Kwa kutaka wamsifie wakati wao wanataka hela tuu.

Ajikite mambo ya maana ikiwamo kuboresha hata Segerea kwani yeye au hata Magufuli kama kuna waliyotenda Kwa makosa sasa wajue wataenda kule hivyo waboreshe makazi yao.

Ujumbe murua, Ila waweza kubezwa


=======


Ni mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania. Maarufu ‘Chidi Benz’. Kwa miaka kadhaa Chidi amekuwa alama ya waathirika wa dawa za kulevya.

Chidi ni kielelezo cha anguko la vijana maarufu wenye kutumia mihadarati. Hata hivyo, hivi karibuni alizungumza mambo ambayo kimsingi yalipaswa kujadiliwa na Bunge.

Kuna kipande cha video kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kikimwonesha Chidi katika mahojiano na chombo kimoja cha habari. Katika video hiyo, anamshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kujielekeza katika masuala ambayo yanahusu nafasi yake.

Chidi anasema Paul Makonda amekuwa akijielekeza kwa wasanii ili wamsifie na kuacha mambo yenye kuhusu cheo chake. Anabainisha kuwa mwisho, wasanii huhitaji wapewe pesa. Akishafeli kwa wasanii, watu watampima kwa yale atakayokuwa ameyafanya kama mkuu wa mkoa.

Akatolea mfano kushughulikia suala la wafanyabiashara wa soko la Karume, upangaji wa vitu ili watu na magari yapite vizuri, akazungumzia kuhusu hali za vituo vya polisi na magereza, kwamba Makonda anatakiwa kwenda na kuangalia wanaowekwa mahabusu na wafungwa wanaishije na wanalala vipi huko?

Chidi alisema mazingira ya magereza yanatakiwa kuboreshwa kwa sababu hali ni mbaya. Alifafanua kuwa watu hujisahau, lakini yeye ameshalala mahabusu na waliokuwa mawaziri, kwa hiyo jela anaweza kwenda yeyote, akiwemo Makonda.

Ni hoja ya bungeni

Alichokizungumza Chidi ni hoja nzito ya bungeni. Amezungumza kwa lugha rahisi yenye kueleweka kwa kila mtu. Kwamba watu hujisahau kuwa jela anaweza kwenda yeyote.

Mtaani kuna msemo kuwa wanaokwenda jela siyo wote wana hatia. Wengi tu wanabambikiwa kesi. Hii imekuwa lawama kwa mahakimu na majaji kuwa miongoni mwao hawatendi haki. Fikiria asiye na kosa, amesingiziwa kisha anakwenda kukutana na mateso saa 24 maisha yake yote.

Hili linapaswa kueleweka; katika nchi huru, watu kwenda jela haitakiwi liwe jambo la kufurahia. Isipokuwa ni uamuzi wenye kuchukuliwa kwa hisia kali ili kuwanyima uhuru wale ambao wanahatarisha uhuru wa wengine. Ile adhabu ya kuwanyima uhuru ni tosha sana. Uhuru ni hitaji la msingi kwa kila binadamu. Hivyo, kwa yeyote mwenye akili timamu, anapofungwa hujutia makosa yake na kufunguka kifikra kwamba anahitaji kuwa raia mwema.

Hata hivyo, Uamuzi wa kupeleka watu jela unatakiwa kufanana na ule wa mzazi anapomwadhibu mtoto wake pendwa. Unakuta mzazi anadondosha chozi lakini hana namna, anatakiwa kufanya jambo ili mwanaye awe mtu bora.

Bunge kama chombo cha uwakilishi, kinapaswa kushughulikia kero za magereza. Watu hawawezi kulala kama wapo kwenye nyumba zao, lakini hawapaswi kulazwa kama mahindi ghalani.

Jela hukutanisha watu wa hovyo kabisa na wengine ni wazuri kuliko waliobaki mitaani. Inatakiwa wale wazuri walindwe na ikiwezekana wao ndiyo wafanye ‘maambukizi’ ya kitabia kwa wengine. Haitakiwi jela liwe eneo ambalo watu wa hovyo wanakuwa na mamlaka ya kuwadhuru wengine na hata kuwafanyia vitendo visivyo vya kibinadamu.

Kuna hili lisipuuzwe

Februari 8 mwaka huu, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi aliipinga hoja ya kuwakutanisha wafungwa na wapenzi wao kwa ajili ya tendo la ndoa, akisema kitendo hicho cha kijamii siyo cha lazima.

Wafungwa kutembelewa faragha na wenzi wao ilipitishwa kwenye nchi nyingi ili kusaidia kulinda ndoa za wafungwa na kuziwezesha familia zao kisaikolojia kuona bado wapo pamoja kipindi chote cha ufungwa hadi wanapoachiwa huru.

Inatakiwa magereza yawe na vyumba maalumu kwa wafungwa wanandoa kukutana kama nchi nyingi zinavyofanya au mfungwa kupewa likizo kwenda nyumbani kukutana na mkewe kama Urusi inavyofanya. Uamuzi wa kujenga mazingira bora gerezani unatakiwa uzingatie kuwa jela si jehanamu. Wanaokwenda kule ni utaratibu wa kikatiba kuwa wakosefu waende wakajifunze na kujutia makosa yao kukosa uhuru. Izingatiwe kuwa jela si mahali pa kukomoana, kwani anaweza kwenda yeyote.
 

Ramadhan James

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
1,928
2,000
Hakika nami nimejifunza nimebadili mtazamo wangu, nilidhani ameharibika kiasi hicho wanachosema kumbe la. " ....Aboreshe kule Segerea, Watu wamebanana wanalala wengi, kule tunalala na Mawaziri, kuna mawaziri kule. Watu wanajisahau kwamba hata Magufuli akimaliza muda wake anaweza akaenda kama ana matatizo ni bora uboreshe kama unajua sio kila unachofanya ni jema" - Chid Benz
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Sikuwa namtilia maanani sana msanii huyu awali lakini baada ya kumsikiliza nimegundua ana akili sana tofauti na wanavyo mchukulia watu wengi.
Mwishoni mwa mahojiano yake katoa ushauri Kwa Makonda aache kujiingiza mambo mengi yasiyo maana ikiwemo wasanii Kwa kutaka wamsifie wakati wao wanataka hela tuu.
Ajikite mambo ya maana ikiwamo kuboresha hata Segerea kwani yeye au hata Magufuli kama kuna waliyotenda Kwa makosa sasa wajue wataenda kule hivyo waboreshe makazi yao.
Ujumbe murua, Ila waweza kubezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Watamfuatilia kama mrundi na akikaa vibaya atatekwa
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,099
2,000
Sikuwa namtilia maanani sana msanii huyu awali lakini baada ya kumsikiliza nimegundua ana akili sana tofauti na wanavyo mchukulia watu wengi.
Mwishoni mwa mahojiano yake katoa ushauri Kwa Makonda aache kujiingiza mambo mengi yasiyo maana ikiwemo wasanii Kwa kutaka wamsifie wakati wao wanataka hela tuu.
Ajikite mambo ya maana ikiwamo kuboresha hata Segerea kwani yeye au hata Magufuli kama kuna waliyotenda Kwa makosa sasa wajue wataenda kule hivyo waboreshe makazi yao.
Ujumbe murua, Ila waweza kubezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaamua kujilipua.... Kaongea kitu ambacho wengi wasingewaza kuongea hata kwa mtutu wa binduki

Jr
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,083
2,000
Dua la kuku hilo kwa mwewe, muulizeni kwanza madawa kaacha?
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,952
2,000
nasikia mbowe kashamtayarishia tundu lisu selo ya kukaa segerea siku akirudi bongo
Uwezekano wa viongozi wa awamu hii kwenda Segerea siku zijazo ni mkubwa sana. Unapokuwa na sh 2.4 trillion au zimepotea au zimetumika bila vielelezo au zimetumika bila kuidhinishwa, ni lazima kwa vyovyote vile, kuna watu siku za mbeleni, hata kama si kesho, lazima watakuja kushtakiwa.

Akina Mramba walishtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuidhinisha mikataba ya pesa kidogo sana ukilinganisha na hii ya matrillion ya sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom