Msanii na mwanaharakati Kala Pina ajiunga na CCM na kujitoa CUF.

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,323
29,584
Habari zenu.
Leo msanii mkongwe wa hip hop na mwanaharakati ajulikanae kama Kala Pina, leo amejiondoa chama cha CUF na kujiunga na CCM.
Kala Pina alishiriki leo katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa ccm ndugu Mtulia na kusema kuwa anajiunga na CCM baada ya kuona juhudi za rais JPM katika kutetea maslahi ya taifa.

Source: TBC habari.

Kweli JPM ni chaguo la Mungu. Mpaka kufika 2020, wenye kujielewa wote watakuwa upande wa JPM.
 
kalapina 2015 aligombea ubunge kinondoni kupitia Act

acha upotoshaji
Nimeweka hivyo kama nilivyoona ktk source. Sio maneno yangu!
Kwani mbona Nyalandu 2015 aligombea kama sisiemu? Tatizo liko wapi hapo, acha kukariri.
 
aliwah kuendesha harakati gan mpaka akaitwa mwanaharakati?
Wewe ni mgeni naona.
Jamaa anapambana na vijana wanaotumia madawa ya kulevya, anapambana kuwasaidia 'kutoka' ktk matumizi ya hayo madawa pia anaelimisha jamii madhara yake.
 
Habari zenu.
Leo msanii mkongwe wa hip hop na mwanaharakati ajulikanae kama Kala Pina, leo amejiondoa chama cha CUF na kujiunga na CCM.
Kala Pina alishiriki leo katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa ccm ndugu Mtulia na kusema kuwa anajiunga na CCM baada ya kuona juhudi za rais JPM katika kutetea maslahi ya taifa.

Source: TBC habari.

Kweli JPM ni chaguo la Mungu. Mpaka kufika 2020, wenye kujielewa wote watakuwa upande wa JPM.
Mnatuchefua na hizo hadisi. Tunataka kusikia Tanzania imezindua chombo cha kuingia mbingu za mbali au imerusha majaribio ya nyuklia au imezindua uundwaji wa ndege. Hayo ya kujiunga na ccm ni njaa vinatusaidia nini???? Umasikini ni laana
 
Mnatuchefua na hizo hadisi. Tunataka kusikia Tanzania imezindua chombo cha kuingia mbingu za mbali au imerusha majaribio ya nyuklia au imezindua uundwa wa ndege. Hayo ya kujiunga na ccm ni njaa vinatusaidia nini???? Umasikini ni laana
Wewe umekalia tu benchi na uko physically fit, unategemea wenzako pekee walete utakacho, hovyo kabisa.
Change your mentality.
 
Back
Top Bottom